Tuweke hisia pembeni Israel ni ya Waisrael

Ilikuwepo wapi? Weka ushahidi.
Hawz kuwa na ushahidi kwa sababu ye mwenyewe amedanganywa 🤣🤣 Anataka aje adanganye na yeye Watu wazima kama sisi 🤣🤣🤣

Kuna kimsemo huwa nakipenda kuwa Mtu mzima kumwambia mtoto neno la kitoto huwa ni Ishara ya Upendo na kujali..

Ila mtu mzima kumwambia Mtu mzima mwenzake Jambo la kitoto Huwa ni dharau...

Kama anao ushahidi Bila kuweka Mythology nimekaa pale Nasubiria
 
Ugomvi huu soon Mungu atauamua mwenyewe na hasara itakuwa kubwa sana kwa dunia na upande mmojawapo na wale watakaokosa fursa ya unyakuo
 
Hapana umekufuru ndugu.
ijumaa kwa mujibu wa Imani ya Kiislam ni siku ambayo Nabii Adam alizaliwa, Quran ilishuka siku ya Ijumaa na inasemekana siku ya hukumu(Qiyama) itakuwa ni siku ya Ijumaa.
Hivyo kutokana na umuhimu huo ndipo ibada ya Ijumaa ikawa na nguvu kwa waumini wa dini ya Uislam kujumuika pamoja na kumuabudu Allah(S.W.W).
Wallah Allam...
 
Hivyo vitabu vinavyoandikwa na waarabu Koko ku justfy uhuni wanaomfanyia Taifa teule la Izrael? Kitabu Cha rejea ni biblia hakuna kingine labda tora ya wayahudi zaidi ya hapo ni propaganda za kijinga
Biblia inathibitisha kuwa waisrael ni wavamizi hapo
 
Umesema sehemu iliyogawanywa ni Gaza. Nakusubiri uje utolee majibu.
Ndio.

Ukanda wa Gaza na Ukanda wa Magharibi ni maeneo halali ya Wapalestina lakini baada ya vita kubwa ya siku sita au Six Days War ya mwaka 1967 Israeli wakaingia mazima ndani ya Gaza na kuitawala hadi leo kwa kuweka masharti kadha wa kadha.

Mji mkuu wa Taifa la Paletina ni Gaza au Gaza City na unatambuliwa na mkataba wa Oslo au Oslo Accord.

Miji ya Gaza na Ukanda wa Magharibi imetenganishwa na katikati ipo Israeli lakini ukanda wenyewe wa Gaza unatawaliwa na Hamas ambao walishinda uchaguzi mwaka 2006.

Baada ya Hamas kuanza kuutawala mji wa Gaza Israeli wakaleta sheria za kufunga njia zote za ardhini, angani na baharini (kutokea Bahari ya Mediterranean) hatua ambayo imekuwa kwa miaka yote hii ikizuia shughuli mbalimbali za kiuchumi , kuingia na kutoka kwa wapalestina kiasi cha uanda huo kuitwa ni gereza lilo wazi.

Sasa utauliza hawa raia waishio Gaza wametokea wapi?

Kama nilivyoelezea hapo juu, jibu ni kwamba baada ya Uingereza kufanikiwa kulitengeneza taifa la Israeli mwaka 1948 wale wapalestina au waarabu waloondoshwa katika maeneo mapya ya Israeli wakiwa wakimbizi wakaingia hapo Ukanda wa Gaza na kufanya ndo makao yao mapya.

Lakini humohumo wamo wapalestina waislamu na pia wapo wapalestina wakristo ambao ni sehemu ndogo sana.

Turudi kwenye suali lako kuhusu mgawanyo wa Gaza.

Kihistoria Gaza ilikuwa ni sehemu ya himaya ya Ottoman wa Uturuki na baada ya vita kuu ya kwanza kwisha mwaka 1918 Uingereza ikajitwalia sehemu hiyo. Baadae Misri ikatawala eneo hilo ( la Ukanda wa Gaza) baada ya Uingereza kuondoka na Israeli kuwa taifa rasmi mwaka 1948.

Lakini Uingereza hawakutamka rasmi nani wanamwachia eneo hilo na kuona hivyo Misri ikajitwalia eneo hilo tokea mwaka 1948 hadi kulipotokea ile vita kubwa ya kwanza kati ya waarabu na Israeli ya mwaka 1967.

Hivyo tokea mwaka 1967 Israeli inatawala ukanda wa Gaza kwa mabavu na kinyume cha sheria za kimataifa na mkataba wa Oslo ndo kidogo umeruhusu wapalestina nao wajitawale lakini wakiongozwa na Hamas.

Kwahiyo ni kama vile ukanda wa Gaza watawaliwa na Israeli lakini una serikali ya Hamas ambayo ilishinda uchaguzi mwaka 2007.

Hivyo ukiunganisha Dots hapo utaona kiini cha mgogoro huu.

Nafikiri ntakuwa nimekupa nuru ya kutosha kwenye hili.
 
Soma historia acha hizi hadithi za juzi, fukua historia ya tangu au kabla ya hapomahali kuitwa Palestine, au hao wanaojiita Wapalestina kabla hawajatokea Misri na kuhamia hapo, weka pembeni vitabu vya dini, isome historia kamili ya hapo mahali.
Nilokieleza hapo juu ndo historia yenyewe na haihusiani na kitabu chochote cha dini.

Waisraeli hawakuwa na eneo rasmi na walitafutiwa maeneo sehemu mbalimbali lakini hapo Palestine ndo wao walikwenda wengi wakiwa ni walowezi.

Ehud Barak ambae alikuwa waziri mkuu wa 10 wa Israeli amezaliwa hapo Palestina ilokuwa chini ya uangalizi wa Uingereza.

Mkuu, mimi nimepiga historia uzuri tu na sijasahau.

Kumbuka History is about past, present and future.

Your job is to dwell between the three as its important to understand context and the circumstances which lead to these ongoing events in the middle east.

I believe, you are smart person and you don't fit in wishy washy type of thinking.
 

Ukifuata historia vizuri hata kabla hapajaitwa Palestina utaona hao mnaosema waliumbiwa hapo walitokea Arabia...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…