Tuweke Historia Sawa. Tuwajadili Marais wa Tanzania tukianzia na Nyerere

Tuweke Historia Sawa. Tuwajadili Marais wa Tanzania tukianzia na Nyerere

Kwangu mimi Mwl Nyerere ni number moja lakini wakati huo huo ni kiongozi wa hovyo.

Alituachia katiba mbaya.
Alituachia uchumi mbaya.
Alituachia muungano mbaya.

Mwl Nyerere hakuwa mwizi wa rasilimali za umma.
 
Hapo kwenye kufeli kwa uchumi nakuunga mkono.
Ishu ya ujamaa haikuwa sahihi kabisa. Ilileta uvivu sana. Ona wenzetu Kenya.
Kimlolongo wa madaraka Mkapa alitakiwa awe Rais wa kwanza
Sera za Magufuli ndio alitakiwa awe rais wa kwanza au wa pili.
Kikwete angefuata then hao waliobakia walitakiwa waje mwaka 2355
Nyerere kauli zake na maamuzi yake yalikuwa yanajipinga (contradictory), anahubiri "ujamaa na kujitegemea" wakati huohuo anataifisha mali za watu na kuzifanya za "umma".

Kama si kujipinga ni nini huko, kuna kujitegemea au kutegemea hapo?

Ukija suala lingine, alikuwa anasema "Afrika Ni Moja" na anahimiza iungane, Akaung'ang'ania muungano wa Zanzibar na Tanganyika, lilipokuja suala la Biafra akahimiza na akasaidia Biafra itengane na Nigeria! Sasa kama si vituko ilikuwa ni nini zaidi?
 
Nimezaliwa kipindi cha awamu ya BWM...kwangu mimi hawa ndio marais bora.

1.J.K Nyerere
2.BW.Mkapa
3.JM.Kikwete
4.Mwinyi
5.Samia(Huyu bado tunampima uwezo wake ingawa kuna mengi anafanya vizri tumpe muda.)

Kwanini nimeweka hivyo hilo list kwanza hao watatu wa mwanzo walikuwa ni Nationalist walioamini Maendeleo ya nchi hii yanaletwa na wananchi wenyewe kwakufanya kazi na kujitegemea wenyewe bila kutembeza bakuli.

Waliamini zaidi katika uchumi wa nchi kupitia rasilmali zetu.

Walipo feli ni kwenye suala la muungano hasa Nyerere kuwakribisha wazenji na kuwalea kama watoto mayatima.

Pia suala la demokrasia haikuwa huwa kipaumbele chao waliamini katika mlengo wa siasa za chama kimoja tu.

Naendelea kujifunza hayo ni maoni yangu

Naomba wafia dini za kuletewe muwe na ustaarabu tujadili hii mada kwa utuvu na weredi

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
nyerere alipokea uhuru
akaongoza nchi kwa miaka 20+ ila akuucheza mwing
 
Hakuna Cha maana mnachojadili zaidi ya UPUMBAVU tu.

Naona mmemiss sana kumtukana Nyerere.

Haya, Nyerere, Mkapa na Magufuli walikuwa Marais wabovu.

Mwinyi, Kikwete na Samia ni Marais BIRA KABISA.

Nimemaliza. Furahini sasa.
Alive
Marais wangu bora wa muda wote, hapo kuna Striker na attacking midfielder's
1 Samia
2 mwinyi
3 kikwete

Marehemu
Nyerere
Mkapa
Magufuli
 
Hakuna Cha maana mnachojadili zaidi ya UPUMBAVU tu.

Naona mmemiss sana kumtukana Nyerere.

Haya, Nyerere, Mkapa na Magufuli walikuwa Marais wabovu.

Mwinyi, Kikwete na Samia ni Marais BIRA KABISA.

Nimemaliza. Furahini sasa.

Tena walikua wabovu haswaa
 
Back
Top Bottom