Tuweke kumbukumbu zetu sawa, huu ndo uchumi wa Magufuli aliouacha, all facts! - Sehemu ya kwanza

Naamini kabisa pamoja na kwamba upo Nje ya BUNGE mchango wakoo huu ulio uwakilisha hapa ni zaidi ya wabunge waliopo BUNGENI

Mungu akubariki
 
Nawashangaa wanaobishana na WB walio ona uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi. Hadi tukapanda kuwa uchumi wa Kati. Watu wanakuja na takwimu zao za kishule shule hapa badala ya actual economy. Moja ya uchumi kukua ni uimarishaji wa huduma kwa wanannchi, hii ni pamoja na afya, Elimu, na miundo mbinu.
Watanzania baadhi walizoea ubadhirifu wa mali ya umma. Sekta binafsi ilitegemea michongo, kuonga na kujichukulia fedha ya serikali na kutoa huduma dhaifu. Mfano makandarasi wengi walijenga barabara au majengo ya serikali yasiyokuwa na kiwango huku wakiwa wamelipwa fedha nyingi. Hela iliyokuwa ikizagaa mtaani ilikuwa fedha ya dhuruma, madawa ya kulevya na ubadhirifu.

Nchi za Ulaya huwezi kuta fedha inazagaa mtaani. Sweden ni moja ya nchi ambayo ni wakali kwa kodi. Hawabembelezi mtu hata awe mfanya biashara mkubwa. Kuna baadhi ya mashirika makubwa ya biashara Sweden yamehama kwa kulalamikia kodi. Na utaratibu wa kulipia kodi Sweden ulianzishwa na kusisitizwa kwa lazima na aliekuwa mfalme wao Gustav, wanasema huyu watu walimchukia kwa ajili ya kuhimiza kodi. Lakini leo wanafurahi na kumkumbuka kuwa ameifanya Sweden kuwa kama leo ilivyo.
Katika serikali ya kikwete, kulikua na mambo mengi machafu, fedha ilichotwa. Hakukuwa na huduma kwa wananchi iliyowawezesha. Watu wa juu kimaisha waliendelea kuwajuu, na masikini aliendelea kuwa masikini.

Nakumbuka naanza kazi, ikaletwa orodha ya malipo ya mshahara, ambayo mimi na mwasibu wangu tulikuwa tunaipokea na kukagua kama wafanyakazi wote wamepata haki zao. Kilichokuwa kinanishangaza na ugeni wangu katika utumishi wa umma, katika orodha ya malipo ya mshahara kulikuwa na majina yapata kumi. Hawa watumishi sikuwajua na sijawahi waona ofisini. Nilimuuliza mhasibu kwani yeye alikuwa mtu mzima ambae kesha kaa katika utumishi yapata miaka 30. Akanambia aya majina hawa watu wengine walishafariki, na wengine kuacha kazi, lakini mishahara yao inaingia hiyo fedha ni ya wakubwa. Nilimwambia tuzuie. Akasema haiwezekani kwani huo ni mtandao mkubwa unaanzia juu. Hii niliiona kwa macho yangu na kushuhudia.

Utawala wa Kikwete posho zilikuwa nyingi. Mtu unaweza pokea posho mbili hadi Tatu wakati umeshalipwa kwa kazi husika. Watu hawakufanya kazi kilichotazamwa ni posho tu. Nilikuwa na ndugu yangu ambae yeye, alikuwa akiingia Bank kuu, anachota pesa huyu alikuwa na wakubwa fulani wa hii nchi. Aliweza ingiza watu weki bank kuu kufanya kazi na baadhi ya mashirika makubwa kama PSPF na kadhalika. Alikuwa na fedha haswa. Lakini baada ya Magufuli kuingia mirija yote ilikata.

Wakati wa Kikwete, wanafunzi wengi waliofahulu walishindwa kwenda shule, kwa kukoswa uniform, ada na michango ya madawati au mingineyo. Nakumbuka nikiwa mtumishi wa umma, ilinibidi kusomesha watoto 10. Pia niliongea na baadhi ya mashirka kuwasaidia baadhi ya wanafunzi wapatao 80 hawa walisomeshwa na hayo mashirika. Na hawa wanafunzi wengi wao walikuwa masikini wa kutupwa katika familia zao.

Naongea vitu ambavyo nilivishuhudia mwenyewe. Situmii theory ya kukariri darasani la asha. Nilishuhudia matajiri wakubwa wenye uwezo walivyokuwa wameiweka serikali mfukoni. Watumishi mbalimbali walionewa na kunyimwa haki zao hasa katika sekta binafsi. Kuna issue moja ya wahindi ambao baada ya kumsaidia mtumishi mmoja alodhulumiwa haki yake. Mmoja wa wahindi hao ambae ni mfanya biashara mkubwa linipigia simu na kunisihi niachane na hilo jambo. Nilipomkatalia alinitishia na kusema ataongea na Rais.
Nilimwambia ongea nae. Kipindi hicho kulijaa dhuruma na ufisadi wa hali ya juu. Wakubwa wengi walishiriki kuuza madawa ya kulevya na kujipatia mamilioni. Tunawajua!

Leo mnaanza mlaumu Magufuli, wengi wenu manaotoa hizo lawama ni wale mirija iliyokatwa. Ndo maana mnamchukia. Huwa najiuliza hivi Magufuli aliingia katika kila nyumba na kuchukua fedha zenu au mishahara yenu? Swala la kuongeza mishahara kwa kutangaza hilo ni lakizamani na limepitwa na wakati. Hakuna nchi duniani zilizoendelea zinazotangaza kuongeza mishahara. Nimebahatika kufanya kazi nje, sijawahi ona rais au waziri mkuu wa nchi akitangaza ongezeko la mishahara.

Mfano katika sehemu nayofanyia kazi. Wanatumia tathimini ya kazi. unapewa fomu unajikadilia utendaji wako wa kazi kwa kujipima. Baadae unakaa na Mkuu wako wa idara mnapitia kwa pamoja kile ulichojipima, mnajadiliana. Ile fomu itakwenda kwa jopo ya maafisa utumishi pamoja na mkuu wako wa idara kulingana na fomu ulojaza utapata ongezeko lako la mshahara. Hivyo mshahara unapandishwa kulingana na perfomance yako kazini.
Tanzania tunajaza hizo fomu lakini hakuna kinachofanyika hata cheo hupandishiwi. Mpaka mkuu wako atakapo jisikia.
Hongera Magufuli kwa ulipotumika. Pumzika kwa amani. Ila ipo siku watanzania watatamani wangekuona tena.
 
Mkuu fungua tutakusapoti NSSF ni janga
 
Dah..!! Mkuu umeongea ukweli mtupu.
 
Mtazamo wangu magufuli alifunga mikanda NA nilijua tutapita hapa NA kuumia ilikua ni lazma. Sasa ndio maana ya kuisoma namba. Ili kesho tuwe pazuri lzma kuumia leo
 
Ni bahati mbaya sana nchi kuongozwa na mtu asiyesikiliza wataalamu bali anaendeshwa na instinct zake mwenyewe.....watu wanaomshauri kinyume wanaonekana wapiga dili au wametumwa na mabeberu.
 
Mwendazake alikuwa anajiona yeye ana akili kuliko watanzania wote milioni 60. Mtu gani hataki ushauri anafanya kazi kwa mawazo yake peke yake. Nadhani ni ile PHD ndio ilikuwa inampa kibri.

Sasa sisi tunaostaafu miaka 20 ijayo lazima tujue kabisa Mwendazake hajaacha kitu kwenye mifuko ya pensheni. Tusije tukapeleka lawama kwa mama bure. Nchi hii haijawahi kupata kiongozi wa hovyo kama huyu mzee.
 
Sasa usilaumu wanaoweka thread usizopenda wakati wasipoweka hizo, ww/nyinyi mlio neutral hamtaweka kabisa. Hayo mengine kwenye post yako nimeshindwa kuyaelewa.
😂😂😂 dahhh ...
Mkuu nilitoa compliment tu na ningeomba yaishe haya maana hakuja haja ya kujibizana kwa kitu kilicho nje ya mada kwa sasa...

Pasaka njema in advance
 
Yeye ndie alikuwa anasema wamachinga wasisumbuliwe wafanye biashara popote. Watendaji wake unawaonea tu.
Kuwaacha machinga hakumaanisha wasitafute njia bora za kuwasaidia kuongeza tija badala ya hasara...Watendaji wengi walitoa majibu mepesi yasiyo na tija...Nikupe mfano waliwasaidiaje machinga kuunganisha mitaji yao ili kweli waweze kubaki kwenye complex yao badala ya kuwa wanatembeza bidhaa?

Kutembeza bidhaa pia ilikuwa market strategies za wafanya biashara wakubwa je walitumiaje hiyo mbinu ku improvise ili iongeze tija?

Wao walichokuwa wanajua ni kutumia mgambo tu na fimbo kuwafukuza machinga kama vibaka vile na siyo raia ambao waliwapa kura viongozi wa nchi; Magufuli kama mwanasiasa yeyote yule ambaye nafasi yake inahitaji kura asingekubali hilo na hapo alionyesha umahiri wake katika kuzilinda kura zake...Ila kama mwanasiasa yeyote asingekataa kupokea options zinazoongeza kodi na kuzilinda kura zake yaani machinga wakaendelea kumwona ndiyo mtetezi wao, huo ndiyo utaalamu ambao wataalamu wetu wengi wanaukosa na kubakia kulala kwamba wanasiasa wanawakwamisha...At the same time kwakukosa ubunifu huo hata uchumi unashindwa kuongezeka yet bado wanataka mishahara mikubwa...Haiji hiyo!
 
It is an excellent piece of information. Continue producing more facts. I remain your keen consumer.
 
Amekuza sana pia tabaka la wanyonge. Mama ntilie, wamachinga na boda boda.
 
Cost accountants and economists bail us out of this calamity: Which is a cheaper and reliable source of electric power in the TZ environment? Please come up with quantified argument.
 

Maelezo yako ni mengi, lakini naomba nikusaidieje kitu, Magufuli hakuwa anategemea kura hata moja ya mpiga kura kuwa rais. Hivyo wakati unaendelea na hizi hekaya zako, achana kabisa na upotoshaji kuwa Magufuli alitegemea kura ya mpiga kura nje ya vyombo vya dola.
 
Sekta ya gesi zaidi ya kuzalisha umeme ingezalisha maelfu ya biashara za bidhaa, huduma na ajira za moja kwa moja mara nyingi zaidi ya zitakazozalishwa na huo mradi wa umeme wa maji.

Umeme ambao ungezalishwa na gesi ingekuwa pesa za uwekezaji na sio hii mikopo,kutopanda mishahara,ubabaishaji wa pensheni na kodi wanazokamuliwa wananchi hadi wanakonda.
 
Mkuu usiziamini takwimu za Magu hata kidogo hazikuwa na uhalisia ndio maana alipiga marufuku kutoa takwimu.

Kiuhalisia inflation imepanda hii haitaji resaerch ya mbobezi
Kwa hili nitakubali kama layman, lakini inflation ni below 5%. Jee umeona, mchele, ndizi, maharagwe ama mazao yamepanda?

Ni bidhaa za viwandani tuu. Kwa hali ambavyo raia wamepigika, hali mbaya, jee unapandisha bei bidhaa nani anunue ?
 
Bahati mbaya sana "wanyonge" ambao ndio kundi kubwa kabisa katika nchi yetu kwa sasa hawawezi kuelewa huu uchambuzi wako makini sana. Kila nikiongea na dereva boda boda anasema kile kilikuwa ni Chuma na wana shaka kama mkuu mpya wa nyumba ataweza kuendeleza uchuma ule.
 
Bora haujaandika huu uzi kwa kizungu tungetoka hapa 🤭😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…