I thought you have grown into a wise old lady as you grow older, you become wiser..., kumbe I was wrong!. Zamani kila ukimtaja Mwalimu Nyerere, ulikuwa ukimtukana laanatulah, kitendo tuu cha kumtaja Mwalimu Nyerere this time bila kumtukana, it's a good start ya kuzeeka vizuri maana...
P
Pascal,
Kuna mambo yanasikitisha yanapotokea.
Mwaka wa 1995 nilialikwa na jumuia moja kuzungumza Mnazi Mmoja katika muhadhara.
Wazungumzaji walikuwa wengi na mimi nilipangiwa kuzungumza baada ya Isha.
Msikiti wa Manyema ni jirani sana na Viwanja Vya Mnazi Mmoja na pia Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba Avenue.
Baada ya sala natoka nje niende Mnazi Mmoja nikakutana na marehemu Sheikh Aboud Maalim, mmoja wa masheikh wenye kuheshimika sana.
Nikamwambia, ''Sheikh nimepangwa kuzungumza hapo Mnazi Mmoja na hivi ndiyo nakwenda lakini naogopa sana.''
Sheikh akanijibu, ''Unawaogopa watu au unaogopa mada yako?''
Shekh akaniombea dua nikaondoka.
Nilikuwa naogopa kwa sababu nilikuwa sijapata kuzungumza katika uwanja wa wazi na umma ulikuwa umefurika.
Miaka ile Waislam walikuwa wamekuja juu sana wanauliza mengi serikalini.
Mada yangu ilikuwa ''Historia ya Uhuru wa Tanganyika.''
Katikati ya mhadhara nikataja jina.
Nikapokelewa na kibwagizo.
Nilipigwa na mshangao kama nimesikia sawasawa au vipi.
Hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kusikia kibwagizo hicho lakini nikawa kama vile akili yangu inakataa kuamini kama kweli nimesikia sawasawa.
Nikakisikia tena kibwagizo kile.
Niliingiwa na hofu na njia pekee kwangu ikawa ni kuacha kulitaja jina lile.
Nilishangaa kuwa hapo ndipo tulipofika.
Asubuhi hata saa nne haijafika cassettes za ule muhadha wangu ziko mitaani zinauzwa na zinanunuliwa kama vitumbua vya moto.
Nilialikwa Zentrum Moderner Orient (ZMO) Berlin kufanya mhadhara na mada yangu ilikuwa historia ya uhuru wa Tanganyika na mashujaa wake waliosahauliwa.
ZMO ni taasisi kubwa sana katika utafiti wa historia.
Katika mhadhara wangu nilieleza jinsi Tanzania ilivyobadilika na nikaeleza yale yaliyonifika Mnazi Mmoja.
Mhadhara wangu uliwafadhaisha wengi katika yale waliyosikia kutoka kwangu na wakaniambia kuwa wamepita wahadhiri wengi kutoka Tanzania na wamezungumza historia ya uhuru lakini yale waliyosikia kutoka kwangu yalikuwa mageni masikioni mwao.
Siku ya kuagana Mkurugenzi wa ZMO aliniita ofisini kwake na kuniuliza maswali mengi lakini swali moja ambalo lilinigusa sana ni pale alipotaka kujua nini kimesababisha hali ile?
Wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika mama zetu katika mikutano ya TANU walikuwa wakitengewa sehemu maalum wasichanganyike na wanaume.
Akina mama hawa walikuwa na wimbo wakiimba katika mikutano ile ubeti wa mwisho ulikuwa unasema hivi., ''In Shaa Allah Mungu yupo Tanganyika tutajitawala.
Naweka picha moja ya mikutano ya TANU ya mwanzo na tazama kushoto utaona weusi hayo ni mabaibui waliyokuwa wanavaa mama na shangazi zetu.
Pascal.
Ulikuwa unaujua wimbo huu au historia hii?
Umepata kujiuliza kwa nii leo imekuwa hivi?
Chuki hizi nini sababu yake?
Picha kwa hisani ya watoto wa Mohamed Shebe aliyekuwa mpiga picha wa TANU kwa kujitolea.