Tuweka mihemko pembeni, Hezbollah kapigwa kachakaa, pona yao ni Biden kuinyima Israel silaha kulazimisha cease fire

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Wiki iliyopita Bunge la marekani lilipiga kura kwa ushindi mkubwa kufuta katazo la kuiuzia Israel Silaha lakini haikuwa hivyo kwa Rais, Biden ana presha kubwa sana ya kutafuta chochote cha kujisifia kwa siku 60 alizobakiza, Alimwambia Netanyahu akubali kustop mashambulizi lasivyo hamuuzii silaha, Netanyahu kwa uchungu imebidi akubali, Biden anajisifia kwenye vyombo kasitisha vita lakini ni kwa siku 60 tu, Baada ya hapo Trump kipenzi cha Israel akiapishwa atafuta katazo

Nawaona Hezbollah wanashangilia hii cease fire, Kwa hizi facts utawaona ni matahira:

Uongozi mzima wa juu wa Hezbollah ulisambaratishwa, ni aibu kubwa sana leadership kuwa vulnerable kiasi hiki, Nasrallah alikuwa anajificha kudhani hawajui alipo lakini kilichomkuta kitabaki kwenye vitabu vya historia.

1732795465390.png

Shambulio la Pagers - Hili shambulizi la mwaka, Ni mchanganyiko wa Supply chain attack na Cyber attack, Hezbollah 1,200 waliobeba pagers walifumuliwa viuno na vilivyomo ndani ya mifuko

1732796283426.png

Israel imeweza kuidhoofisha ngome kuu ya Hezbollah - Lebanon ya kusini ilikuwa ngome kuu ya Hezbollah, Kwa mara ya kwanza kwa kipindi kirefu, Jeshi la Lebanon limediriki kwenda kulichukua eneo hili, hapo kabla jeshi la lebanon walikuwa kama waangalizi wa nyumba lakini muda huu wanarudi kuwa wamiliki wa nyumba, hawakuwa na nguvu yoyote mbele ya Hezbollah, walikuwepo Lebanon ya kusini lakini kwa uchache na waliwekewa masharti na Hezbollah wasithubutu kuingilia mambo yasiyowahusu, Ni baada ya Israel kuidhoofisha ngome hio ndio wameweza kupata ujasiri wa kuchukua maeneo hayo na kuwashambulia Hezbollah.

1732796544761.png
 
Hata Hizbollah ingepewa silaha na Super Power Mzito kama Marekani basi Israel ingechakaa
Hezbollah hawana uwezo wa kununua ndege za bilioni 200, achilia mbali gharama za maintanance

Hezbollah hawana uwezo wa kumodify, Israel akinunua hizo ndege anatoa vitu vingi anaweka vyake.

Silaha nyingi Israel ananunua, ni silaha chache sana anapewa.

Huo msaada wa dola bilioni 3 za silaha wanaopewa Israel ni mdogo sana, Kwa mwaka huu uchumi wao umeshuka lakini ni Dola bilioni 500 (Zaidi ya shilingi trilioni moja na nusu) kusanya nchi zote afrika mashariki na kati hazigusi
 
Wamechakazwa sana! Ndo maana wamekuwa laini kupata hii fursa ya kustisha mapigano. Walikuwa wanapumulia mashine hata boss wao Iran ameshukuru usitishaji mapigano kutokea.

Israel kasema anaconcentrate kwa Hamas na Iran
 
Kwa Israeli ni wazi in short run waliweza kuwadhibiti hawa jamaa ila kwa mahesabu ya long-run israel ingeishia kupata hasara maana kuna mahali israeli wameanza kuchemka,unajua kuwapiga hawa izbolah siyo jambo jepesi inahitaji mikakati ya mda mrefu sasa kuuwa viongoz siyo mkakati unaoweza kubadili hali ya vita hato kidogo ,kubwa ni kuua miundo mbinu yote ya adui inayompa nguvu ya kufanya mashambulizi hilo israel ameshindwa kabisa,yan kiufup bora tuu wamekaa mezani pamoja,kwa upande wa izbolah nao hawana Cha kujivunia maana hata wao malengo yao ya kuipiga tafu Hamas mpaka mwisho hayakutimia kwa haraka kama walivyodhani hivyo hii ngoma ni kati hakuna mshindi
 
Uongozi mzima wa juu wa Hezbollah ulisambaratishwa, ni aibu kubwa sana leadership kuwa vulnerable kiasi hiki, labda kama hujui maana ya uongozi

View attachment 3164352

Shambulio la Pagers - Hili shambulizi la mwaka, Ni mchanganyiko wa Supply chain attack na Cyber attack, Hezbollah 1,200 waliobeba pagers walifumuliwa viuno na vilivyomo ndani ya mifuko

View attachment 3164357

Kwa mara ya kwanza kwa kipindi kirefu Jeshi la Lebanon Linaingia Sehemu za Hezbollah - Baada ya cease fire jeshi la Lebanon limeanza kuingia maeneo ya Lebanon ya kusini ilikuwa ngome ya Hezbollah, Ni baada ya jeshi la Israel kuwashughulikia Hezbolah

View attachment 3164364
Kwenye asymetrical warfare israel ndio kachapwa kwa kuwa objective za Netanyahu ni kurudisha masettler north kwa nguvu za kijeshi hilo amefeli viongozi wa hizbullah kuuliwa hio ndio vita soldiers die ili taasisi iendeleee kusimama na their home front iwepo watu walijua wakifanya decapitation things will fall apart ila wapi taasisi imara huendelea kusimama imara hii hizbullah wameonyesha kuwa wao ni taasisi imara despite kuwa faced na entire western intelligence na adui yao kupewe all kinds of support ila vita imeisha kwa makubaliano amani na sio kwa kusign surrender agreement ,world equation of power is shifting midege mikubwa na mimeli mikubwa ni anasa tu vidrone vidogo tu na makombora vinaleta mageuzi makubwa sana ktk uwanja wa mapambano.
 
Uongozi mzima wa juu wa Hezbollah ulisambaratishwa, ni aibu kubwa sana leadership kuwa vulnerable kiasi hiki, labda kama hujui maana ya uongozi

View attachment 3164352

Shambulio la Pagers - Hili shambulizi la mwaka, Ni mchanganyiko wa Supply chain attack na Cyber attack, Hezbollah 1,200 waliobeba pagers walifumuliwa viuno na vilivyomo ndani ya mifuko

View attachment 3164357

Kwa mara ya kwanza kwa kipindi kirefu Jeshi la Lebanon Linaingia ngome za Hezbollah - Baada ya cease fire jeshi la Lebanon limeanza kuingia ngome za Lebanon, Hii yote ni baada ya jeshi la Israel kuwadhoofisha Hezbollah

View attachment 3164364
Hezbollah ni Chama cha siasa na kundi la kijeshi, kuua viongozi wao wa siasa si kuwashinda kwenye medani ya Vita.

Hebu niambie kama unaongea bila bias yoyote IDF wamefanya nini ground invasion yao Lebanon? Miezi 2 wamepiga hatua kieneo kidogo cha kilomita 7 tu, kila wakisonga mbele wanapewa kichapo wanarudi,

Israel hana Tabia ya kutangaza wanajeshi wake wanao kufa ila Lebanon tumeona Mamia ya Viongozi wakubwa wakubwa wa kijeshi Vyeo kama Luten, colonel, staff etc wakitangazwa kufa.

Tumeona Reserve wa Jeshi la Israel wakilazimishwa kureport jeshini mpaka wengine kujiua kwa kukataa kwenda, it's not coincidence walikua wakipukutika.

Israel kapigwa Lebanon, walishindwa nini kusubiria Trump aingie Madarakani kama tatizo ni Biden?
 
Israel hajafikia objective zake za kijeshi. Kashindwa kuwasukuma Hezbollah nyuma ya mto Litani, kashindwa kuanzisha military buffer zone hata moja ndani ya Lebanon, kashindwa kumaliza missiles za Hizbollah. Alijaribu kuua viongozi wake, lakini makamanda wengine washachukua nafasi.

Wakati huohuo, Hizbollah iliendelea kutwanga makombora ndani ya Israel, wakazi maelfu kwa maelfu wa Israel kaskazini hawajarejea makwao

KIUFUPI kama Israel ingekuwa inashinda Usingesikia kuitishwa kusitishwa mapigano, Lakini Hizbollah nayo inachapa, Israel kupitia marekani wakaona wajaribu kutafuta ushindi wa mezani ambao wameshindwa kuupata katika uwanja wa mapambano
 
Kwa Israeli ni wazi in short run waliweza kuwadhibiti hawa jamaa ila kwa mahesabu ya long-run israel ingeishia kupata hasara maana kuna mahali israeli wameanza kuchemka,unajua kuwapiga hawa izbolah siyo jambo jepesi inahitaji mikakati ya mda mrefu sasa kuuwa viongoz siyo mkakati unaoweza kubadili hali ya vita hato kidogo ,kubwa ni kuua miundo mbinu yote ya adui inayompa nguvu ya kufanya mashambulizi hilo israel ameshindwa kabisa,yan kiufup bora tuu wamekaa mezani pamoja,kwa upande wa izbolah nao hawana Cha kujivunia maana hata wao malengo yao ya kuipiga tafu Hamas mpaka mwisho hayakutimia kwa haraka kama walivyodhani hivyo hii ngoma ni kati hakuna mshindi
Miundo mbinu mingi wameweza kuiharibu ndio maana jeshi la Lebanon kwa mara yakwanza kwakipindi kirefu limepata ujasiri wa kwenda kwenye ngome zao, kungekuwa na miundombinu imara wasingethubutu.
 
Israel hajafikia objective zake za kijeshi. Kashindwa kuwasukuma Hezbollah nyuma ya mto Litani, kashindwa kuanzisha military buffer zone hata moja ndani ya Lebanon, kashindwa kumaliza missiles za Hizbollah. Alijaribu kuua viongozi wake, lakini makamanda wengine washachukua nafasi.

Wakati huohuo, Hizbollah iliendelea kutwanga makombora ndani ya Israel, wakazi maelfu kwa maelfu wa Israel kaskazini hawajarejea makwao

KIUFUPI kama Israel ingekuwa inashinda Usingesikia kuitishwa kusitishwa mapigano, Lakini Hizbollah nayo inachapa, Israel kupitia marekani wakaona wajaribu kutafuta ushindi wa mezani ambao wameshindwa kuupata katika uwanja wa mapambano
Alieitisha kusitishwa mapigano ni Biden tena kinyume na Bunge lake lililomkataza,

Israel kaweza kuisambaratisha Lebanon ya kusini kwa kiasi kikubwa, hii ni ngome kuu ya Hezbollah, Jeshi la lebanon kwa mara ya kwanza kwa kipindi kirefu imepata ujasiri wa kwenda kusimamia hayo maeneo
 
Hezbollah hawana uwezo wa kununua ndege za bilioni 200, achilia mbali gharama za maintanance

Hezbollah hawana uwezo wa kumodify, Israel akinunua hizo ndege anatoa vitu vingi anaweka vyake.

Silaha nyingi Israel ananunua, ni silaha chache sana anapewa.

Huo msaada wa dola bilioni 3 za silaha wanaopewa Israel ni mdogo sana, Kwa mwaka huu uchumi wao umeshuka lakini ni Dola bilioni 500 (Zaidi ya shilingi trilioni moja na nusu) kusanya nchi zote afrika mashariki na kati hazigusi
Hizi data ziliisha kuwa debunked humu. Na kama una Abcd za uchumi utaelewa huo Uchumi mkubwa ni wa kupewa.

Chukulia mfano huu rahisi.

Wewe una mtaji wa laki 1 kuuza Genge, unapata faida 10% kila mwaka. Nije mimi nakusaidia laki 1 kwa mwaka.

Baada ya Miaka 10 zile laki 1 zitakua zime accumulate na kuwa milioni 1 + faida yako mtaji wa Genge utakuwa zaidi ya milioni 1, after miaka 20 mpaka 30 utakuwa na mtaji kama milioni 5, je mtu akija kusema una milioni 5 na hela laki 1 unayopewa kila mwaka ni kidogo tu mtaji wako wa milioni 5 ni mkubwa atakua sahihi?

Israel Anapewa $3B na Usa ya silaha kila mwaka, keyword ni msaada wa Kijeshi ambao una accumulate kwenye uchumi wao, hawapewi tu misaada ya kijeshi bali misaada ya kiuchumi na sector nyengine. Jumla so far misaada Israel aliyopewa na Usa ni $310B hio ni Usa pekee hapo ongezea na Ulaya na Nchi nyengine washirika tunaongelea Figure zaidi ya $400B, kuwa na Uchumi wa $500B na umepewa misaada zaidi ya 75% ya huo Uchumi is nothing to be proud of.
 
Alietisha kusitishwa mapigano ni Biden tena kinyume na Bunge lake lililomkataza,

Israel kaweza kuisambaratisha Lebanon ya kusini kwa kiasi kikubwa, hii ni ngome kuu ya Hezbollah, Jeshi la lebanon kwa mara ya kwanza kwa kipindi kirefu imepata ujasiri wa kwenda kusimamia hayo maeneo
Tupe ushahidi wowote kwamba Israel kaweza kuisambaratisha Lebanon ya Kusini.
 
Kwa mara ya kwanza kwa kipindi kirefu jeshi la Lebanon limeenda kusimamia Lebanon ya kusini na kuwazuia Hezbollah, ni baada ya Israel kkufanya yake
 
Miundo mbinu mingi wameweza kuiharibu ndio maana jeshi la Lebanon kwa mara yakwanza kwakipindi kirefu limepata ujasiri wa kwenda kwenye ngome zao, kungekuwa na miundombinu imara wasingethubutu.
Ni kweli mkuu ila bado mashambulizi mengi ya hizbolla yamekua Kila uchwao ,hali hii imeweka mashaka juu ya miundo mbinu hiyo kushambuliwa na kudhibitiwa kama inavyotakiwa
 
Hizi data ziliisha kuwa debunked humu. Na kama una Abcd za uchumi utaelewa huo Uchumi mkubwa ni wa kupewa.

Chukulia mfano huu rahisi.

Wewe una mtaji wa laki 1 kuuza Genge, unapata faida 10% kila mwaka. Nije mimi nakusaidia laki 1 kwa mwaka.

Baada ya Miaka 10 zile laki 1 zitakua zime accumulate na kuwa milioni 1 + faida yako mtaji wa Genge utakuwa zaidi ya milioni 1, after miaka 20 mpaka 30 utakuwa na mtaji kama milioni 5, je mtu akija kusema una milioni 5 na hela laki 1 unayopewa kila mwaka ni kidogo tu mtaji wako wa milioni 5 ni mkubwa atakua sahihi?

Israel Anapewa $3B na Usa ya silaha kila mwaka, keyword ni msaada wa Kijeshi ambao una accumulate kwenye uchumi wao, hawapewi tu misaada ya kijeshi bali misaada ya kiuchumi na sector nyengine. Jumla so far misaada Israel aliyopewa na Usa ni $310B hio ni Usa pekee hapo ongezea na Ulaya na Nchi nyengine washirika tunaongelea Figure zaidi ya $400B, kuwa na Uchumi wa $500B na umepewa misaada zaidi ya 75% ya huo Uchumi is nothing to be proud of.
$ 3B ni tone kwenye nchi yenye uchumi wa $500B

Makampuni ya Tech yanawekeza Israel kwasababu wameelimika na wana uwezo mkubwa wa uvumbuzi, Israel inafahamika dunioani kuwa "The start up nation 'ndio nchi inayoongoza kwa mbanano mkubwa wa Tech Start ups zinazofanikiwa

Ulitaka microsoft wafungue ofisi zao za ubunifu kwa wanaorushia vijiti drone ?
 
Hezbollah hawana uwezo wa kununua ndege za bilioni 200, achilia mbali gharama za maintanance

Hezbollah hawana uwezo wa kumodify, Israel akinunua hizo ndege anatoa vitu vingi anaweka vyake.

Silaha nyingi Israel ananunua, ni silaha chache sana anapewa.

Huo msaada wa dola bilioni 3 za silaha wanaopewa Israel ni mdogo sana, Kwa mwaka huu uchumi wao umeshuka lakini ni Dola bilioni 500 (Zaidi ya shilingi trilioni moja na nusu) kusanya nchi zote afrika mashariki na kati hazigusi
Israel inategemea mno msaada wa Marekani Ili iweze kuendeleza vita yake.
 
Hezbollah hawana uwezo wa kununua ndege za bilioni 200, achilia mbali gharama za maintanance

Hezbollah hawana uwezo wa kumodify, Israel akinunua hizo ndege anatoa vitu vingi anaweka vyake.

Silaha nyingi Israel ananunua, ni silaha chache sana anapewa.

Huo msaada wa dola bilioni 3 za silaha wanaopewa Israel ni mdogo sana, Kwa mwaka huu uchumi wao umeshuka lakini ni Dola bilioni 500 (Zaidi ya shilingi trilioni moja na nusu) kusanya nchi zote afrika mashariki na kati hazigusi
Hata Israel bila misaada ya western hawezi Hilo zoezi
 
Back
Top Bottom