Naipendatz
JF-Expert Member
- Jul 27, 2011
- 5,096
- 8,234
FHH (Fk Him Harder)Huu Uzi ni mzuri Sana kwakuwa uko kisayansi na tutamlaani magu milele ameharibu maisha yetu mtu yule. Alale alipojiandalia.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
FHH (Fk Him Harder)Huu Uzi ni mzuri Sana kwakuwa uko kisayansi na tutamlaani magu milele ameharibu maisha yetu mtu yule. Alale alipojiandalia.
Mkuu usiziamini takwimu za Magu hata kidogo hazikuwa na uhalisia ndio maana alipiga marufuku kutoa takwimu.Hii hapa siyo kweli kwa sababu kutokuongeza kwa mishahara kulisababisha inflation Tanzania ibaki kuwa ya chini sana. Aliingia madarakani kukiwa na 5.59% na wakati anaondoka inflation ilikuwa 3.56% Kwa hiyo madai ya gharama za maisha kupanda siyo ya kweli. Tatizo lililokuwepo na mzunguko hafifu wa fedha kutokana kna kudhibiti matumizi ya pesa za serikali. Uchumi wa Tanzania umekuwa unategemea sana pesa za serikali kuliko pesa za watu binafsi; serikali ikibana matumizi ya pesa zake basi watu wanalia hawana hela. Ilikuwa hivyo enzi za Mkapa mwanzoni, na enzi za magufuli. Serikali ikishaanza kulegeza usimamaizi wa matumiz yake basi ndipo unaona pesa zinakuw nyingi mitaani na inflation inaongezeka.
View attachment 1741777
Yule mbunge alikua anasema aongezewe muda msalimieni
Binafsi naona hizi ndiyo zile tunasema uchumi wa kwenye makaratasi ila kipindi cha JK tuseme tu ukweli fedha nyingi zilikuwa ni haram na hazikuwa zinaingia kwenye mzunguko ili lilipelekea mtaani hela kuzagaa kiasi ata laki ikaitwa si pesa ola sasa laki tunajua ni pesa.
Wafanyabiashara sikuzote wazo lao la kwanza kukwepa kodi, kipindi cha JK kuna meli 60 ziliwai kutia nanga pale bandarini Dar es Salaam na meli hizo zote hazikuwa recorded mahala popote na mwisho kontena zikapotea kusiko julikana, Zaman kipindi cha JK kontena kupotea huko bandarini kilikuwa kitu cha kawaida, Bandarini hapakuwa na scana ata ya kuscan vitu vinavyopita bandarini.
Nenda pale airport kipindi cha JK hakuna kikicho scsniwa ili kijulikane ni kitu gani...
Mwisho wa siku Magufuli alitamani kujenga Tanzania ya kesho, Magufuli hakuwa mwanasiasa ila alikuwa kiongozi, aliona bora aanze upya kuliko kuendelea na staili waliyotumia watangulizi wake.
Mwisho niseme tu huu wa kipindi cha Hayati ndo ulikuwa uchumi wetu halisi, huko nyuma kulikuwa na wajanja tu wenye kuchuma walivyotaka kuchuma lakini kwenye kujenga nchi hamna kitu.
Nakumbuka kipindi cha JK NGO zilopeta kweli lakini ki ukweli kabisa walikuwa hawalipi ata Tsh 150,000/= kwa mwaka wala hawapeleki ata hesabu zao za mwaka kwa msajili lakini alivyoingia Magufuli aligakikisha kila Wizara inayoona kuna sehemu inatakiwa ikusanye fedha inatakiwa kufanya hivo, hapo ukaanza utaratibu kama hupeleki hesabu zako kwa na hulipi ada shirika lako litafungwa na mengi yalifungwa maana yalikuwa hewa na hewa kweli cos ata mimi mwenyewe nishawah fanya kazi huko najua vyema na mpaka sasa mwenye NGO yake ninahakika anafanya kazi kwa unyofu mno.
Kiuweli tulichekea na tulipata mtu ambae alikuwa anatuambia ukweli, hizi habari za kulembeana na kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa hakuwa nazo.View attachment 1741699
Fungua macho utazame,
1. Unasema enzi ya JK pesa ilikuwa ni haramu, naomba ufafanue kivipi? wakati watu walikuwa wanafanya kazi na kupata pesa, kwani kipindi cha JK pesa zilikuwa zinagawiwa bure? Kwanini useme eti zilikuwa za haramu?
2. Yaani wewe uchumi kudorora, mzunguko wa pesa haupo ndo unasema huo kwako ndo uchumi halisi? Kuwa serious mkuu.. fungua macho utazame tena kauli yako.
Hizo nilizotoa siyo takwimu za Magu! Wala sijui takwimu za Magu ziko wapi bali hizo ni za World Bank. Ngoja niweke hiyo chati tena kutoka World BankMkuu usiziamini takwimu za Magu hata kidogo hazikuwa na uhalisia ndio maana alipiga marufuku kutoa takwimu.
Kiuhalisia inflation imepanda hii haitaji resaerch ya mbobezi
Achana naye huyo kwani ni wazi hii mada inamzidi kimo. Ndio hawa hawa akili waliziweka rehani wakabakia kugonga meza. Kwao huyo dikteta uchwara alikuwa mungu mtu.Hizi ndo tunaita hekaya /mtu unatafuta point between lines hupati ! kapumzike maana huelewi kinachojadiliwa hapa
Achana naye huyo kwani ni wazi hii mada inamzidi kimo. Ndio hawa hawa akili waliziweka rehani wakabakia kugonga meza. Kwao huyo dikteta uchwara alikuwa mungu mtu.
Mkuu, nilipoona tu I'd yako ya: "Naamtombe mushi" nikahisi kuna shida, bado kidogo nisisome uzi, ila baada ya kupitia, nimeona uchambuzi ni makini na weledi wa kiuchumi. Big up🤝Kwa wale ambao wana mashaka na uchambuzi wangu kuhusu masuala ya kiuchumi...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Shujaa wa Africa?
Kamoooooon!!!
[emoji23][emoji23][emoji23] we Jamaa unazani nipo siliasi na nilichoandika soma tena na tena.alikuwa shujaa wa familia yako labda. usitujumuishe watz wote.
[emoji2958][emoji2958][emoji2958]Yaani ninacheka utafikiri mazuri
Kitu pekee alichojaliea binadamu ni ubinafsi, ndio maana kukawepo na msemo wa mwenye kushiba hamjui mwenye njaa.Mbaya zaidi, ni yeye kujifanya anajua kila kitu... aiseee watanzania itabidi tuwe makini sana huko mbeleni.... hii nchi ilikuwa ishafika point inaenda kuparanganyika.. ni kama miujiza imetendeka... halafu wale wapuuzi wanaongea mambo ya kufuta ukomo wa uraisi.. aiseeee
Kha!kha!kha!,Usimlaani Bali mwombee alale mahali pema peponi.Huu Uzi ni mzuri Sana kwakuwa uko kisayansi na tutamlaani magu milele ameharibu maisha yetu mtu yule. Alale alipojiandalia.
hii ndo hasa faida ya jf. unapata elimu kubwa na taarifa kubwa toka kwa watu makini nyanja tofauti. shukran mdau kushiriki uzalishaj wa kizaz cha kujibu hoja kwa hoja, mana ni kama kinapotea!Habarini wakuu…
Wakati bado tukiwa kwenye maombolezo, nimeona ni vema nifanye utafiti kidogo wa kumulika uchumi wa Hayati Magufuli, ili tuweke record zetu sawa, maana huku mtaani na kwenye vyombo vya habari kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana.
Japo mimi sijawahi kuwa mshabiki wa Hayati Magufuli, ila leo ntajaribu kuwa objective sana, kwa faida ya watu wa pande zote mbili, wale wanaoponda na wala wanaosifia. Nataka tufike kwenye mizania ya kujua ukweli wa Magufuli, ili kama mtu unasifia ujue unasifia kitu gani na kama unaponda ujue unaponda kitu gani.
Leo ntagusia viashiria vichache ambavyo vinanguvu katika uchumi wa nchi yeyote. Na viashiria hivo vina uhusiano wa viwakilishi kwenye kanuni ya kutafuta zao la nchi yaani GDP.
(GDP = Consumption + Investment + Government Spending + Net export)
Viashiria ambavyo ntaviangalia ni hivi vifuatavyo
1) Credit growth (Ukuaji wa mikopo inayotolewa na benki za kibiashara) – Hiki kiashiria kinawakilisha performance ya sekta binafsi kwenye uwekezaji, ukuaji wa mzunguko wa pesa, private sector confidence, performance ya mabenki ya kibiashara, na pia ni kiashiria cha consumption. Unapokuwa na declining trend, kwenye credit growth maana yake hayo mambo yote niliyoyataja lazima yawe negatively affected.
Ni nini kina determine credit growth? (Ama ni nini kisababishi cha ukuaji wa mikopo kwenye mabenki ya kibiashara kwa sekta binafsi?) – Nadhani hichi ni kitendawili ambacho Hayati Magufuli na wanaomzunguka wameshindwa kukijibu kwa miaka karibu sita aliyokuwa madarakani.
Asilimia karibu 65% mpaka 75% ya uchumi wa Tanzania upo determined na sekta binafsi, na hiyo inayobaki 25% mpaka 35% ndo sekta ambayo ni government nikimaanisha ile sekta inayohusu ukusanyaji wa mapato na bejeti ya nchi.
Utawala wa Magufuli, ulikuja na uwekezaji na matumizi makubwa kwenye projects kama Kununua Ndege, Ujenzi wa flyovers, Ujenzi wa Madaraja, Ujenzi wa Makao Makuu Dodoma, Ujezi wa Bwawa la Umeme, Ujenzi wa SGR na vinginevyo. Kwa ufupi naweza kukadiria kwamba, kwa miaka 6 iliyopita kuna Trillioni 40 mpaka 60 ambazo zilienda kwenye hizi projects za utawala Magufuli. Binafsi sina tatizo na hii approach ya Magufuli kwenye miundo mbinu, kwanza ntazidi kumsifu kwenye hili suala.
Tatizo kubwa ambalo nililiona na ambalo ndo kitendawili alichoshindwa kukijibu Magufuli na utawala wake ni kwamba, mipango ya kutekeleza hii miradi haikuangalia uwezo halisi wa nchi wa kutengeneza mapato ya ku finance hii miradi ambayo ilihitaj kiasi kikubwa cha pesa na rasilimali za viwandani.
Matokeo yake, serikali ya Magufuli ikajikuta ipo kwenye stress kubwa ya kupata pesa za ku finance hii miradi ya mapesa mengi. Kwa hiyo option zilikuwa ni mbili 1) Aaache kutekeleza hii miradi ya mepesa mengi au 2) Afanye kila njia kupata pesa.
Haiba ya Magufuli ilimfanya atumie njia namba mbili ‘Kutafuta pesa kwa gharama yeyote’. Nadhani hii njia ndo imefanya mpaka leo tuna vilio kwa wafanyabiashara, wawekezaji, wafanyakazi, mabenki, kwa sababu hii njia ilikuja na action zifuatazo za kutafuta pesa.
a) Kikosi kazi cha kukusanya kodi – Fairness kwenye mfumo wa kodi ilipotea, hakukua na logic tena, naweza sema kwa miaka sita iliyopita nchi ilikuwa kwenye ‘Unyang’anyi wa kodi’ na sio ‘Ukusanyaji wa kodi’. Madam President ameongea vema sana jana kuhusu hichi kitu. Hichi ndio kikubwa ambacho kimeua confidence ya sekta binafsi, matokeo yake ikaathiri mzunguko wa pesa kwenye uchumi, kwasababu kumbuka sekta binafsi ndio haswa wateja wa mabenki ya kibiashara. Kwa kuthibitisha hilo angalia trend ya utoaji mikopo kuanzia mwaka 2010 enzi ya kikwete mpaka 2020. Enzi ya Kikwete sekta binafsi ilikuwa inakuwa kwa kasi sana n ahata unaweza kuona trend ya utoaji wa mikopo ambayo ilikuwa ni kwa wastani wa asilimia Zaidi ya 13% wakati ukuaji wa mikopo kwenye utawala wa Magufuli ni wastani wa asilimia 5.6% kwa miaka mitano iliyopita. So unaweza kuona ni kwa namna gani sera ya Magufuli kwenye kodi ilivoua sekta binafsi na ukuaji wa mikopo.
View attachment 1741641
View attachment 1741642
Kwa kuangalia data za ongezeko la ukusanyaji wa mapato kwa miaka 10 iliyopita pamoja na ongezeko la utoaji mikopo kwa sekta binafsi kama zilivo hapo juu, tunaweza kuwa na conclusion zifuatazo kuhusu uchumi wa Magufuli dhidi ya watangulizi wake.
- Kwa miaka mitano ya mwisho ya utawala wa Kikwete, kwa ujumla aliweza kuongeza kodi kwa karibu asilimia 88% kwa kuangalia kodi iliyokusanywa 2011 na ile iliyokusanywa 2015, wakati huo huo, sekta binafsi ilikuwa ikifanya vizuri kwa kuangalia uwiano wa mikopo na zao ghafi la ndani, ilikuwa ikipanda kutoka 12.21% mwaka 2011 mpaka 14.47% mwaka 2015 alipotoka madarakani. (Key note: Utawala wa Kikwete uliweza kuongeza makusanyo ya kodi mwaka hadi mwaka, na wakati huo huo sekta binafsi ilikuwa inamea mwaka hadi mwaka – Economically hii ndio tunaiita positive
- Kwa miaka mine ya Magufuli 2016 – 2019 (sikuweza kupata data za 2020), kwa ujumla aliweza kuongeza makusanyo ya kodi kwa asilimia 56% ndani ya miaka minne 2016 -2019, wakati huo huo mikopo kwa sekta binafsi ilianza kudorora kwa kuangalia uwiano wa mikopo na GDP ambao kwa miaka hiyo minne imekuwa ikienda chini kutoka ile peak iliyofikiwa na utawala wa kikwete ya 14.47% mwaka 2015 mpaka 12.05% mwaka 2019. Hii ki uchumi tunaiita growth ambayo ni negative, yaani GDP inakuwa lakini sekta ya mikopo inadorora, na unaweza kuona ni kipindi hichi hichi nchi ilikuwa na sera za kodi za unyang’anyi.
b) Kutokuongeza mishahara ya watumishi wa umma – ilikuwa pia ni lazima utawala wa Magufuli ufanye hichi kitu ambacho is unfair, kwa minajili ya kulinda pesa za kufanya miradi. Kwa miaka sita iliyopita, kipato cha mfanyakazi kimeporomoka karibu kwa asilimia 18% kutokana na kupanda kwa gharama za maisha na serikali kushindwa kuongeza mishahara.
c) Kuzuia fao la kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii – ambacho wengi hawajui ni kwamba katika harakati za kutafuta pesa za miradi, utawala wa magufuli ndani ya miaka 6, wamekopa Zaidi ya Trillioni 12 kwenye hii mifuko ya hifadhi ya jamii, kitu ambacho kimepelekea hii mifuko kuwa ni kama imefilisika na ndio maana ikabidi wazuie fao la kujitoa kwasababu mifuko imekaushwa na serikali.
d) Kukua kwa haraka kwa deni la serikali (madeni ya nje na ndani) – Hii ndo ilikuwa karata ya mwisho ya kupata pesa, kwa sababu njia zote tatu hapo juu ni kama hazikuzaa matunda. (Ntaelezea kwa mapana hichi kitu nyuzi zinazofuata)
Hayo ni baadhi ya mambo yaliyotokea kama sera za uchumi wa Magufuli ambao ntaendelea kuuchambua, ila kwanza nataka mnielewe taratibu ili tuweze kwenda sawa.
Kwa wale ambao wana mashaka na uchambuzi wangu kuhusu masuala ya kiuchumi naomba mpitie baadhi ya nyuzi zangu ambazo niliwahi kuandika kipindi cha nyuma na ambazo zitahusika moja kwa moja na uchambuzi kuhusu uchumi wa Magufuli. Naahidi kuwaletea vipande vipande na hoja chache chache ili msije kuchanganyikiwa na rundo la taarifa.
-----------------------------------------------------------------------------------------------------
1. Ukali wa maisha kwa watanzania - Serikali tafakarini kuongeza mishahara ya Watumishi wa Umma, ukali wa maisha ni bomu linaloua taratibu!
2. Kuadimika kwa saruji nchini - Serikali haiwezi kukwepa lawama ya kuadimika na kupanda kwa bei ya Saruji nchini. Waziri wa Viwanda ana kazi sana, kuna janga linatunyemelea
3. Uchumi bado upo kwenye mkwamo - ‘Namba zinanuka’ – kwanini nasema bado uchumi wetu upo kwenye mkwamo?
4. Serikali imedumaza mifuko ya hifadhi ya jamii - ‘Namba zinanuka’ – Serikali imechangia kudumaza mifuko ya Hifadhi ya Jamii
5. Uchumi wetu ni dhaifu - USHAHIDI: IMF hawajakosea, Uchumi wetu ni ‘DHAIFU’