msabillah
JF-Expert Member
- Dec 5, 2011
- 4,764
- 3,192
Umlaani pekeyako sawa!Huu Uzi ni mzuri Sana kwakuwa uko kisayansi na tutamlaani magu milele ameharibu maisha yetu mtu yule. Alale alipojiandalia.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umlaani pekeyako sawa!Huu Uzi ni mzuri Sana kwakuwa uko kisayansi na tutamlaani magu milele ameharibu maisha yetu mtu yule. Alale alipojiandalia.
Weka mambo bayana unafichaficha niniIla mimi nimemuelewa Magufuli kwenye baadhi ya mambo baada ya kufariki.
Kuna vitu nimekua exposed kwake kwa hivi karibuni kwa siku za mwisho mwisho za uhai wake, ndio nikaja kujua alikua na nia gani.
Tuache uwongo...
1. Anasema kipindi cha JK kuna meli 60 zilitia nanga na kushusha mizugo pasipo kurekodiwa. Tafadhali tujuze TAREHE au mwezi.
2: Unasema kipindi cha JK viwanja vya ndege vilikuwa havina scana na kupelekea mizigo kuingia pasipo kukaguliwa.
Huu ni Uongo ata shetani anauogopa.
Niseme tu toka awamu ya Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Jk na jpm teknolojia imekua ikikua siku baada ya siku na imerahisisha mambo mengi.
Mfano, Kipindi cha JK ndio ulianzishwa mfumo wa EFD katika ukusanyaji Kodi, na ilichukua miaka kadhaa kutoa mafunzo na kuusimika mfumo huu nchi nzima. Kipindi cha JPM
Mfumo huu ndio ulikuwa umekwishaenea na ulimrahisishia sana awamu ya 5 kukusanya kodi.
Ni wanafiki flani anajiita wasio na vyema lakini ili ni wanachama kindakindakiNyie unaosema hamna vyama, huwa hamuwezi kuanzisha uzi zenu mpaka msubiri wenye vyama waanzishe? Sasa hapo tatizo ni hao wenye vyama kuanzisha nyuzi zinazobeba vyama vyao, au nyie msio na vyama lakini hamuwawez kujianzishia uzi zenu?
Tuongeze wiz , na kuchota mapesa B.OT mradi wa 2b unawekewa bajeti ya 5b ilizipatikNa za kuJa kupiga laga na kununua real esta za bei ya kawaida kwa gharama kubwa maana kuna sehem ya kuzichotta kwa uraisiNaantombe Mushi
kwahiyo sasa ni kipi kifanyike ili mzunguko wa pesa uwe mkubwa kama enzi za kikwete?
Kwa hiyo hela haram mpaka igawiwe bureFungua macho utazame,
1. Unasema enzi ya JK pesa ilikuwa ni haramu, naomba ufafanue kivipi? wakati watu walikuwa wanafanya kazi na kupata pesa, kwani kipindi cha JK pesa zilikuwa zinagawiwa bure? Kwanini useme eti zilikuwa za haramu?
2. Yaani wewe uchumi kudorora, mzunguko wa pesa haupo ndo unasema huo kwako ndo uchumi halisi? Kuwa serious mkuu.. fungua macho utazame tena kauli yako.
Umeandika kwa kutumia hisia badala ya akili.JPM ametwaliwa ili watanzania milioni 60 wapone imagine angeendelea kwa miaka mitano nchi ingekuwaje? Na wale wapuuzi wengine walitaka atawale miaka 20 zaidi Mungu akasema nitaliponya taifa langu Tanzania.
Nani kakutaja hapaUmlaani pekeyako sawa!
Naantombe Mushi, leo hii nimebadili avatar na sababu ya kufanya hivyo ni kumtakia kila la kheri Rais Samia Suluhu Hassan kama atafanya kweli. Mimi nakataa na itachukua muda mwingi kuiamini na kuikubali CCM kwani ni wazi kuwa adui wa taifa hili si mwingine bali ni hilo zimwi CCM. Hujuma na madhambi yaliyofanywa na CCM kwa taifa letu hili ni makubwa na ni mengi.Habarini wakuu…
Wakati bado tukiwa kwenye maombolezo, nimeona ni vema nifanye utafiti kidogo wa kumulika uchumi wa Hayati Magufuli, ili tuweke record zetu sawa, maana huku mtaani na kwenye vyombo vya habari kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana.
Japo mimi sijawahi kuwa mshabiki wa Hayati Magufuli, ila leo ntajaribu kuwa objective sana, kwa faida ya watu wa pande zote mbili, wale wanaoponda na wala wanaosifia. Nataka tufike kwenye mizania ya kujua ukweli wa Magufuli, ili kama mtu unasifia ujue unasifia kitu gani na kama unaponda ujue unaponda kitu gani.
Leo ntagusia viashiria vichache ambavyo vinanguvu katika uchumi wa nchi yeyote. Na viashiria hivo vina uhusiano wa viwakilishi kwenye kanuni ya kutafuta zao la nchi yaani GDP.
(GDP = Consumption + Investment + Government Spending + Net export)
Viashiria ambavyo ntaviangalia ni hivi vifuatavyo
1) Credit growth (Ukuaji wa mikopo inayotolewa na benki za kibiashara) – Hiki kiashiria kinawakilisha performance ya sekta binafsi kwenye uwekezaji, ukuaji wa mzunguko wa pesa, private sector confidence, performance ya mabenki ya kibiashara, na pia ni kiashiria cha consumption. Unapokuwa na declining trend, kwenye credit growth maana yake hayo mambo yote niliyoyataja lazima yawe negatively affected.
Ni nini kina determine credit growth? (Ama ni nini kisababishi cha ukuaji wa mikopo kwenye mabenki ya kibiashara kwa sekta binafsi?) – Nadhani hichi ni kitendawili ambacho Hayati Magufuli na wanaomzunguka wameshindwa kukijibu kwa miaka karibu sita aliyokuwa madarakani.
Asilimia karibu 65% mpaka 75% ya uchumi wa Tanzania upo determined na sekta binafsi, na hiyo inayobaki 25% mpaka 35% ndo sekta ambayo ni government nikimaanisha ile sekta inayohusu ukusanyaji wa mapato na bejeti ya nchi.
Utawala wa Magufuli, ulikuja na uwekezaji na matumizi makubwa kwenye projects kama Kununua Ndege, Ujenzi wa flyovers, Ujenzi wa Madaraja, Ujenzi wa Makao Makuu Dodoma, Ujezi wa Bwawa la Umeme, Ujenzi wa SGR na vinginevyo. Kwa ufupi naweza kukadiria kwamba, kwa miaka 6 iliyopita kuna Trillioni 40 mpaka 60 ambazo zilienda kwenye hizi projects za utawala Magufuli. Binafsi sina tatizo na hii approach ya Magufuli kwenye miundo mbinu, kwanza ntazidi kumsifu kwenye hili suala.
Tatizo kubwa ambalo nililiona na ambalo ndo kitendawili alichoshindwa kukijibu Magufuli na utawala wake ni kwamba, mipango ya kutekeleza hii miradi haikuangalia uwezo halisi wa nchi wa kutengeneza mapato ya ku finance hii miradi ambayo ilihitaj kiasi kikubwa cha pesa na rasilimali za viwandani.
Matokeo yake, serikali ya Magufuli ikajikuta ipo kwenye stress kubwa ya kupata pesa za ku finance hii miradi ya mapesa mengi. Kwa hiyo option zilikuwa ni mbili 1) Aaache kutekeleza hii miradi ya mepesa mengi au 2) Afanye kila njia kupata pesa.
Haiba ya Magufuli ilimfanya atumie njia namba mbili ‘Kutafuta pesa kwa gharama yeyote’. Nadhani hii njia ndo imefanya mpaka leo tuna vilio kwa wafanyabiashara, wawekezaji, wafanyakazi, mabenki, kwa sababu hii njia ilikuja na action zifuatazo za kutafuta pesa.
a) Kikosi kazi cha kukusanya kodi – Fairness kwenye mfumo wa kodi ilipotea, hakukua na logic tena, naweza sema kwa miaka sita iliyopita nchi ilikuwa kwenye ‘Unyang’anyi wa kodi’ na sio ‘Ukusanyaji wa kodi’. Madam President ameongea vema sana jana kuhusu hichi kitu. Hichi ndio kikubwa ambacho kimeua confidence ya sekta binafsi, matokeo yake ikaathiri mzunguko wa pesa kwenye uchumi, kwasababu kumbuka sekta binafsi ndio haswa wateja wa mabenki ya kibiashara. Kwa kuthibitisha hilo angalia trend ya utoaji mikopo kuanzia mwaka 2010 enzi ya kikwete mpaka 2020. Enzi ya Kikwete sekta binafsi ilikuwa inakuwa kwa kasi sana n ahata unaweza kuona trend ya utoaji wa mikopo ambayo ilikuwa ni kwa wastani wa asilimia Zaidi ya 13% wakati ukuaji wa mikopo kwenye utawala wa Magufuli ni wastani wa asilimia 5.6% kwa miaka mitano iliyopita. So unaweza kuona ni kwa namna gani sera ya Magufuli kwenye kodi ilivoua sekta binafsi na ukuaji wa mikopo.
View attachment 1741641
View attachment 1741642
Kwa kuangalia data za ongezeko la ukusanyaji wa mapato kwa miaka 10 iliyopita pamoja na ongezeko la utoaji mikopo kwa sekta binafsi kama zilivo hapo juu, tunaweza kuwa na conclusion zifuatazo kuhusu uchumi wa Magufuli dhidi ya watangulizi wake.
- Kwa miaka mitano ya mwisho ya utawala wa Kikwete, kwa ujumla aliweza kuongeza kodi kwa karibu asilimia 88% kwa kuangalia kodi iliyokusanywa 2011 na ile iliyokusanywa 2015, wakati huo huo, sekta binafsi ilikuwa ikifanya vizuri kwa kuangalia uwiano wa mikopo na zao ghafi la ndani, ilikuwa ikipanda kutoka 12.21% mwaka 2011 mpaka 14.47% mwaka 2015 alipotoka madarakani. (Key note: Utawala wa Kikwete uliweza kuongeza makusanyo ya kodi mwaka hadi mwaka, na wakati huo huo sekta binafsi ilikuwa inamea mwaka hadi mwaka – Economically hii ndio tunaiita positive
- Kwa miaka mine ya Magufuli 2016 – 2019 (sikuweza kupata data za 2020), kwa ujumla aliweza kuongeza makusanyo ya kodi kwa asilimia 56% ndani ya miaka minne 2016 -2019, wakati huo huo mikopo kwa sekta binafsi ilianza kudorora kwa kuangalia uwiano wa mikopo na GDP ambao kwa miaka hiyo minne imekuwa ikienda chini kutoka ile peak iliyofikiwa na utawala wa kikwete ya 14.47% mwaka 2015 mpaka 12.05% mwaka 2019. Hii ki uchumi tunaiita growth ambayo ni negative, yaani GDP inakuwa lakini sekta ya mikopo inadorora, na unaweza kuona ni kipindi hichi hichi nchi ilikuwa na sera za kodi za unyang’anyi.
b) Kutokuongeza mishahara ya watumishi wa umma – ilikuwa pia ni lazima utawala wa Magufuli ufanye hichi kitu ambacho is unfair, kwa minajili ya kulinda pesa za kufanya miradi. Kwa miaka sita iliyopita, kipato cha mfanyakazi kimeporomoka karibu kwa asilimia 18% kutokana na kupanda kwa gharama za maisha na serikali kushindwa kuongeza mishahara.
c) Kuzuia fao la kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii – ambacho wengi hawajui ni kwamba katika harakati za kutafuta pesa za miradi, utawala wa magufuli ndani ya miaka 6, wamekopa Zaidi ya Trillioni 12 kwenye hii mifuko ya hifadhi ya jamii, kitu ambacho kimepelekea hii mifuko kuwa ni kama imefilisika na ndio maana ikabidi wazuie fao la kujitoa kwasababu mifuko imekaushwa na serikali.
d) Kukua kwa haraka kwa deni la serikali (madeni ya nje na ndani) – Hii ndo ilikuwa karata ya mwisho ya kupata pesa, kwa sababu njia zote tatu hapo juu ni kama hazikuzaa matunda. (Ntaelezea kwa mapana hichi kitu nyuzi zinazofuata)
Hayo ni baadhi ya mambo yaliyotokea kama sera za uchumi wa Magufuli ambao ntaendelea kuuchambua, ila kwanza nataka mnielewe taratibu ili tuweze kwenda sawa.
Kwa wale ambao wana mashaka na uchambuzi wangu kuhusu masuala ya kiuchumi naomba mpitie baadhi ya nyuzi zangu ambazo niliwahi kuandika kipindi cha nyuma na ambazo zitahusika moja kwa moja na uchambuzi kuhusu uchumi wa Magufuli. Naahidi kuwaletea vipande vipande na hoja chache chache ili msije kuchanganyikiwa na rundo la taarifa.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------
1. Ukali wa maisha kwa watanzania - Serikali tafakarini kuongeza mishahara ya Watumishi wa Umma, ukali wa maisha ni bomu linaloua taratibu!
2. Kuadimika kwa saruji nchini - Serikali haiwezi kukwepa lawama ya kuadimika na kupanda kwa bei ya Saruji nchini. Waziri wa Viwanda ana kazi sana, kuna janga linatunyemelea
3. Uchumi bado upo kwenye mkwamo - ‘Namba zinanuka’ – kwanini nasema bado uchumi wetu upo kwenye mkwamo?
4. Serikali imedumaza mifuko ya hifadhi ya jamii - ‘Namba zinanuka’ – Serikali imechangia kudumaza mifuko ya Hifadhi ya Jamii
5. Uchumi wetu ni dhaifu - USHAHIDI: IMF hawajakosea, Uchumi wetu ni ‘DHAIFU’
Basi wewe tumia akili badala ya hisia . Hujakatazwa.Umeandika kwa kutumia hisia badala ya akili.
Barikiwa Sana mkuuNaantombe Mushi, leo hii nimebadili avatar na sababu ya kufanya hivyo ni kumtakia kila la kheri Rais Samia Suluhu Hassan kama atafanya kweli. Mimi nakataa na itachukua muda mwingi kuiamini na kuikubali CCM kwani ni wazi kuwa adui wa taifa hili si mwingine bali ni hilo zimwi CCM. Hujuma na madhambi yaliyofanywa na CCM kwa taifa letu hili ni makubwa na ni mengi.
Umenifanya niikumbuke Jamii Forums ya enzi hizo kabla haijavamiwa na viwavi vilivyomwagwa humu na CCM ili kulitetea hilo dude kwa maslahi binafsi. Jamii Forums imekuwa kama, kwa kutumia lugha ya Baba wa Taifa, kokoro linalozoa tu bila kujali ni takataka au upuuzi mwingine na ilikuwa ni swala la muda tu apatikane mtu kama dikteta uchwara tuliyekuwa naye.
Tumuombe Mungu ampe hekima na busara Rais Samia Suluhu Hassan, vitu viwili vilivyokosekana kabisa ndani ya utawala wa kidhalimu uliopita. Busara na hekima zinapokosa kwa kiongozi, matokeo ndio kama tulivyoshuhudia katika miaka hii minne ya mateso, utawala wa kiimla usiokuwa tayari kupokea ushauri zaidi ya utii kutoka kwa watu walio tayari kuweka rehani akili zao.
Nafuatilia kwa karibu michango yako na nakuomba uendeleze hapo ulipofikia...
Mama aangazie na huyu mdudu GPSA kwanin akae pale kushindana na wafanyabiashara binafsi tena wale hali ya chini, serikali ijitoe ili huyu mfanyabiashara apumue.Mama kaanza vizuri, sekta binafsi ilichokikosa kwa Magufuli ni confidence ambayo ilitokana na unyonywaji.. So confidence ikirejea, uwekezeja lazima utaimarika kwenye sekta binafsi, trust me, utaona mabadiliko ndugu yangu.
Wenye pesa hawahitaji bughudha, na Rais Samia ameshawahakikishia hilo, mambo yata improve, na mzunguko wa pesa utaanza kuongezeka, tuombe uzima baada ya miezi sita kutoka sasa... kutakuwa na improvement
Unajua ni kwanini riba ilishushwa? Riba haishushwi kama uchumi uko stable.Riba ya mikopo ni 14 %
Kwa kutumia hizo taasisi Magu alikuwa sawa wakandarasi binafsi budgeti ziko juu sana wizi humohumo ili kukomesha hilo hiyo ndio ilikuwa dawa yake na kuokoa muda wa kutangaza matendakwa maarifa yangu limited ya kiuchumi
1. Magufuli alitumia mfumo wa kuchukua pesa kwa watu ili afanikishe anayoyataka..
Pesa ilizunguka serikalini sababu hata wajenzi na makampuni mara nyingi alitumia TBA na Jkt.
Hapa utaona tu haikuwa muujiza tax base kusinyaa, mzunguko wa pesa kuwa mdogo, mfumuko wa bei kushuka, na ile miradi mikubwa kuanzishwa kwa pamoja huku uhusiano na nchi wahisani kutetereka, ni lazma Debt to GDP ratio ingepanda kwa speed kali na uchumi kukua negatively
2. Kikwete alikuwa anaachia pesa kwa wananchi.. Alikuwa anaongeza mishahara, miradi ilihusisha sekta binafsi kwa upana zaidi na kodi haikukusanywa kwa kiwango wala efforts kubwa. Hii tu ilitosha kusababisha uchumi kupaa zaidi na ule mfumo wake wa kutembeza bakuli ambao ulipunguza mzigo wa kodi kwa wananchi na kutekeleza miradi yake pasipo kuwaumiza...
There was no way deni liwe kubwa sana kuliko kipindi cha Magufuli au mabenki yasitoe mikopo zaidi ilhali purchasing power ya watu ipo juu mtaani
Asante kwa mchango wako mzuri, asante sana.Habarini wakuu…
Wakati bado tukiwa kwenye maombolezo, nimeona ni vema nifanye utafiti kidogo wa kumulika uchumi wa Hayati Magufuli, ili tuweke record zetu sawa, maana huku mtaani na kwenye vyombo vya habari kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana.
Japo mimi sijawahi kuwa mshabiki wa Hayati Magufuli, ila leo ntajaribu kuwa objective sana, kwa faida ya watu wa pande zote mbili, wale wanaoponda na wala wanaosifia. Nataka tufike kwenye mizania ya kujua ukweli wa Magufuli, ili kama mtu unasifia ujue unasifia kitu gani na kama unaponda ujue unaponda kitu gani.
Leo ntagusia viashiria vichache ambavyo vinanguvu katika uchumi wa nchi yeyote. Na viashiria hivo vina uhusiano wa viwakilishi kwenye kanuni ya kutafuta zao la nchi yaani GDP.
(GDP = Consumption + Investment + Government Spending + Net export)
Viashiria ambavyo ntaviangalia ni hivi vifuatavyo
1) Credit growth (Ukuaji wa mikopo inayotolewa na benki za kibiashara) – Hiki kiashiria kinawakilisha performance ya sekta binafsi kwenye uwekezaji, ukuaji wa mzunguko wa pesa, private sector confidence, performance ya mabenki ya kibiashara, na pia ni kiashiria cha consumption. Unapokuwa na declining trend, kwenye credit growth maana yake hayo mambo yote niliyoyataja lazima yawe negatively affected.
Ni nini kina determine credit growth? (Ama ni nini kisababishi cha ukuaji wa mikopo kwenye mabenki ya kibiashara kwa sekta binafsi?) – Nadhani hichi ni kitendawili ambacho Hayati Magufuli na wanaomzunguka wameshindwa kukijibu kwa miaka karibu sita aliyokuwa madarakani.
Asilimia karibu 65% mpaka 75% ya uchumi wa Tanzania upo determined na sekta binafsi, na hiyo inayobaki 25% mpaka 35% ndo sekta ambayo ni government nikimaanisha ile sekta inayohusu ukusanyaji wa mapato na bejeti ya nchi.
Utawala wa Magufuli, ulikuja na uwekezaji na matumizi makubwa kwenye projects kama Kununua Ndege, Ujenzi wa flyovers, Ujenzi wa Madaraja, Ujenzi wa Makao Makuu Dodoma, Ujezi wa Bwawa la Umeme, Ujenzi wa SGR na vinginevyo. Kwa ufupi naweza kukadiria kwamba, kwa miaka 6 iliyopita kuna Trillioni 40 mpaka 60 ambazo zilienda kwenye hizi projects za utawala Magufuli. Binafsi sina tatizo na hii approach ya Magufuli kwenye miundo mbinu, kwanza ntazidi kumsifu kwenye hili suala.
Tatizo kubwa ambalo nililiona na ambalo ndo kitendawili alichoshindwa kukijibu Magufuli na utawala wake ni kwamba, mipango ya kutekeleza hii miradi haikuangalia uwezo halisi wa nchi wa kutengeneza mapato ya ku finance hii miradi ambayo ilihitaj kiasi kikubwa cha pesa na rasilimali za viwandani.
Matokeo yake, serikali ya Magufuli ikajikuta ipo kwenye stress kubwa ya kupata pesa za ku finance hii miradi ya mapesa mengi. Kwa hiyo option zilikuwa ni mbili 1) Aaache kutekeleza hii miradi ya mepesa mengi au 2) Afanye kila njia kupata pesa.
Haiba ya Magufuli ilimfanya atumie njia namba mbili ‘Kutafuta pesa kwa gharama yeyote’. Nadhani hii njia ndo imefanya mpaka leo tuna vilio kwa wafanyabiashara, wawekezaji, wafanyakazi, mabenki, kwa sababu hii njia ilikuja na action zifuatazo za kutafuta pesa.
a) Kikosi kazi cha kukusanya kodi – Fairness kwenye mfumo wa kodi ilipotea, hakukua na logic tena, naweza sema kwa miaka sita iliyopita nchi ilikuwa kwenye ‘Unyang’anyi wa kodi’ na sio ‘Ukusanyaji wa kodi’. Madam President ameongea vema sana jana kuhusu hichi kitu. Hichi ndio kikubwa ambacho kimeua confidence ya sekta binafsi, matokeo yake ikaathiri mzunguko wa pesa kwenye uchumi, kwasababu kumbuka sekta binafsi ndio haswa wateja wa mabenki ya kibiashara. Kwa kuthibitisha hilo angalia trend ya utoaji mikopo kuanzia mwaka 2010 enzi ya kikwete mpaka 2020. Enzi ya Kikwete sekta binafsi ilikuwa inakuwa kwa kasi sana n ahata unaweza kuona trend ya utoaji wa mikopo ambayo ilikuwa ni kwa wastani wa asilimia Zaidi ya 13% wakati ukuaji wa mikopo kwenye utawala wa Magufuli ni wastani wa asilimia 5.6% kwa miaka mitano iliyopita. So unaweza kuona ni kwa namna gani sera ya Magufuli kwenye kodi ilivoua sekta binafsi na ukuaji wa mikopo.
View attachment 1741641
View attachment 1741642
Kwa kuangalia data za ongezeko la ukusanyaji wa mapato kwa miaka 10 iliyopita pamoja na ongezeko la utoaji mikopo kwa sekta binafsi kama zilivo hapo juu, tunaweza kuwa na conclusion zifuatazo kuhusu uchumi wa Magufuli dhidi ya watangulizi wake.
- Kwa miaka mitano ya mwisho ya utawala wa Kikwete, kwa ujumla aliweza kuongeza kodi kwa karibu asilimia 88% kwa kuangalia kodi iliyokusanywa 2011 na ile iliyokusanywa 2015, wakati huo huo, sekta binafsi ilikuwa ikifanya vizuri kwa kuangalia uwiano wa mikopo na zao ghafi la ndani, ilikuwa ikipanda kutoka 12.21% mwaka 2011 mpaka 14.47% mwaka 2015 alipotoka madarakani. (Key note: Utawala wa Kikwete uliweza kuongeza makusanyo ya kodi mwaka hadi mwaka, na wakati huo huo sekta binafsi ilikuwa inamea mwaka hadi mwaka – Economically hii ndio tunaiita positive
- Kwa miaka mine ya Magufuli 2016 – 2019 (sikuweza kupata data za 2020), kwa ujumla aliweza kuongeza makusanyo ya kodi kwa asilimia 56% ndani ya miaka minne 2016 -2019, wakati huo huo mikopo kwa sekta binafsi ilianza kudorora kwa kuangalia uwiano wa mikopo na GDP ambao kwa miaka hiyo minne imekuwa ikienda chini kutoka ile peak iliyofikiwa na utawala wa kikwete ya 14.47% mwaka 2015 mpaka 12.05% mwaka 2019. Hii ki uchumi tunaiita growth ambayo ni negative, yaani GDP inakuwa lakini sekta ya mikopo inadorora, na unaweza kuona ni kipindi hichi hichi nchi ilikuwa na sera za kodi za unyang’anyi.
b) Kutokuongeza mishahara ya watumishi wa umma – ilikuwa pia ni lazima utawala wa Magufuli ufanye hichi kitu ambacho is unfair, kwa minajili ya kulinda pesa za kufanya miradi. Kwa miaka sita iliyopita, kipato cha mfanyakazi kimeporomoka karibu kwa asilimia 18% kutokana na kupanda kwa gharama za maisha na serikali kushindwa kuongeza mishahara.
c) Kuzuia fao la kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii – ambacho wengi hawajui ni kwamba katika harakati za kutafuta pesa za miradi, utawala wa magufuli ndani ya miaka 6, wamekopa Zaidi ya Trillioni 12 kwenye hii mifuko ya hifadhi ya jamii, kitu ambacho kimepelekea hii mifuko kuwa ni kama imefilisika na ndio maana ikabidi wazuie fao la kujitoa kwasababu mifuko imekaushwa na serikali.
d) Kukua kwa haraka kwa deni la serikali (madeni ya nje na ndani) – Hii ndo ilikuwa karata ya mwisho ya kupata pesa, kwa sababu njia zote tatu hapo juu ni kama hazikuzaa matunda. (Ntaelezea kwa mapana hichi kitu nyuzi zinazofuata)
Hayo ni baadhi ya mambo yaliyotokea kama sera za uchumi wa Magufuli ambao ntaendelea kuuchambua, ila kwanza nataka mnielewe taratibu ili tuweze kwenda sawa.
Kwa wale ambao wana mashaka na uchambuzi wangu kuhusu masuala ya kiuchumi naomba mpitie baadhi ya nyuzi zangu ambazo niliwahi kuandika kipindi cha nyuma na ambazo zitahusika moja kwa moja na uchambuzi kuhusu uchumi wa Magufuli. Naahidi kuwaletea vipande vipande na hoja chache chache ili msije kuchanganyikiwa na rundo la taarifa.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------
1. Ukali wa maisha kwa watanzania - Serikali tafakarini kuongeza mishahara ya Watumishi wa Umma, ukali wa maisha ni bomu linaloua taratibu!
2. Kuadimika kwa saruji nchini - Serikali haiwezi kukwepa lawama ya kuadimika na kupanda kwa bei ya Saruji nchini. Waziri wa Viwanda ana kazi sana, kuna janga linatunyemelea
3. Uchumi bado upo kwenye mkwamo - ‘Namba zinanuka’ – kwanini nasema bado uchumi wetu upo kwenye mkwamo?
4. Serikali imedumaza mifuko ya hifadhi ya jamii - ‘Namba zinanuka’ – Serikali imechangia kudumaza mifuko ya Hifadhi ya Jamii
5. Uchumi wetu ni dhaifu - USHAHIDI: IMF hawajakosea, Uchumi wetu ni ‘DHAIFU’
Wengi waliojipendekeza kwa kauli zao hizi nategemea wananchi hawatawarudisha tena bungeni,labda ufanyike upendeleo wa hali ya juu !Yule mbunge alikua anasema aongezewe muda msalimieni