Tuweke kumbukumbu zetu sawa, huu ndo uchumi wa Magufuli aliouacha, all facts! - Sehemu ya kwanza

Ila mimi nimemuelewa Magufuli kwenye baadhi ya mambo baada ya kufariki.

Kuna vitu nimekua exposed kwake kwa hivi karibuni kwa siku za mwisho mwisho za uhai wake, ndio nikaja kujua alikua na nia gani.
Weka mambo bayana unafichaficha nini
 

Hiyo niliyowekea rangi siyo kweli. Mfumo wa EFD ulianzishwa mwishoni mwa kipindi cha pili cha Mzee Mwinyi! Ukaendelezwa na Mpaka na kuja kukamilishwa na JK.
 
Nyie unaosema hamna vyama, huwa hamuwezi kuanzisha uzi zenu mpaka msubiri wenye vyama waanzishe? Sasa hapo tatizo ni hao wenye vyama kuanzisha nyuzi zinazobeba vyama vyao, au nyie msio na vyama lakini hamuwawez kujianzishia uzi zenu?
Ni wanafiki flani anajiita wasio na vyema lakini ili ni wanachama kindakindaki
 
Naantombe Mushi
kwahiyo sasa ni kipi kifanyike ili mzunguko wa pesa uwe mkubwa kama enzi za kikwete?
Tuongeze wiz , na kuchota mapesa B.OT mradi wa 2b unawekewa bajeti ya 5b ilizipatikNa za kuJa kupiga laga na kununua real esta za bei ya kawaida kwa gharama kubwa maana kuna sehem ya kuzichotta kwa uraisi
 
Kwa hiyo hela haram mpaka igawiwe bure
Mtu akuiza heroine zake akaja akanunua mahekalu atakuwa na pesa halali bado
 
JPM ametwaliwa ili watanzania milioni 60 wapone imagine angeendelea kwa miaka mitano nchi ingekuwaje? Na wale wapuuzi wengine walitaka atawale miaka 20 zaidi Mungu akasema nitaliponya taifa langu Tanzania.
Umeandika kwa kutumia hisia badala ya akili.
 
Naantombe Mushi, leo hii nimebadili avatar na sababu ya kufanya hivyo ni kumtakia kila la kheri Rais Samia Suluhu Hassan kama atafanya kweli. Mimi nakataa na itachukua muda mwingi kuiamini na kuikubali CCM kwani ni wazi kuwa adui wa taifa hili si mwingine bali ni hilo zimwi CCM. Hujuma na madhambi yaliyofanywa na CCM kwa taifa letu hili ni makubwa na ni mengi.

Umenifanya niikumbuke Jamii Forums ya enzi hizo kabla haijavamiwa na viwavi vilivyomwagwa humu na CCM ili kulitetea hilo dude kwa maslahi binafsi. Jamii Forums imekuwa kama, kwa kutumia lugha ya Baba wa Taifa, kokoro linalozoa tu bila kujali ni takataka au upuuzi mwingine na ilikuwa ni swala la muda tu apatikane mtu kama dikteta uchwara tuliyekuwa naye.

Tumuombe Mungu ampe hekima na busara Rais Samia Suluhu Hassan, vitu viwili vilivyokosekana kabisa ndani ya utawala wa kidhalimu uliopita. Busara na hekima zinapokosa kwa kiongozi, matokeo ndio kama tulivyoshuhudia katika miaka hii minne ya mateso, utawala wa kiimla usiokuwa tayari kupokea ushauri zaidi ya utii kutoka kwa watu walio tayari kuweka rehani akili zao.

Nafuatilia kwa karibu michango yako na nakuomba uendeleze hapo ulipofikia...
 
Barikiwa Sana mkuu
 
Mama aangazie na huyu mdudu GPSA kwanin akae pale kushindana na wafanyabiashara binafsi tena wale hali ya chini, serikali ijitoe ili huyu mfanyabiashara apumue.
 
Kwa kutumia hizo taasisi Magu alikuwa sawa wakandarasi binafsi budgeti ziko juu sana wizi humohumo ili kukomesha hilo hiyo ndio ilikuwa dawa yake na kuokoa muda wa kutangaza matenda
 
Mwigulu naye aangazie sana kwenye mifumo ya ukusanyaji mapato, hasa huko chini kwenye halmashauri mapato mengi yanapotea kwa kuishia kwa wajanja wachache, japo sikuizi imeletwa control no. lkn bado haisaidii sana.
 
Asante kwa mchango wako mzuri, asante sana.

1) Naomba ungetu rahisishia kimaelezo hatua unazopendekeza serikali uchukue ili credit regime iwe restores?

2) Serikali imekuwa ikifanya manunuzi makubwa kwa Mfano, ununuzi wa ndege, jee serikali ilitakiwa ifanya nini?

3) Kumekuwa na shrinking of money supply kutoka 20% kwa mwaka na kushusha mpaka 10% kwa mwaka, jee una ushauri gani hapa?

4) jee ni kipi kimefanya mabenki yapunguze mikopo?

5) jee ungependekeza mifuko ya Mafao ya wafanyakazi iwekeze wapi ili kukuza uchumi?

6) una ushauri gani kwa miradi makubwa inayo endelea?

Naomba utusaidie kutuelimisha. Asante.
 
Yule mbunge alikua anasema aongezewe muda msalimieni
Wengi waliojipendekeza kwa kauli zao hizi nategemea wananchi hawatawarudisha tena bungeni,labda ufanyike upendeleo wa hali ya juu !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…