Tuweke Historia Sawa. Tuwajadili Marais wa Tanzania tukianzia na Nyerere

Baba wataifa ametusaidia sana kwenye kujenga umoja ila alibug sana kuforce muungano wa tanganyika na zanzibar..mpk leo sijawahi kujua aliwaza nn!
 
Hili jambo unalolizingumzia halina upya wowote, kila siku unaliongelea, labda km ni jipya ktk uzi huu ila kwa sisi tunaokufahamu humu ndani hakuna jipya...its too boring, plz tuambie kitu kipya ambacho hujawahi kukisema kt nyuzi nyingine.
Gobole,
Naona umeghadhibika.

Nasema jipya kwa kuwa toka uhuru historia iliyokuwa imetamalaki ni hii historia rasmi ambayo wewe na wengine wengi mkisomeshwa.

Ninaposema historia mpya ni hii niliyoandika, ",The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika."

Niliposema mpya nilikusudia historia iliyomo katika kitabu hiki.
Nakubali kwako inaweza kuwa inachosha na "boring," lakini hii isikupe shida.

Uamuzi ni wako.
Acha kunisoma utakuwa umenusurika.

Kalamu yangu inachoma.
Inakata kama upanga.

Maneno yangu ndani ya historia ya TANU yanakuumiza hukuwahi kuyasikia majina unayosoma wala historia za wazalendo hawa.

Wala hukupata kuona picha zao wakiwa bega kwa bega na Julius Nyerere wakipambana na mkoloni.

Nafsi yako ya ndani inakuambia, "Hii ndiyo historia ya kweli bahati mbaya ilifutika."

Lakini tambua pia nina wasomaji wengi sana na wananiandikia kiasi siwezi kuwajibu wote.

Vitu vipya ninavyo vingi sana.
Kuna publisher anapitia kazi zangu kanistaajabisha mno.

Anasema kwa haraka anakisikia nina makala 10, 000.

Nimepita kwa haraka nimeshangazwa sana makala nyingine sikumbuki kuziandika wala mwaka wake.

Nafikiri kuanza kuziweka hizi hapa barzani.
Unawajua wazalendo hao hapo chini?

Umepata kuziona picha hizi popote kabla sijaziweka hapa?
Unajua historia zao?


February 1955


1956
 
Binafsi mimi Rais Shujaa wetu ni Nyerere

Na Rais fala kuliko wote ni mwendazake wa Chato. Tuendelee kumshukuru Mungu kwa kila jambo

Cc: mbunge wa chato MENGELENI KWETU
 
1. Julius Kambarage Nyerere
2. Samia Suluhu Hasan
3. Jakaya Mrisho Kikwete
4. Benjamin William Mkapa
5. Ally Hassan Mwinyi
6.. John Pombe Magufuli

Kila mtu ashinde mechi zake
 
1. Julius Kambarage Nyerere
2. Samia Suluhu Hasan
3. Jakaya Mrisho Kikwete
4. Benjamin William Mkapa
5. Ally Hassan Mwinyi
6.. John Pombe Magufuli

Kila mtu ashinde mechi zake
1. J. K.Nyerere
2. B. Mkapa
3. Samia
4. Kikwete
5. JPM
 
Glenn,
Hapana udini hapa.

Naeleza historia ya uhuru wa Tanganyika na mchango wa Waislam katika kupambana na ukoloni.

Mimi sioni kama ni udini.

Ukiwa unataka tujadili udini nina mengi tofauti kabisa na haya unayosoma hapa.

Fungua uzi mpya utahakikisha ninayokueleza kuwa hii ni historia ya mchango wa Waislam katika kuunda TANU - 'a field of enquiry.''

Kwa nini niliamua kufanya utafiti na kuandika kitabu ni kuwa hii ni historia yangu ya wazee wangu na jamii yangu iliyofutika au kufutwa kwa kudhamiria.

Hii ni historia ya vizazi vitatu iliyokuwa hadi 1998 imeandikwa popote historia inayoanza mwishoni mwa 1800.

Historia hii inamuhusu sana babu yangu Salum Abdallah.

Yeye alikuwapo African Association ilipoundwa na alikuwapo TANU ilipoasisiwa na kashiriki kwa hali na mali kupigania uhuru wa Tanganyika.


 
Umahiri wa kuongea ni moja ya sifa kubwa sana za Nyerere, ni kipaji bila shaka.

Nakumbuka nilisoma mahala aliwahi kuhutubia Umoja wa Mataifa mada inayohusu "mipaka ya outer space" licha ya "standing ovation", Nyerere alibebwa akishangiliwa (katika late 70s au 80s". Mwenye kumbukumbu hiyo atatuletea hapa. Hiyo ilitokana na "eloquence" yale na mbinu yake ya kuhutubia kama anapiga "story" ambayo waongeaji woyte wazuri huwa ni hivyo.

Kama usemavyo kuongea ni "usanii" basi nikukubalie alikuwa ni msanii kweli kweli "wa kiwango cha lami".

Kuhusu suala la ujamaa, hakuna aliyemsaliti, bali kwa mtazamo wangu alijisaliti mwenyewe kwa kutokuelewa alitakalo, maana huku alikuwa anatuhimiza "ujamaa na kujitegemea" wakati huo-huo anataifisha mali za watu na kuzifanya "mali za umma". What a contradiction.
 
Si tatizo la kutumia au kutokutumia mtaji.

Kumbuka kuwa Nyerere aliichukua nchi ikiwa ni msafirishaji wa kwanza wa mazao ya mashamba katika Afrika, nchi yenye rasilimali tele, yenye miundombinu inayojitosheleza kwa wakati huo.

Matokeao ndani ya miaka 10 tukawa masikini wa mwisho na omba omba wa kwanza katika Afrika. Hadi hii leo, kwa maneno ya "Bwana Mapesa - "Nchi omba omba". Haujatuishia licha ya jitoihada za Kikwete kutuonodoa katika kuomba bajeti yetu toka asilimia zaidi ya 60 mpaka kutufikisha chini ya asilimia 40.

Katuachia misingi mibovu ya uchumi ambayo itatuchukuwa muda mrefu sana kujing'atua kutoka kwenye umasikini.

Nadiriki kusema, misingi mibovu aliyotuachia inatupelekea hadi leo hii hatupo huru kiuchumi kama nchi.
 
Ukiona uzi wowote wanashirikiana FaizaFoxy na Mohamed Said ujue kuna lengo maalum la kuchafua dini fulani au viongozi fulani.

Mambo yatajifunua kadiri watu watakavyoendelea kuchangia.
Weka ushahidi.

Jukwaa hili liko wazi, wacha porojo na "character assassination" kwa uoga wako tu.

Wewe hapa ukiona huafikiani na hoja ya yeyote si unaweka hoja yako? Kama huiafiki hoja yangu yoyote upo huru kuweka hoja zako, kama siziafiki nipo huru kuweka hoja zangu.

Kuna tatizo lipi katika hayo? Au unataka kuukimbia/ tuukimbie ukweli?
 
Binafsi mimi Rais Shujaa wetu ni Nyerere

Na Rais fala kuliko wote ni mwendazake wa Chato. Tuendelee kumshukuru Mungu kwa kila jambo

Cc: mbunge wa chato MENGELENI KWETU
Tupe sifa za "shujaa" wako kivyako. Binafsi nimemsifu kwa kuwa ni muongeaji mzuri sana.
 
Ukiona uzi wowote wanashirikiana FaizaFoxy na Mohamed Said ujue kuna lengo maalum la kuchafua dini fulani au viongozi fulani.

Mambo yatajifunua kadiri watu watakavyoendelea kuchangia.
Gun...
Huenda wewe ni mgeni na mimi na hujanisoma au si mgeni lakini hujanisoma vya kutosha.

Ingekuwa mimi naandika ili kuchafua dini nisingedumu hapa JF.
Mimi nimepewa tuzo na JF kwa uandishi wangu wa historia:


Maxence Melo akinikabidhi ''Cerificate of Appreciation.''
 
Safi kabisa mkuu umenena vilivyo
 
Kwa mtazamo wangu, Mwalimu Nyerere alifurahisha alipoongea, alikuwa ni muongeaji mzuri na mchekeshaji mzuri. Katika uongozi wa nchi, naamini kabisa Nyerere alishindwa kabisa katika mambo ya uchumi.
Tanzania imewahi kupata marais wawili tu, Nyerere na Mkapa. Wanabaki kuwa marais bora wa nyakati zote. Ninaamini walimaliza vizuri na Bwana Yesu Kristo na sasa wapo sehemu salama.
 

"...Nasubiria kwa makini to get the real motive behind this thread.."
 
Tanzania imewahi kupata marais wawili tu, Nyerere na Mkapa. Wanabaki kuwa marais bora wa nyakati zote. Ninaamini walimaliza vizuri na Bwana Yesu Kristo na sasa wapo sehemu salama.
Kama ni kwa mtazamo wako huo wa jina la Yesu, upo sahihi. Lakini kiuchumi naamini Nyerere alishindwa. Kwa Mkapa bado sijafika katika gumzo hili.
 
Walipigania uhuru kama waislamu au kama watanganyika?

Naona uzi huu mmejazana watoto wa upande ule ili kueneza udini.
 
Hawa waliitana kuja kueneza dini. Wamejaa uzi mzima.
 
Ok tuanze na wewe uliyeanzisha mada,nini unachokijua kwenye historia ya nchi hii,nini unadhani kipo,na kipi hakipo,nn kiongezewe au kiboreshwe katika historia yetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…