Nikuulize kiufupi tu, heshima aliyopewa mwanaume wa zamani bado anapewa heshima hiyo miaka hii anzio 2010,
Mamlaka yenu tunazidi kuyaona ya kawaida sana hamuungurumi wala kututisha tena, tumewakanyaga vilivyo na saiv tunawapanda vichwani bado kuwakalia ili tuwatawale vizuri
Kapeace wewe ni mwanamke àmbaye naamini umesoma na kuelimika.
Heshima ya Mwanaume bado ingalipo.
Labda kama Unazungumzia Hofu na woga uliotengenezwa na mfumo Ovu wa Zamani ili kukandamiza haki ya kundi Fulani.
Heshima haishuki Kwa sababu heshima NI heshima. Heshima NI KWELI tupu.
Zamani kuliko na dhana nyingi za uongouongo Ambazo zililenga kuogopesha Watu kuliko kuleta heshima.
Mfano,Zamani ilisemekana, mzungu hafi Jambo ambalo lilifanya Waafrika waogope wazungu. Lakini Siku hizi hiyo kitu haipo Kwa sababu ûjinga umeondoka.
Zamani, Watu waliogopa Wazazi badala ya kuwaheshimu Kwa ile dhana ya uongo ya Laana.
Lakini Siku hizi watu hawaogopi Wazazi isipokuwa wanawaheshimu. Ndîo maana Siku hizi Mzazi hawezi kukuamulia Jambo ambalo wewe unaona siô Sahihi. Ila Zamani waliweza Mpaka kukuchagulia Mke au Mume kilazima utake usitake. Ukibisha wanakutishia Laana. Siku hizi wanajua hata wakukulaani haiwezeni Kwa sababu janja Yao umejulikana.
Zamani Wanawake waliogopa Wanaume Kwa Sababu mbalimbali,
Mosi, ulinzi na usalama. Dunia iliyopita ilikuwa ya ubabeubabe.
Pili, huduma na Haki ya KUMILIKI utajiri
Zamani Mwanamke asiye na Mwanaume Hana ujanja wa kuishi Kwa sababu atapata Wapi chàkula, atatumia Ardhi Ipi Wakati kîla Ardhi inamilikiwa na Mwanaume.
Zamani, Mfalme alidhaniwa ananguvu za kimungu yàani Sawa na Mungu.
Walitisha Watu badala ya kusema UKWELI.
Zamani, waalimu waliogopwa Sana lakini Siku hizi hawaogopwi ila wanaheshimiwa.
Ukifanya ya heshima utaheshimika na kuheshimiwa Bila kujali Nafasi yako.
Lakini Zamani unaweza ukafanya Mabaya na Watu wakakuheshimu kinafiki Kwa hofu(woga) lakini mioyoni mwao hawakuheshimu.
Tunapoelekea NI kuzuri zaidi maana uongo na ukweli vitakuwa Mbingu na Ardhi, magharibi na Mashariki.
Bado utasema Mwanaume Sasa hivi haheshimiki?
Semà Mwanaume Sasa hivi haogopeki.
Yàani usemè Zamani Mwanaume alikuwa anaheshimika na Wanawake kwakuoa wake wengi? Kweli?
Yàani wewe uolewe na Mwanaume alafu akuletee wake Wenza Kumi usemè utamheshimu? Unajua maana ya kumheshimu Mtu kwèli?