Tuweke kumbukumbu zetu sawa, huu ndo uchumi wa Magufuli aliouacha, all facts! - Sehemu ya kwanza

Naantombe Mushi
kwahiyo sasa ni kipi kifanyike ili mzunguko wa pesa uwe mkubwa kama enzi za kikwete?
Mama kaanza vizuri, sekta binafsi ilichokikosa kwa Magufuli ni confidence ambayo ilitokana na unyonywaji.. So confidence ikirejea, uwekezeja lazima utaimarika kwenye sekta binafsi, trust me, utaona mabadiliko ndugu yangu.

Wenye pesa hawahitaji bughudha, na Rais Samia ameshawahakikishia hilo, mambo yata improve, na mzunguko wa pesa utaanza kuongezeka, tuombe uzima baada ya miezi sita kutoka sasa... kutakuwa na improvement
 
Binafsi naona hizi ndiyo zile tunasema uchumi wa kwenye makaratasi ila kipindi cha JK tuseme tu ukweli fedha nyingi zilikuwa ni haram na hazikuwa zinaingia kwenye mzunguko ili lilipelekea mtaani hela kuzagaa kiasi ata laki ikaitwa si pesa ola sasa laki tunajua ni pesa.

Wafanyabiashara sikuzote wazo lao la kwanza kukwepa kodi, kipindi cha JK kuna meli 60 ziliwai kutia nanga pale bandarini Dar es Salaam na meli hizo zote hazikuwa recorded mahala popote na mwisho kontena zikapotea kusiko julikana, Zaman kipindi cha JK kontena kupotea huko bandarini kilikuwa kitu cha kawaida, Bandarini hapakuwa na scana ata ya kuscan vitu vinavyopita bandarini.

Nenda pale airport kipindi cha JK hakuna kikicho scsniwa ili kijulikane ni kitu gani...

Mwisho wa siku Magufuli alitamani kujenga Tanzania ya kesho, Magufuli hakuwa mwanasiasa ila alikuwa kiongozi, aliona bora aanze upya kuliko kuendelea na staili waliyotumia watangulizi wake.

Mwisho niseme tu huu wa kipindi cha Hayati ndo ulikuwa uchumi wetu halisi, huko nyuma kulikuwa na wajanja tu wenye kuchuma walivyotaka kuchuma lakini kwenye kujenga nchi hamna kitu.

Nakumbuka kipindi cha JK NGO zilopeta kweli lakini ki ukweli kabisa walikuwa hawalipi ata Tsh 150,000/= kwa mwaka wala hawapeleki ata hesabu zao za mwaka kwa msajili lakini alivyoingia Magufuli aligakikisha kila Wizara inayoona kuna sehemu inatakiwa ikusanye fedha inatakiwa kufanya hivo, hapo ukaanza utaratibu kama hupeleki hesabu zako kwa na hulipi ada shirika lako litafungwa na mengi yalifungwa maana yalikuwa hewa na hewa kweli cos ata mimi mwenyewe nishawah fanya kazi huko najua vyema na mpaka sasa mwenye NGO yake ninahakika anafanya kazi kwa unyofu mno.

Kiuweli tulichekea na tulipata mtu ambae alikuwa anatuambia ukweli, hizi habari za kulembeana na kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa hakuwa nazo.
 
JPM ametwaliwa ili watanzania milioni 60 wapone imagine angeendelea kwa miaka mitano nchi ingekuwaje? Na wale wapuuzi wengine walitaka atawale miaka 20 zaidi Mungu akasema nitaliponya taifa langu Tanzania.
Kuna verse moja hivi ya hip hop inasema..

Hakuna nafsi inayoweza kuwa juu ya mungu, unaweza uka try na mwisho ukawa juu kizungu.../

Kuna nafsi zinajaribu kuwa juu kinguvu, mwisho wanabebwa kama nyanya iliyo juu ya fungu.../
 
Wengine mkisoma mnakuwa msaada sana kwa wale mliowaacha vijijini, well done guy.
 
Mzee alikuwa mpuuzi sana yule! Halafu kuna mataahira yalikuwa yanataka atawale milele!
 
Mkuu umenikosha Kwa uchambuzi huu. Kiukweli tumelia mara nying na kusisitiza kuwa nchi yetu haina uwezo wa kutekeleza miradi ya matrilioni Kwa wakati mmoja lakin Mwendazake akawaamimisha wajinga kuwa sis sio wazalendo.
 
Fungua macho utazame,

1. Unasema enzi ya JK pesa ilikuwa ni haramu, naomba ufafanue kivipi? wakati watu walikuwa wanafanya kazi na kupata pesa, kwani kipindi cha JK pesa zilikuwa zinagawiwa bure? Kwanini useme eti zilikuwa za haramu?

2. Yaani wewe uchumi kudorora, mzunguko wa pesa haupo ndo unasema huo kwako ndo uchumi halisi? Kuwa serious mkuu.. fungua macho utazame tena kauli yako.
 
Nyie unaosema hamna vyama, huwa hamuwezi kuanzisha uzi zenu mpaka msubiri wenye vyama waanzishe? Sasa hapo tatizo ni hao wenye vyama kuanzisha nyuzi zinazobeba vyama vyao, au nyie msio na vyama lakini hamuwawez kujianzishia uzi zenu?


wengine utatuonea tu,
specialization yetu ni kusoma na kuchangia tu

kuhusu hao waanzisha thread zenye nondo, itabidi tuwaeleweshe tu kuwa hata darasa lenye watoto watukutu wasiojali kuhusu shule zaidi ya kupenda ubishi wa Diamond Vs Ali kiba ,
bado huwa wana waalimu wanaomaliza syllabus kwa kutimiza wajibu tu

ijapokuwa huwa wanajua wanapanda maharage wakitegemea kuvuna mahindi..
"wasted energy"
 
Mkuu umenikosha Kwa uchambuzi huu. Kiukweli tumelia mara nying na kusisitiza kuwa nchi yetu haina uwezo wa kutekeleza miradi ya matrilioni Kwa wakati mmoja lakin Mwendazake akawaamimisha wajinga kuwa sis sio wazalendo.
Na hii ndo point kubwa, sio kwamba tulikuwa tunapinga miundo mbinu, ila tulikuwa tunataka serikali iifanye kwa step ili isiparalse uchumi.. umenipata vema hapo
 
Asante mkuu,
 
Waambie wakipata muda wapite na hapa ili waelewe vizuri [emoji116][emoji116]

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…