Tuweke kumbukumbu zetu sawa, huu ndo uchumi wa Magufuli aliouacha, all facts! - Sehemu ya kwanza

Mkuu usiziamini takwimu za Magu hata kidogo hazikuwa na uhalisia ndio maana alipiga marufuku kutoa takwimu.

Kiuhalisia inflation imepanda hii haitaji resaerch ya mbobezi
 
Hizi ndo tunaita hekaya /mtu unatafuta point between lines hupati ! kapumzike maana huelewi kinachojadiliwa hapa
 
Hata me sijamwelewe /huenda anaishi Msumbiji huyu
 
Mkuu usiziamini takwimu za Magu hata kidogo hazikuwa na uhalisia ndio maana alipiga marufuku kutoa takwimu.

Kiuhalisia inflation imepanda hii haitaji resaerch ya mbobezi
Hizo nilizotoa siyo takwimu za Magu! Wala sijui takwimu za Magu ziko wapi bali hizo ni za World Bank. Ngoja niweke hiyo chati tena kutoka World Bank

 
Hizi ndo tunaita hekaya /mtu unatafuta point between lines hupati ! kapumzike maana huelewi kinachojadiliwa hapa
Achana naye huyo kwani ni wazi hii mada inamzidi kimo. Ndio hawa hawa akili waliziweka rehani wakabakia kugonga meza. Kwao huyo dikteta uchwara alikuwa mungu mtu.
 
Upo sahihi kiongozi///kama Taifa tulikuwa kwenye economic messy asikwambie mtu kwakweli.Jamaa anasisitiza tuchape kazi tu tuache kulalamika huku katunyang'anya economic instruments dahhhhh ,anyway Mungu amweke pale anapostahili
Achana naye huyo kwani ni wazi hii mada inamzidi kimo. Ndio hawa hawa akili waliziweka rehani wakabakia kugonga meza. Kwao huyo dikteta uchwara alikuwa mungu mtu.
 
Nimesoma andiko lako, nitalisoma tena baadae leo. Umenifanya nitafakari mambo mengi zaidi. Thank you
 
Kwa wale ambao wana mashaka na uchambuzi wangu kuhusu masuala ya kiuchumi...
Mkuu, nilipoona tu I'd yako ya: "Naamtombe mushi" nikahisi kuna shida, bado kidogo nisisome uzi, ila baada ya kupitia, nimeona uchambuzi ni makini na weledi wa kiuchumi. Big up🤝
 
Siwezi kuuelewa huu uchambuzi unless uniambie kwa nini viwanda vingi abavyo ni vya binasfsi na serikali vilikufa awamu zilizopita na vilianza fufuka awamu ya JPM. Swali lingine kama hali ilikuwa mbaya ya kiuchumi kwa nini tuliingia uchumi wa kati?

Wana wa Israeli walipokuwa wanatoka Misri kwenda Kanani walipitia misukosuko ya kila aina njiani, ilifika mahali wakaanza kumlamu Musa wakisema ni heri warudi kule walipotoka. Kwangu mimi Magufuli ataendelea kuwa Rais bora kuwahi kumshuhudia katika maisha yangu, kwasababu ya ujasiri wake hasa kwenye kutujengea misingi ya nchi yenye uchumi endelevevu kwa siku zijazo.

Kupanga ni kuchagua na ili kufikia maendeleo ya kweli lazima kuna kizazi kijotoe sadaka kwa ajili ya wengine. Wakiloni walivamia Afrika miaka hiyo bila kujali wanyama wakali na magonjwa wakachukua dhahabu na almasi wakaenda jenga nchi zao, leo wajukuu zao wanakula matunda ya jasho la mababu zao.

Ni kweli JPM hakuongeza mishahara na alitoa fao la kujitoa, aliongeza makato kwa wanufaika wa bodi ya mkopo nk, lakini wanachi tulimuelewa nia ya yake, sababu matokeo yake tuliyaona kila tulipo safiri ndani ya nchi hii.

Miradi mikubwa mikubwa kama SGR Dar to Moro takriban 7trill, Nyerere george 6.9trill, Daraja la busis 6.9bill zahanati, vituo vya afya na hospitali za rufaa kila mkoa, masoko na basi stend kila mkoa, ujenzi wa meli ziwa Victoria, Nyasa na Tanganyika, vyote hivi vilihitaji pesa. Kwa akili ya kwaida ukifikiria miradi mingi, ukiacha reli ya SGR ilikuwa inakamilika kabla ya 2024 na ndio maana hayat Rais Magufuli aliwaasa wafanyakazi wawe wazalendo na kwamba angeongeza mshahara kabla hajamaliza muda wake.

Miradi hii mikubwa aliyoianzisha JPM ndio ingeongeza ukusanyaji wa kodi kwa siku za mbeleni na ndio ikafanya nchi iweze kujitegemea. Narudia tena kusema Rais Magufuli alikuwa ni kiongozi mwenye maono makubwa sana tulichewa kumpata, tulipompata hajadumu. katuachia dira ya maendeleo ya taifa ambayo tukiifuata taifa linakwenda kujitegemea kwa kipindi kifupi.

Siku zote unapotatua matatizo kwa watu wengine unaweza kusababisha matatizo kwa wengine, hatotokea kamwe kiongozi atayewarisha wote. R.I.P JPM.
 
Barikiwa sana chifu,hii taarifa imekaa vzr,nafikiri wale waafidhina wa utawala uliopita,watapata shule sasa.
 
Kitu pekee alichojaliea binadamu ni ubinafsi, ndio maana kukawepo na msemo wa mwenye kushiba hamjui mwenye njaa.

Hao ndugu walio kuwa wanataka kuondolewa kwa ukomo sio kwamba hawakua hawoni hali ilivyo la, bali wako kwenye shibe.

Kosa kubwa la yule mheshimiwa Ni kutokupokea ushauri kutoka sehemu husika au mtu sahihi, mtaalam wa afya atoe ushauri wa afya, mtaalam wa uchumi kadhalika, mtaalam wa elimu hivyo hivyo, mtaam was kijeshi Mambo ya jeshi.

Lakini kwake yeye sidhani Kama kitu Kama hiki kiliwezekanika ndio maana kwingi kuliharibika na karibu kila sehemu kwenye nchi nzima kuliharibika na kungekua na Hali mbaya ambayo historia isingesahau.
 
hii ndo hasa faida ya jf. unapata elimu kubwa na taarifa kubwa toka kwa watu makini nyanja tofauti. shukran mdau kushiriki uzalishaj wa kizaz cha kujibu hoja kwa hoja, mana ni kama kinapotea!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…