Tuwekane Sawa; Single mother NI Yule asiyeweza kuhudumia Watoto wake na Anahitaji kutunziwa Watoto na Mwanaume Mwingine àmbaye hakumzalisha

Tuwekane Sawa; Single mother NI Yule asiyeweza kuhudumia Watoto wake na Anahitaji kutunziwa Watoto na Mwanaume Mwingine àmbaye hakumzalisha

Tatizo lako unajigeuza mpiga ramli sasa ili ku justify kosa lako la kimantiki kwenye ku define neno "single" kulingana na mada yako, umeshaelekezwa elewa, acha ubishi.

Hapa duniani neno "single" halijawahi kumaanisha mzazi mwanamke kukosa pesa, umedanganya.

Ndîo maana nikakuambia ungesoma Mada ukaelewa ungejua kinachozungumziwa.

Nilikuuliza swali Huko juu ñàona Kwa makusudi umejifanya kipofu hulioni.
Ukiulizwa ujûmbe au lengo la àndiko hili utajibuje kama kweli ulisoma?
Naamini ulisoma ndîo maana upo Hapa unachangia maonî yako Kulingana na kile ulichoelewa
 
Bold & Underline

Hizo Ndoa za babu yako umezishuhudia ukiwa na umri gani? Yaani ulikua Unajitambua kwa kiasi gani?

Hao wanawake 9 uliongea nao wote wakakwambia wako na Amani na furaha kwenye hizo Ndoa?

Babu yako alikua na watoto wangapi? Maisha yao na mama zao yalikuwaje baada ya kuondoka kwake?

Athari za ndoa za mitala huwa sio za kujificha, matokeo tunayaona mpaka leo maana Kama Ndoa za waliotutangulia zingekua that perfect, basi the ripples of reflections tungeziona mpaka kwenye ndoa za sasa.
Lakini ni kinyume chake kiasi inatupa mwanga wa yake yaliyopita kwamba hayakua all glorious and perfect Kama unavyojaribu kutuaminisha hapa.
Hizo ndoa nimeziona wakati nakua na sikuwahi kuwahoji (well hata wewe huwezi leo ukaenda kuwahoji wake za watu namna wanavyoishi na waume zao) lakini nachojua babu alikuwa na watoto zaidi ya 40+ na wote ninaowajua aliwapa mahitaji ya msingi mashamba elimu etc (japo elimu siyo ile kubwa nadhani ni jinsi mtoto mwenyewe alivyokuwa anafaulu ila wapo walimu nadhani watatu na daktari mmoja)

Babu amekufa mzee aged 116 na mimi kuweka huo mfano sikusema mtu akaoe wake tisa ila nieleweke nilijaribu kueleza umuhimu wa mke kubaki ndani ya nyumba na watoto wake kama baba anatimizia familia mahitaji ya msingi.
 
Sasa kwa hiyo definition yako àmbayo Mtoto wa kidato cha Kwanza ataeleza,
Tuambie nini kinasababisha Wanawake single mother kuandamwa na kukejeliwa mitañdaoni Wakati single Father hawafanyiei hivyo?
Kama Moja ya sababu kûbwa siô suala la kiuchumi kuachana na mambo ya Mapenzi?
Sasa la kuandamwa haliondoi maana halisi ya Single parents mkuu usichanganye mafaili.

Tukija kwenye sababu za kuandamwa ni kutokana na tabia zao hasa wanaanzisha mahusiano mapya, baadhi ya hoja za wanaolalamikia hao single mothers ni kukosa msimamo na kuendeleza mapenzi na wazazi wenzao ilihali wako kwenye mahusiano mengine, ndio hapo watoa hoja wanasema ukiwa na mahusiano na Single mother hakikisha amekuonyesha kaburi la mwenzi wake.

Ikumbukwe Single mother wanaolalamikiwa sana na kuandamwa ni wale ambao wazazi wenzao wapo, sio wale wajane.

Sasa ukisema kwanini single fathers hawaandamwi sana basi ujue hawana changamoto kubwa maana kwenye hilo tunategemea walalamikaji wawe wanawake wanaoishi nao, sasa kama hawalalamiki tutawalazimisha walalamike ili kubalansi ikwesheni mkuu?
 
Hizo ndoa nimeziona wakati nakua na sikuwahi kuwahoji (well hata wewe huwezi leo ukaenda kuwahoji wake za watu namna wanavyoishi na waume zao)
Sasa wewe kuziona kwa nje wakati wa makuzi yako ndio ukaja na conclusion kwamba walipendana na kuheshimiana wote 9 na babu yako hakuwaumiza hisia zao?

lakini nachojua babu alikuwa na watoto zaidi ya 40+ na wote ninaowajua aliwapa mahitaji ya msingi mashamba elimu etc (japo elimu siyo ile kubwa nadhani ni jinsi mtoto mwenyewe alivyokuwa anafaulu ila wapo walimu nadhani watatu na daktari mmoja)
Watoto zaidi ya 40 na mama zao 9 halafu unakuja na mfano wa watoto wanne (4) tu?

Babu amekufa mzee aged 116 na mimi kuweka huo mfano sikusema mtu akaoe wake tisa ila nieleweke nilijaribu kueleza umuhimu wa mke kubaki ndani ya nyumba na watoto wake kama baba anatimizia familia mahitaji ya msingi.
Unatambua kwamba kuna mahitaji ya msingi ya family kwa pamoja na mahitaji ya msingi ya mke? Na kulindwa kwa hisia zake huyo mke ni sehemu ya hayo mahitaji?

Na ndicho umeambiwa huko juu kwamba ili mwanamke adumu kwenye Ndoa, kuna mambo mengi sana yanahitajika ikiwemo ulinzi wa hisia zake na mwanamke ni kiumbe wa Hisia.

Hao bibi zako kubaki kwenye ndoa na babu yako ni mengi yanayoweza kuchangia lakini kubwa zaidi ni ulezi wa watoto na sio mapenzi wala huduma.
 
Sasa la kuandamwa haliondoi maana halisi ya Single parents mkuu usichanganye mafaili.

Tukija kwenye sababu za kuandamwa ni kutokana na tabia zao hasa wanaanzisha mahusiano mapya, baadhi ya hoja za wanaolalamikia hao single mothers ni kukosa msimamo na kuendeleza mapenzi na wazazi wenzao ilihali wako kwenye mahusiano mengine, ndio hapo watoa hoja wanasema ukiwa na mahusiano na Single mother hakikisha amekuonyesha kaburi la mwenzi wake.

Ikumbukwe Single mother wanaolalamikiwa sana na kuandamwa ni wale ambao wazazi wenzao wapo, sio wale wajane.

Sasa ukisema kwanini single fathers hawaandamwi sana basi ujue hawana changamoto kubwa maana kwenye hilo tunategemea walalamikaji wawe wanawake wanaoishi nao, sasa kama hawalalamiki tutawalazimisha walalamike ili kubalansi ikwesheni mkuu?
Angesoma hiyo sentensi yako ya kwanza kwa utulivu, angetambua kosa lake.

Majibu yake kwangu namuona anazidi kupotea tu, lakini hawezi kunipoteza mimi, thread yake haina mantiki.
 
Ndîo maana nikakuambia ungesoma Mada ukaelewa ungejua kinachozungumziwa.

Nilikuuliza swali Huko juu ñàona Kwa makusudi umejifanya kipofu hulioni.
Ukiulizwa ujûmbe au lengo la àndiko hili utajibuje kama kweli ulisoma?
Naamini ulisoma ndîo maana upo Hapa unachangia maonî yako Kulingana na kile ulichoelewa
Màda yako nimeisoma nikaielewa, ndio maana nikakujibu.

Hata mdau hapo juu nae amekusoma, akakuelewa, ndio maana nae ameona kosa lako la kimantiki kwenye maana ya neno "single"
 
TUWEKANE SAWA; SINGLE MOTHER NI YULE ASIYEWEZA KUHUDUMIA WATOTO WAKE NA ANAHITAJI KUTUNZIWA WATOTO NA MWANAUME MWINGINE ÀMBAYE HAKUMZALISHA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kelele zote na Kejeli zote unazozisikia Kuwahusu single mother msingi wake Mkûu ni ufukara walionao Wanawake wengi.
Kimsingi Kejeli hizô zinawahusu Wanawake wasiokuwa, tegemezi Kwa Wanaume, wasiotaka kufanya Kazi na kujihudumia waô na Watoto waô. Wanaotumia Watoto waô kama miradi ya Kujipatia kipato.

Hao ndîo huitwa single Mother.

Hakunaga single Father Duniani Kwa sababu hakunaga wanaume weñye Watoto àmbao watahitaji Mwanamke Mwingine atoe huduma za kifedha na mahitaji Kwa Watoto waô.
Ndîo maana hata ukimuita Mwanaume single Father kwàke haina Ñguvu, haimuumi.

Single mother NI neno baya na Kejeli Kwa Wanawake tegemezi, nyonyaji na wale ambao wakitaka mahusiano mapya huwapa Mizigo Wenza wapya kuwatunza Watoto àmbao siô Waô.

Mwanamke mwenye Kazi yake, mwenye uwezo wa kulea Watoto wake mwenyewe HAYUPO kwèñye kundi la single mother na hata ukimuita single mother haiwezi kumuuma zaidi atakuona hamnazo kwani hajakupa Wala kumpa yeyote Mtoto au Watoto wake uwalee.

Mwanamke mwenye Kazi na anayeweza Kumudu kulea Watoto wake ukimuoa hawezi kuwa mzigo wa msalaba zaidi sana mtasaidiana Majukumu ya Kûtunza Watoto wenu kama ilivyolengo Kuu la Ndoa yàani kusaidiana.

Watu wanaosema hawataki Kuoa single mother tafsiri Yao kûbwa NI kwamba hawataki kujibebesha Misalaba ya Maisha Kwa kulea Watoto AMBAO siô Waô. Na kuachiwa mzigo wote wa kuvuja jasho kupita kiasi.

Kûna msemo Siku hizi unasema Vijana wanataka mashangazi, lakini ukifuatilia Kwa undani mashangazi mengi yanayotajwa Hapo NI masingle mother Zamani yaliitwa sugar mummy yàani Mwanamke mwenye kujiweza kiuchumi.

Single mother asiye na Kazi Wala ASIYEWEZA kujihudumia hayupo kundi la sugar mummy au shangazi Bali yupo lile kundi linalokimbiwa Kila Siku na Vijana na Wanaume.

Taikon master kama mtaalamu wa sosholojia na saikolojia ndîo maana kîla nipatapo Nafasi nawaambia Dada zangu na Binti zangu ni lazima ufanye Kazi za uzalishaji Hilo Wala siô ombi bali ni Amri àmbayo hata mwenyezi Mungu aliitoa kuwa Mtu sharti afanye Kazi kama hutaki kudhihakiwa au kudhalilishwa.

Wewe kama Huna Kazi na tegemezi hata serikali iwekwe Sheria Kali ya kunyonga Watu wanaokejeli, dhihaki, kunyanyaswa na kudhalilisha Wanawake tegemezi, elewa Watu wataendelea kuivunja hiyo Sheria Kwa sababu hiyo NI Asili kuwa Mtu tegemezi ni mtu aliyeamua kudharauliwa na kukejeliwa.

Mumeo anapokuambia uache Kazi na usifanye Kazi íwe KW Nia yoyote Ile nzuri au Mbaya. Elewa Siku mkiachana anakuwekea mazîngira Magumu ya kukejeliwa na kudharauliwa.
Hutoitwa Sugar mummy kama uliachwa alafu hujiwezi. Hutoitwa shangazi ilhali hujiwezi.
Utaitwa single mother na matusi kibao.

Fikiria unawatoto wawili au Watatu, unamiaka 30+ alafu unàtaka Mwanaume mpya akuhudumie wewe na Watoto wako ukijitafakari Akili yako itakuwa inachaji kweli?
Wanaume waache mabinti wabichu WA tiktok, Instagram Huko kweli waje uwabebeshe misalaba isiyowahusu, kweli dada zangu hiyo inawaingia akilini?

Mambo yamebadilika.

Elimu bure na zinatolewa Sawa Kwa jinsi zote Mbili why hutaki kusoma?

Fursa za Kazi zinatolewa kwa jinsia zote Mbili Kwa usawa why hutaki kufanya Kazi ujitegemee?
Unafikiri serikali na Dunia ya Sasa imechukua uamuzi WA kufanya hivyo NI wajinga na wéwe ndîo unaakili kuwashinda ndîo maana hutaki Shule na hutaki Kazi Kwa kutegemea kuwa Mwanaume Fulani atakutunzia Watoto uliozaa na Wanaume Wengine Huko.
Kwèli?

Dada zangu, Binti zangu nawaomba, Nipo chini ya miguu Yenu. Legezeni vishikizo vya Akili zenu ili mnielewe. Kufanya Kazi NI kwaajili Yenu wenyewe na Watoto wenu. NI kwaajili ya heshima Yenu baadaye mambo yatakapobadilika.

Msiwe wajinga.

Hivi kwaakili yako, Mwanaume amekuta Wanawake wawili warembo, wôte wanamtaka, wôte wanamtoto lakini mmoja anakazi (anajiweza)na mwingine hana kazi(hajiwezi) hivi unadhani huyo Mwanaume atamchagua Nani?
Kwa ulivyo mjinga utasema ataangalia anayempenda.

Mambo ya kuangalia anayempenda yanaishia CHINI ya Miaka 30 Huko.

Hivi Mwanaume mwenye Miaka 35 unafikiri amependa wangapi Huko Nyuma Mpaka alipokutana na wéwe akupende wewe akuchague wewe dhidi ya mwanamke mwenzako mwenye uwezo wa kumsaidia kimaisha na kutimiza Ndoto zào Kwa pàmoja?

Binti yàngu, Mimi Babaako huenda ukaniona ninakukera Sana lakini elewa ninayoyasema ndîo ukweli wènyewe.

Fanya Kazi. Kazi NI Ibada. Jitahidi ujitegemee na usiwe mzigo Kwa Mtu yeyote Yule.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi.
Kwa Sasa Dar es salaam
Huko tuendapo utakuja na mada kwamba Mwanaume ni yule tu afanyaye kazi za kulima kwa jembe la mkono, abebaye mizigo na kuwinda, wengine wote utakuja utwambie hawapo kundi la wanaume
 
Nashauri tuwapumzishe hao Single Mothers, Kuna wengine walipata mimba Kwa kubakwa na wakaishia kuwa single mother.

Wengine ilitokea Waume zao wamefungwa vifungo vya muda mrefu magerezani, hivyo kubaki na Jukumu la kulea watoto peke yao.
🤣🤣🤣🤣🤣 Tulibakwa!?? Aaa...hapana kwa kweli.Tuliivulia kabisa mkuu....na maiki tukaikamata,tukaimba na kuiweka wenyewe chini.Sema tu kitu kikiwa si chako siyo chako tu😉
 
Back
Top Bottom