FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Mwaka huu wa 2022 unatuingiza mwaka wa 61 toka Tanganyika tupate Uhuru.
Kwanza na "declare interest", binafsi nimezaliwa Tanganyika, kwa maana nimezaliwa kabla ya Uhuru na kabla ya muungano. Namshukuru Mwenyezi Mungu nimezipitia awamu 7 za uongozi wa nchi yetu hii ambayo sasa inaitwa Tanzania. Nimepitia awamu ya utawala wa Muingereza kwa kuzaliwa kabla ya Uhuru na na nimepitia awamu zote zilizofatia baada ya Uhuru.
Nimeiishi historia yetu, mengi nayatazama kwa mtazamo wa 'nilikuwepo". Kwa kuwa historia ya nchi huhusisha mambo mengi na awamu nilizopitia zilipita kwenye aina nyingi za kisiasa, kiuchumi, kimichezo, kijamii na kimaisha kwa ujumla. Nafahamu uzi huu utaibua hisia na mitazamo tofauti. Tuujadili kiuungwana, kwa heshima na taadhima na tuvumiliane mitazamo yetu, kwani kila mmoja wetu anayo anayoyafahamu kwa mtazamo wake a kwa kusikia kwake au kwa kusomeshwa kwake.
Kuna yaliofurahisha na kuchukiza katika historia yetu kwa kila mmoja wetu kwa muono wake.
Kwa mtazamo wangu, Mwalimu Nyerere alifurahisha alipoongea, alikuwa ni muongeaji mzuri na mchekeshaji mzuri. Katika uongozi wa nchi, naamini kabisa Nyerere alishindwa kabisa katika mambo ya uchumi.
Tuendelee....