Tuwekane Sawa; Single mother NI Yule asiyeweza kuhudumia Watoto wake na Anahitaji kutunziwa Watoto na Mwanaume Mwingine àmbaye hakumzalisha


Ndîo maana nikakuambia ungesoma Mada ukaelewa ungejua kinachozungumziwa.

Nilikuuliza swali Huko juu ñàona Kwa makusudi umejifanya kipofu hulioni.
Ukiulizwa ujûmbe au lengo la àndiko hili utajibuje kama kweli ulisoma?
Naamini ulisoma ndîo maana upo Hapa unachangia maonî yako Kulingana na kile ulichoelewa
 
Hizo ndoa nimeziona wakati nakua na sikuwahi kuwahoji (well hata wewe huwezi leo ukaenda kuwahoji wake za watu namna wanavyoishi na waume zao) lakini nachojua babu alikuwa na watoto zaidi ya 40+ na wote ninaowajua aliwapa mahitaji ya msingi mashamba elimu etc (japo elimu siyo ile kubwa nadhani ni jinsi mtoto mwenyewe alivyokuwa anafaulu ila wapo walimu nadhani watatu na daktari mmoja)

Babu amekufa mzee aged 116 na mimi kuweka huo mfano sikusema mtu akaoe wake tisa ila nieleweke nilijaribu kueleza umuhimu wa mke kubaki ndani ya nyumba na watoto wake kama baba anatimizia familia mahitaji ya msingi.
 
Sasa la kuandamwa haliondoi maana halisi ya Single parents mkuu usichanganye mafaili.

Tukija kwenye sababu za kuandamwa ni kutokana na tabia zao hasa wanaanzisha mahusiano mapya, baadhi ya hoja za wanaolalamikia hao single mothers ni kukosa msimamo na kuendeleza mapenzi na wazazi wenzao ilihali wako kwenye mahusiano mengine, ndio hapo watoa hoja wanasema ukiwa na mahusiano na Single mother hakikisha amekuonyesha kaburi la mwenzi wake.

Ikumbukwe Single mother wanaolalamikiwa sana na kuandamwa ni wale ambao wazazi wenzao wapo, sio wale wajane.

Sasa ukisema kwanini single fathers hawaandamwi sana basi ujue hawana changamoto kubwa maana kwenye hilo tunategemea walalamikaji wawe wanawake wanaoishi nao, sasa kama hawalalamiki tutawalazimisha walalamike ili kubalansi ikwesheni mkuu?
 
Hizo ndoa nimeziona wakati nakua na sikuwahi kuwahoji (well hata wewe huwezi leo ukaenda kuwahoji wake za watu namna wanavyoishi na waume zao)
Sasa wewe kuziona kwa nje wakati wa makuzi yako ndio ukaja na conclusion kwamba walipendana na kuheshimiana wote 9 na babu yako hakuwaumiza hisia zao?

lakini nachojua babu alikuwa na watoto zaidi ya 40+ na wote ninaowajua aliwapa mahitaji ya msingi mashamba elimu etc (japo elimu siyo ile kubwa nadhani ni jinsi mtoto mwenyewe alivyokuwa anafaulu ila wapo walimu nadhani watatu na daktari mmoja)
Watoto zaidi ya 40 na mama zao 9 halafu unakuja na mfano wa watoto wanne (4) tu?

Babu amekufa mzee aged 116 na mimi kuweka huo mfano sikusema mtu akaoe wake tisa ila nieleweke nilijaribu kueleza umuhimu wa mke kubaki ndani ya nyumba na watoto wake kama baba anatimizia familia mahitaji ya msingi.
Unatambua kwamba kuna mahitaji ya msingi ya family kwa pamoja na mahitaji ya msingi ya mke? Na kulindwa kwa hisia zake huyo mke ni sehemu ya hayo mahitaji?

Na ndicho umeambiwa huko juu kwamba ili mwanamke adumu kwenye Ndoa, kuna mambo mengi sana yanahitajika ikiwemo ulinzi wa hisia zake na mwanamke ni kiumbe wa Hisia.

Hao bibi zako kubaki kwenye ndoa na babu yako ni mengi yanayoweza kuchangia lakini kubwa zaidi ni ulezi wa watoto na sio mapenzi wala huduma.
 
Angesoma hiyo sentensi yako ya kwanza kwa utulivu, angetambua kosa lake.

Majibu yake kwangu namuona anazidi kupotea tu, lakini hawezi kunipoteza mimi, thread yake haina mantiki.
 
Màda yako nimeisoma nikaielewa, ndio maana nikakujibu.

Hata mdau hapo juu nae amekusoma, akakuelewa, ndio maana nae ameona kosa lako la kimantiki kwenye maana ya neno "single"
 
Huko tuendapo utakuja na mada kwamba Mwanaume ni yule tu afanyaye kazi za kulima kwa jembe la mkono, abebaye mizigo na kuwinda, wengine wote utakuja utwambie hawapo kundi la wanaume
 
Nashauri tuwapumzishe hao Single Mothers, Kuna wengine walipata mimba Kwa kubakwa na wakaishia kuwa single mother.

Wengine ilitokea Waume zao wamefungwa vifungo vya muda mrefu magerezani, hivyo kubaki na Jukumu la kulea watoto peke yao.
🤣🤣🤣🤣🤣 Tulibakwa!?? Aaa...hapana kwa kweli.Tuliivulia kabisa mkuu....na maiki tukaikamata,tukaimba na kuiweka wenyewe chini.Sema tu kitu kikiwa si chako siyo chako tu😉
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…