Tuwekane Sawa; Single mother NI Yule asiyeweza kuhudumia Watoto wake na Anahitaji kutunziwa Watoto na Mwanaume Mwingine àmbaye hakumzalisha

Umeandika bandiko refu sana la kuwalaumu hao single mother,umewaita wavivu,tegemezi na lawama kibao,

Swali langu ni kwamba,hao watoto wanaohangaika na Mama yao ambaye wewe unamuita tegemezi,Baba wa hao watoto hua wanakua wapi? Ni nani mwenye jukumu la kuwatunza hao watoto?

Mwanaume aliyekamilika anakubali vipi watoto wake wapitie maisha magumu mpaka Mama yao kutafuta msaada kwa Mwanaume mwingine?

Inawezekana pia kua hao Single mother wana matatizo yao mengine but sababu kuu ni kwa baadhi ya sisi wanaume kushindwa kuwatunza watoto wako wewe mwenyewe,

Moja ya sifa kuu ya Mwanaume ni kuihudumia familia yako,haijalishi nini kilitokea kati yako na huyo x wako.
 
Ila nao wanawake wanazingua kwanini wanawapa vijana wa ovyo utam🤔
 
Umeandika bandiko refu sana la kuwalaumu hao single mother,umewaita wavivu,tegemezi na lawama kibao,
Mimi nimeongea kilichopo kwèñye jamii. Labda wewe na wengîneo ndîo mtashndwa kuelewa ujûmbe WA nilichoandika.

Swali langu ni kwamba,hao watoto wanaohangaika na Mama yao ambaye wewe unamuita tegemezi,Baba wa hao watoto hua wanakua wapi? Ni nani mwenye jukumu la kuwatunza hao watoto?

Hili nilishaeleza kuwa, mama kama anaona hawezi kuwatunza Watoto awapeleke Kwa Baba Yao. Mwanamke anajijua Hana uwezo wa Kutoa Pesa za Watoto why abaki na Watoto kama siô ushenzi?
Mwanaume aliyekamilika anakubali vipi watoto wake wapitie maisha magumu mpaka Mama yao kutafuta msaada kwa Mwanaume mwingine?

Kama Mwanamke ameng'ang'ania Watoto unategemea mwanaume Afanye nini?
Mama apeleke Watoto Kwa Baba Yao ili Baba asigawanye Pesa ili zitoshe Kûtunza Watoto Kwa pàmoja.

Mfano, wewe kipato chako NI Laki tatu. Umeoa na unawatoto wawili lakini kûna Mwanamke ulimzalisha, hivyo jumla unawatoto Watatu. Unategemea njia Ipi NI rahisi kumlea Mtoto WA nje Kwa Mshahara wa Laki tatu, je Mtoto huyo aletwe Hapo nyumbani kwako ili bajeti ya Laki tatu isigawanywe ale na nduguze au abaki nje Huko Kwa Mamaake apate kidunchu au asipate Kabisa?
Inawezekana pia kua hao Single mother wana matatizo yao mengine but sababu kuu ni kwa baadhi ya sisi wanaume kushindwa kuwatunza watoto wako wewe mwenyewe,
Narudia, Mwanamke kama hawezi Kûtunza Watoto awapeleke Kwa Baba Yao.
Labda abaki nao Kwa makubaliano kuwa Baba atahudumia Mtoto huyo akiwa Kwa mamaake
Moja ya sifa kuu ya Mwanaume ni kuihudumia familia yako,haijalishi nini kilitokea kati yako na huyo x wako.

Huduma ya Mtoto NI suala la Upendo na mahesabu ya kiuchumi.
Unaweza Ukawa na Upendo lakini mahesabu ya kiuchumi yakagoma ndîo maana njia rhiai NI aidha Watu wasiachane ila kama itawalazimu kuachana Basi Yule mwenye uwezo Ndio abaki na Mtoto
 
Ila nao wanawake wanazingua kwanini wanawapa vijana wa ovyo utam🤔
Ni ngumu sana kumpima mtu kirahisi na kumjua kua huyu ni wa hovyo au sio wa hovyo,

Wapo Wanawake wamezalishwa na vijana hao unaowaita wahovyo ila wapo pia wanaume wamewazalisha Wanawake wa hovyo pia,

Uhovyo wa mtu hauna jinsia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…