Tuwekane Sawa; Single mother NI Yule asiyeweza kuhudumia Watoto wake na Anahitaji kutunziwa Watoto na Mwanaume Mwingine àmbaye hakumzalisha

Tuwekane Sawa; Single mother NI Yule asiyeweza kuhudumia Watoto wake na Anahitaji kutunziwa Watoto na Mwanaume Mwingine àmbaye hakumzalisha

Mimi nimeongea kilichopo kwèñye jamii. Labda wewe na wengîneo ndîo mtashndwa kuelewa ujûmbe WA nilichoandika.
Kwenye jamii pia wapo Wanaume waliowatelekeza watoto wao,hao ndio nimewaongelea,
Hili nilishaeleza kuwa, mama kama anaona hawezi kuwatunza Watoto awapeleke Kwa Baba Yao. Mwanamke anajijua Hana uwezo wa Kutoa Pesa za Watoto why abaki na Watoto kama siô ushenzi?
Kwani hujawahi kusikia kua kuna Wanaume wamewakataa watoto wao? Hujawahi kusikia kua kuna watoto wametelekezwa na Baba zao? Hujasikia story ya Ommy Dimpoz na Baba yake? Hujasikia story ya Diamond na Baba yake?
Kama Mwanamke ameng'ang'ania Watoto unategemea mwanaume Afanye nini?
Mama apeleke Watoto Kwa Baba Yao ili Baba asigawanye Pesa ili zitoshe Kûtunza Watoto Kwa pàmoja.

Mfano, wewe kipato chako NI Laki tatu. Umeoa na unawatoto wawili lakini kûna Mwanamke ulimzalisha, hivyo jumla unawatoto Watatu. Unategemea njia Ipi NI rahisi kumlea Mtoto WA nje Kwa Mshahara wa Laki tatu, je Mtoto huyo aletwe Hapo nyumbani kwako ili bajeti ya Laki tatu isigawanywe ale na nduguze au abaki nje Huko Kwa Mamaake apate kidunchu au asipate Kabisa?

Narudia, Mwanamke kama hawezi Kûtunza Watoto awapeleke Kwa Baba Yao.
Labda abaki nao Kwa makubaliano kuwa Baba atahudumia Mtoto huyo akiwa Kwa mamaake

Huduma ya Mtoto NI suala la Upendo na mahesabu ya kiuchumi.
Unaweza Ukawa na Upendo lakini mahesabu ya kiuchumi yakagoma ndîo maana njia rhiai NI aidha Watu wasiachane ila kama itawalazimu kuachana Basi Yule mwenye uwezo Ndio abaki na Mtoto
Huduma ya mtoto sio suala la upendo bali ni jukumu,huwezi ukaacha kumtunza mwanao na kutoa sababu kua eti huna upendo kwa Mwanao,chanzo kikuu cha matatizo ya hao Single mothers ni Wanaume kukimbia majukumu yao ya kuwatunza watoto wao.
 
Kumbe ndio iko hivyo ? Sikua najua

Wanadamu wanafiki sana.
Hujawahi kusikia wakisema siwezi lea bao au damu ya Mtu Mwingine.
Sasa mwanamke kama anaweza Kûtunza Watoto wake mwenyewe hiyo statement inakufa automatically

Inabaki Ile ya kuchat na ex wake Jambo ambalo single mother wengi hufanya Kwa kudai matumizi ya Watoto.

Lakini kama single mother anajiweza hawezi kumtafuta mara Kwa mara Mzazi mwenza Kisa matumizi
 
Kwa sababu jukumu la Mojawapo la Wanaume NI ulinzi wa Ndoa na jamii ikiwemo Wanawake.

Hata Huko Gaza wanaopiga kelele kuwatetea Wanawake na Watoto wanaouwa NI Wanaume.

Yapo makundi MAWILI.
1. Kundi àmbalo linawakandamiza Wanawake na wanaona wanahiyo Haki ya kuwakandamiza.

2. Kundi linalotetea Wanawake na kuwaamsha kuwa nao ni Watu wanaotakiwa wajitambue ili Ûtu waô uheshimike.

NI vita ya Mwanaume mwema, nuru Vs mwanaume Mbaya, Giza.
Wanawake ndio maslahi ya makundi hayo mawili

Hakuna vita Baina ya mwanaume na Mwanamke
Msijifiche kwenye kichaka cha ulinzi wa jamii, upo wakati huyo mnaemtetea atawatawala ndipo mtajutia huu muda mnaosumbuka nae, bado kidogo mwanamke atakuwa juu ya mwanaume katika nyanja zote, mtaruka na kukanyagana,
 
Kwenye jamii pia wapo Wanaume waliowatelekeza watoto wao,hao ndio nimewaongelea,

Kwani hujawahi kusikia kua kuna Wanaume wamewakataa watoto wao? Hujawahi kusikia kua kuna watoto wametelekezwa na Baba zao? Hujasikia story ya Ommy Dimpoz na Baba yake? Hujasikia story ya Diamond na Baba yake?

Huduma ya mtoto sio suala la upendo bali ni jukumu,huwezi ukaacha kumtunza mwanao na kutoa sababu kua eti huna upendo kwa Mwanao,chanzo kikuu cha matatizo ya hao Single mothers ni Wanaume kukimbia majukumu yao ya kuwatunza watoto wao.

Stori ya Immy dimpo, Diamond na wenzake NI Stori Ambazo ukizifuatilia utagundua kuwa Wanawake waling'ang'ania kuondoka na Watoto.

Nafahamu wàpo Wababa wanaokataa Watoto lakini katika mazîngira Fulani hasa mazîngira Tata. Wakati huohuo ninawajua waliokubali Watoto Kwa shinikizo lakini Watoto hao siô Watoto waô halisi.

Baba anapokataa Watoto sababu kûbwa huwa ni uaminifu mdogo Kwa huyo aliyembebea huyo Mtoto.
NI Haki ya Mtu kama haamini kuwa Mtoto siô wake kuaminishwa na kuthibitishiwa

Tuliona Kwa Yusufu Mume WA Maria
Tuliona Kwa Lamecki Babaake Nabii Nuhu àmbaye naye alikuwa mbioni kunikataa Nuhu sio Mwanaye kisa na Mkasa hawafanani.

Serikali lazima iweke mazîngira ràfiki ya Haki katika suala la HAKI ya Mtoto na Mzazi kuepuka utapeli, dhulma na ukatili
 
Msijifiche kwenye kichaka cha ulinzi wa jamii, upo wakati huyo mnaemtetea atawatawala ndipo mtajutia huu muda mnaosumbuka nae, bado kidogo mwanamke atakuwa juu ya mwanaume katika nyanja zote, mtaruka na kukanyagana,

Hiyo haitakuja kutokea Dunia ingalipo.
Ukiona mwanamke anatawala ujue Nyuma Yake kûna kundi la Mwanaume au Wanaume Fulani wanaomlinda.

Hiyo Ipo hivyo kihistoria na itabaki hivyo Miaka yôte.

Mwanamke akiweza kumtawala Mwanaume ujue Mwanadamu anaweza kumtawala Mungu.
 
Jana nimeota Nina mimba.niliota nimepima kipimo nikasema Nina mimba.kiukweli sijasex almost 2yrs.nilipokea majibu kwa masikitiko.naombeni tafsiri wakuu.kusema kweli nilikuwa na appointment yabkupiga tukio ila nimeogopa

Ngoja wataalamu waje
 
Mkuu! Kapate tu utamu sababu inaweza kutokea sio lazima iwe mzagamuano wa leo hata wa mwakani
 
Wakati mwingine huwa unakurupuka kuandika tena kwa confidence sana.

Single mother ni mwanamke anayelea mtoto/watoto peke yake bila ya uwepo wa mwanaume pembeni yake, haijalishi huyu mwanamke awe na uwezo kiuchumi au asiwe nao.

Lazima utambue, umuhimu wa mzazi wa kiume kwenye malezi ya mtoto wakati mwingine ni zaidi ya kutoa pesa za matunzo, na ndio maana hata hao single mothers wenye uwezo kiuchumi, bado wanahitaji kwa nguvu uwepo wa mzazi wa kiume pembeni yao.
 
Mwanamke anaweza akawa na Adabu akaolewa Kabisa lakini kwèñye Ndoa akaambiwa asifanye Kazi. Akamheshimu Mumewe na kumsikiliza.
Alafu mwisho WA Siku akapewa talaka au Mumewe akamfanyia mambo ya hiyana, au akataka kumuongezea Mke Mwingine.

Baàda ya kufukuzwa, Hana Kazi, hawezi kujitegemea na uzoefu WA kujitegemea Hana.
Hawezi kujitunza wala Kûtunza Watoto wake aliowazaa mwenyewe Wakati Kuku na Wanyama wengine wanatunza.

Alafu anashindwa Kupata Mwanaume Mwingine Kwa Sababu huyo Mwanaume Mwingine anamuona mzigo yeye na Watoto wake.

Bado unaona sina sababu ya kuwaambia Ukweli?
Bold kubwa:Mwanamke wa hivyo huyo ni sawa na mama yako,au mama wa rafiki yako even mama yangu kama bado unawaona ktk ndoa zao na waume zao,mwanaume ukiondoa kuzaa watoto anachokitafuta kwa mkewe ni heshima na masikilizano so kwa muktadha huo simuoni mume wa mwanamke wa kwenye mfano wako akimfanyia mabaya.

Bold ndogo:kwa ishu ya kuongeza mke nadhani imekaa kidini zaidi inapaswa alijue hilo lah kama siyo la kidini amuulize mume may be anahitaji watoto wengi zaidi huku yeye akiwa uwezo wa kuwazaa hana,but still mimi nikiwa kama mwanaume nasema hii sababu ya kuongezewa mke siyo sababu ya kumfanya mwanamke aondoke kwa mumewe ikiwa anatimiziwa yote ya msingi kifamilia then kama hayatekelezwi zipo sheria za nchi ustawi wa jamii watamlazimisha mume awajibike kwa familia yake lakini wengi unaowaona mitaani hizi sababu sizo zinazowakimbiza kwa waume sababu kuu ni kiburi,dharau kwa kujifariji kwao kwamba anachokifanya mwanaume nao wanakiweza.
 
Kwèñye Ndoa kûna mambo meñgi makuu heshima ikiwepo, kuna Upendo, kûna kutimiziana Ndoto na furaha katika Maisha, n.k
Bold ndogo:kwa ishu ya kuongeza mke nadhani imekaa kidini zaidi inapaswa alijue hilo lah kama siyo la kidini amuulize mume may be anahitaji watoto wengi zaidi huku yeye akiwa uwezo wa kuwazaa hana,but still mimi nikiwa kama mwanaume nasema hii sababu ya kuongezewa mke siyo sababu ya kumfanya mwanamke aondoke kwa mumewe ikiwa anatimiziwa yote ya msingi kifamilia then kama hayatekelezwi zipo sheria za nchi ustawi wa jamii watamlazimisha mume awajibike kwa familia yake lakini wengi unaowaona mitaani hizi sababu sizo zinazowakimbiza kwa waume sababu kuu ni kiburi,dharau kwa kujifariji kwao kwamba anachokifanya mwanaume nao wanakiweza.

Mwanaume na Mwanamke waliopo ndoani hupaswa kutimiziana haja zào kimwili, kiroho, kihisia na Kiakili

Wewe umchukulie Mkeo Mke Mwingine utegemee unamtimizia haja Zake kihisia?
 
Back
Top Bottom