Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
- Thread starter
- #41
Vijana wa sasa ni mapenzi na kunywa bia sana.
Wanasema bia tamu
Na kuzalisha mabinti hovyohovyo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vijana wa sasa ni mapenzi na kunywa bia sana.
Wanasema bia tamu
Pro max wako hapa. Nakusalimu.[emoji23][emoji23][emoji23]
Noma Sana...
Hapo mbinu inayofaa ni kuwa msiri. Wewe kila siku ukipigiwa simu lalamika kuwa mambo hayaendi,
Pro max wako hapa. Nakusalimu.
Mkuu! Mimi ni mzazi na nina miaka yangu kadhaa zaidi 50. Ulichosema nakupa tano 💯. Hila wazazi tunakosea sana kuweka tumaini kwa watoto ile hali hatukuwekeza kwa hao watoto tunaowategemea watutunze!NARUDIA; SIO WAJIBU WA MTOTO KUTUNZA WAZAZI WAKE.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Vijana wekezeni, wekeni akiba, kwaajili ya uzee wenu. Hicho hicho kidogo mnachokipata wekezeni na wekeni akiba. Ukishakuwa mkubwa hakuna mwenye wajibu wa kukutunza na kukuhudumia isipokuwa wewe mwenyewe. Nguvu na Akili zako ndizo zitakutunza na kukuhudumia. Hii zaidi ni Kwa Wanaume.
Kuzaa hata panya anazaa. Kulea hata Kunguru analea. Kumsomesha mtoto wako ni sehemu ya wajibu wa mzazi yaani malezi.
Usijesema sijui nimekuzaa kwani Nani hatazaa bhana? Kuzaa ni Majaliwa Ila Kulea ni wajibu wa mzazi.
Unapozaa Watoto elewa kuwa hata Watoto wako watazaa na kuwa na wajibu Kwa wale watakaowazaa.
Majukumu ya mzazi Baada ya kuzaa(ndio maana akaitwa mzazi) ni Kumlea mtoto(kumuandaa mtoto na Maisha yake Duniani) kumtunza na kumhudumia mtoto kama chakula, malazi na mavazi. Kuteseka kwaajili ya Watoto wako hiyo haimhusu mtoto. Sio hisani wala fadhila Kwa mtoto.
Ila mtoto kuteseka kwaajili yako hiyo ni hisani au fadhila, ni shukrani. Na wala sio lazima.
Sio uungwana mtoto aweke akiba kwaajili ya Wazazi wake. Bali mzazi ndio huweka akiba kwaajili ya Watoto wako. Ndio maana ukaitwa mzazi na Yule akaitwa mtoto na ndio maana ukamzaa.
Sio uzae mtoto ili umfanye mzazi wako, yaani katoto ndio Kwanza kana miaka 30 unaanza kukageuza Mzazi wako Wakati wewe ndiye ulikazaa. Huo ni uhuni.
Heshima ya mzazi sio tuu kuzaa Bali kutegemewa kuwa chanzo cha mambo nyeti Kwa mtoto wako.
Ni Tabia Mbaya Sana ambayo wazazi wengi tumedumu nayo Kwa Karne nyingi kuwafanya Watoto tegemeo letu. Wakati Sisi ndio tunatakiwa tuwe tegemeo Lao.
Hakuna laana yoyote ya mtoto kushindwa kumtunza mzazi au wazazi wake. Hakuna laana yoyote. Zingatia laana ili iitwe laana lazima iwe inahusisha uvunjaji wa sheria, amri, na Kanuni za Mungu yaani Kanuni za Asili. Laana inatoka Kwa Mungu Baada ya kuvunja amri, sheria na Kanuni zake.
Hakuna amri yoyote inayotaka mzazi atake malezi na matunzo Kwa mtoto wake.
Hakuna amri hiyo kwani uwepo wake ungezifanya Kanuni na sheria za Mungu/asili ziji-contradict zenyewe. Mfano hakuna sababu ya uwepo wa kufanya kazi Kwa Siku sita na kujiwekea akiba ili kuweka urithi Kwa Watoto ambayo ni amri pia, ilhali tunajua kabisa kuna amri inayoagiza Watoto watulee Sisi wazazi wao.
Pia sheria ya kuwaheshimu wazazi isingekuwa na maana yoyote ikiwa Wazazi haohao wanategemea kulelewa na kutunzwa na watoto. Kuzaa mtoto haitoshi kufanya mzazi aheshimiwe. Nilisema hata Panya anazaa au Nyumbu porini anazaa.
Sheria ya kufanya kazi Kwa Siku sita yaani binadamu anatakiwa Kwa zaidi ya asilimia 90 Maisha yake yawe ni kazi alafu asilimia 10 ndio iwe mapumziko. Siku moja ndani ya wiki moja. Ili ajitumikie yeye mwenyewe na kama ataamua kuwa na familia atumikie familia yake aliyoianzisha.
Hakuna aliyemtuma aanzishe familia, hakuna aloyemtuma azae Watoto.
Na hapakuwa na mapatano yoyote baina ya Mzazi na mtoto. Hivyo ni jukumu na wajibu wa mzazi kumtunza mtoto.
Uwekezaji na uwekaji wa Akiba za uzeeni ni muhimu Sana.
Urithi na Zawadi ambazo mzazi hutoa Kwa Watoto ndio vitumike kumtunzia mtoto.
Mfano, umehangaika Kwa miaka yako yote, umewekeza kwenye mashamba au mifugo au nyumba au Migodi au miradi mingine. Sasa umri umeenda nguvu zimepungua, unaamua kumuita mtoto wako na kumwambia;
"Mwanangu sasa umri umenitoka, uzee umebisha hodi na nguvu zake zimenishinda. Nilitamani ningeendelea kufanya kazi lakini Wakati ni ukuta. Nimefanya yaliyo ndani ya uwezo wangu, wala haikutokea siku nikadharau jasho langu Kwa kuwa mbadhirifu WA fedha na Mali zangu, nilijiheshimu na kuheshimu nguvu zangu, naam ndilo jasho langu, nilichobarikiwa niliwekeza na kujiwekea akiba ya nyakati kama hizi. Nikaanzisha Mradi huu na ule. Lakini nikakuweka kwenye Mradi huu(labda wa mifugo) ili tusaidiane, nawe upate uzoefu. Angalau sasa ninakuona unaweza kumudu kuendesha Mradi huu,
Nimeona nikuachie Mradi huu wewe ndiye uwe msimamizi Mkuu kwaajili yangu, ili chochote kitakachopatikana humo unilee na kunitunza katika uzee wangu. Na wala hautafanya Bure, kazi yako Hii itakulipa na muda wako nitaulinda na kuuheshimu, utalisha familia yako kupitia Mradi huu. Lakini ni Ombi langu nami unilee kupitia kidogo hiki ambacho Mungu alinijalia katika mapito yangu. Na sitaki useme Baba yako nilikuelemea, nilikuchosha, na sikuwa Baba Bora kwako"
Hivy ndivyo utakavyofanya, na sio vinginevyo.
Jasho Lako, nguvu zako ulizowekeza Kwa miaka mingi ndizo zitakazokulisha.
Wanasema utavuna ulichokipanda, msemo huo unaenda sambamba na ule usemao Watu hawavuni maembe kwenye Mapera. Bali huvuna maembe kwenye mti WA mwembe.
Kama utatumia Mali zako vibaya basi hautakuwa na wakumlaumu na hakuna atakayekuwa na wajibu juu yako.
Mungu anaposema umtegemee yeye pekee anamaanisha ushike maagizo na amri zake.
Ikiwa utategemea siku moja Watoto wako watakusaidia badala ya kuwasaidia katika Ujana wao, ikiwa utawategemea Watoto ilhali ulipaswa umtegemee Mungu katika Ujana wako Kwa kufuata amri na Kanuni zake ikiwa ni pamoja na kufanya kazi na kujiwekea akiba na urithi Kwa Watoto.
Nakuhakikishia Dunia itawafanya Watoto wako wasipate au wapate vinavyowatosha wao wenyewe na watoto wao pekee na kukusahau wewe mzazi wao na sio Kwa kupenda Bali kukufundisha wewe Kwa Njia ngumu kuwa ulikosea.
Lakini ikiwa utajifunza kumtegemea Mungu basi utajitegemea. Na ukijitegemea basi Watoto wako nao watajitegemea na kuweza kukupa shukrani na hisani.
Wazazi wote ambao wanauwezo na wanatamani kuwasaidia Watoto wao mara nyingi Watoto wao ndio huwaambia kuwa Sisi ndio tunatakiwa kukusaidia wewe mzazi Kwa sababu umezeeka na ulifanya kazi kubwa.
Na Wazazi wengi ambao wanadai na kutaka kusaidiwa wengi wao watoto wao nao huhitaji msaada wa Wazazi wao.
Kanuni ni Ileile usisahau, mwenye Nacho huzidi kuongezewa na asiye nacho hata kile kidogo anachodhani anacho ananyang'anywa.
Vijana acheni kucheza na kutapanya Mali. Jiheshimu, heshimuni jasho lenu. Tumieni Pesa Kwa nidhamu.
Usijesema unatumia Pesa kwani kifo lipo, ndio utakufa lakini vipi Watoto na wajukuu wako ambao utawaacha?
Na vipi la usipokufa mapema?
Nadhani wengi hawajabarikiwa kuwa na Bibi na Babu walikula chumvi yaani wenye age kuanzia miaka 80 Huko.
Kama umebarikiwa kuwaona Babu na Bibi zako Kwa umri huo nilioutaja basi kajifunze Kutoka kwao. Sio uwaulize nop! Bali hata Kwa kuwatazama Maisha yao ya uzee.
Utajua nini unachopaswa kukifanya.
Mwisho; Vijana saidieni wazazi wenu kulingana na uwezo na moyo utakavyokutuma. Wala usielemewe na kuona mzigo. Na wala mzazi asikushutumu na kukushinikiza Kwa Jambo ambalo sio wajibu wako
Taikon Acha nipumzike SASA.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mkuu! Mimi ni mzazi na nina miaka yangu kadhaa zaidi 50. Ulichosema nakupa tano 💯. Hila wazazi tunakosea sana kuweka tumaini kwa watoto ile hali hatukuwekeza kwa hao watoto tunaowategemea watutunze!
Well said! Oa au olewa kwa makabila mengi ya jamii zilizoenda shule wakati ukuchangia kufanikiwa kwao alafu ulete utegemezi wa kumtegemea sijui kwasababu ni mwanangu au mkwe uone!Ukabila Mkuu.
Muliondoa ukabila alafu mnataka muishi kama zamani.
Ukabila pekee ndio unaweza kutufanya tuishi na Wazazi wetu.
Wapemba mara nyingi au wasomali au wahindi huoana wao Kwa wao. Wanaukabila hiyo ndio sababu wanauwezo wa ku-maintain norms na taboos zao kama kuishi na Wazazi wao.
Sasa Sisi wengine viherehere tunapinga ukabila alafu muda huohuo tunataka mambo yanayohusu ukabila yaendelee.
Yapo makabila mzazi anawezà kuishi Kwa Watoto, makabila mengine hayawezi.
Sasa assume hapo umeoa kwenye kabila ambalo kiutamaduni mnatofautiana unafikiri nini kitatokea?
Wazee wa zamani yapo mambo mengi walikuwa na hoja.
Hayo unayo ita maandiko matakatifu ni stori za kutungwa na uongo.Asante Kuhani kwa ushauri mzuri na wenye kujenga. Lakini Kuhani mimi nina swali moja; miaka hii mtu akifikisha miaka 70 au 80, tayari ni mzee, kikongwe asiyejiweza (ki-nguvu, hata kiafya), na anahitaji usaidizi katika umri huo. Ukisoma maandiko matakatifu (biblia), utaona kuwa akina Elia, Henoko, na wengineo, waliishi miaka 700 mpaka 900. Wengine walizaa watoto wakiwa na umri wa miaka 500 mpaka 600. Kwahiyo hawa akina Elia na Henoko walpokuwa kwenye umri wa miaka 70 - 80, ni wazi kuwa walikuwa bado vijana na walitegemewa na wazazi wao. Sasa swali langu ni kwanini leo umri huo (70 - 80) mtu anakuwa mzee, tena kikongwe? Hali hiyo imesababishwa na nini? Au imetokana na mabadiliko ya tabia nchi?
Mkuu, mbona unaamini maandiko katika discipline zingine kama vile jiografia, sayansi, historia, na mengineyo.. Kwanini uone haya ni ya kweli na sio maandiko kutoka kwenye biblia?Hayo unayo ita maandiko matakatifu ni stori za kutungwa na uongo.
Hakuna binadamu aliye ishi miaka 700 mpaka 900 ni uongo.
Mkuu kweli una amini inawezekana mtu kuishi miaka 900?Mkuu, mbona unaamini maandiko katika discipline zingine kama vile jiografia, sayansi, historia, na mengineyo.. Kwanini uone haya ni ya kweli na sio maandiko kutoka kwenye biblia?
Mkuu mbona hiyo ni michache! Methusela aliishi miaka 969, Adamu aliishi miaka 930. Mungu aliwajalia watu wa zamani kuishi maisha marefu.Mkuu kweli una amini inawezekana mtu kuishi miaka 900?
Kizazi hiki bado watu wema wapo na wana mpendeza Mungu kweli kweli.Mkuu mbona hiyo ni michache! Methusela aliishi miaka 969, Adamu aliishi miaka 930. Mungu aliwajalia watu wa zamani kuishi maisha marefu.
Nahisi hii ilitokana na watu wa wakati huo kuishi maisha ya kumpendeza Mungu, yaani hawakuishi katika dhambi kama nyakati zetu hizi.
Watu wanasema kuwa mshahara wa dhambi ni mauti, huenda hili ndilo linalotugharimu kizazi hiki; tumekuwa tukimkosea sana Mungu na hivyo kupelekea kutupunguzia umri wa kuishi.
Mpango wa Mungu ulikuwa kuwa binadamu aishi milele (bila kufa), lakini baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi pale bustani ya Edeni, ndipo walimuudhi Mungu, na kupewa adhabu ya kifo.
Tangu zama hizo, dhambi zimekuwa zikiongezeka vizazi hadi vizazi, na ndio maana hata umri wa kuishi umekuwa ukipungua kizazi hadi kizazi. Unaona hao akina Methusela waliishi zaidi ya miaka 900 (three digits), lakini leo hii, mtu akiishi miaka mingi sana ni miaka 90 (two digits).
Trend inaonyesha kuwa kama hatutabadilika (kuacha dhambi), basi muda wowote umri wa kuishi utarudi mpaka tarakimu moja (single digit)! Yaani mtu akijitahidi sana, atafikisha miaka 9, hapo ni mzee kikongwe anasubiri kifo!
Ni kweli kuwa kuna watu wema na wenye mapenzi mema kwa Mungu wetu, tatizo watu hao wapo katika dunia ileile iliyonajisiwa na hivyo nao kupakwa matope! Kumbuka Mungu naye ana nafsi, hivyo huchukizwa kama tunavyochukizwa sisi binadamu. Huyo mtu mwema hawezi kuepukana na watenda maovu wote wanaomzunguka; lazima kwa namna moja au nyingine atashirikiana nao, na hivyo naye kuwa na harufu ya maovu. Huyu anasababishiwa na wengine japo yeye hataki. Vinginevyo mtu huyo asikae duniani, jambo ambalo haliwezekani. Dunia inatawaliwa na shetani (huenda pagumu kueleweka hapa). Tukumbuke Mungu ni mtakatifu asiye na doa lolote, binadamu gani anayeishi katika dunia iliyojaa dhambi asiwe na doa? Ni sawa na kusema utembee kwenye mvua, halafu ukwepe matone yote ya mvua, ni jambo lisilowezekana. Tujitahidi tu kujiweka karibu na Mungu, lakini tusiseme kuwa tu wasafi! Yesu alikuwa anawaambia watu, hakuna aliye mwema ila ni Mungu peke yake. Hii inamaanisha kuwa hakuna binadamu asiye na dhambi!Kizazi hiki bado watu wema wapo na wana mpendeza Mungu kweli kweli.
Vipi je mbona Hawawezi fikisha hiyo miaka?