Tuweke kumbukumbu zetu sawa, huu ndo uchumi wa Magufuli aliouacha, all facts! - Sehemu ya kwanza

Mkuu ungemwacha tu..darasa lolote lile lazma wawepo bongolala...we endelea kumwaga nondo
 
.........Mushi,
Naogopa kutaja jina lako la kwanza maana lina-sound kama.......kwa jamii ya Waswahili.
Anyway mimi nakupa kudo's kwa uchambuzi wako makini. Anayepingana na wewe ktk hoja zako hizi Kiuchumi atakuwa ni zwazwa,chizi, mpuuzi na shabiki kindakindaki wa marehemu Jiwe.

Ni dhahiri Jiwe ame- cripple our economy to the very lowest stage!! Jiwe alikuwa ana tamba kuwa "nchi hii ni tajiri sana" ilihali AKIKWAPUA FEDHA YA WAZEE KWENE MIFUKO YA JAMII KIADI CHA KUTISHIA MIFUKO HIYO KUFILISIKA...!! Fikiria wazee wengi waliostaafu kipindi hiki cha marehemu kuna wengi wamekufa bila ya kupata stahiki zao za mafao....! Kuna wazee leo wana mwaka 1-3 au zaidi HAWAJALIPWA!!!???.

Lakini Wababaiishaji na Wapiga debe wa Jiwe waliendelea kumsifu, kumpigia magoti,kumlamba miguu na hata kumwabudu kama vile kimungu fulani hivi! Miradi yote ambayo marehemu Magufuli ameifanya kwa lulazimisha HUKU AKIENDELEA KUWADHULUMU WATZ WALIO WATUMISHI KWA KUWANYIMA STAHIKI ZA MAFAO YAO, NYONGEZA YA MISHAHARA, AJIRA KWA WATZ WALIOKUWA WANA FUZU VYUONI n.k.

Lakni pia upande wa Wafanyibiashara ilikuwa mbaya kuliko maelezo. Biashara nyingi zimefungwa. Tembea mijini utashangaa kuona milango/fremu za maduka zikiwa closed au zina MAGUFULI 2/2( Kufuli la TRA na la MFANYABISHARA)! Kisa? Mfanya biashara ANADAIWA KODI YA MILIONS IF NOT BILLIONS...!!!

Mimi kwa upande wa Miundombinu siwezi kumpongeza Marehemu Jiwe! Huwezi kujenga miundombinu on the expense of Watanzania kwa KUWAUMIZA!! Bado kuna miradi haikuwa na ulazima wowote; mfano IKULU YA CHATO, INTERNATIONAL AIRPORT CHATO NA CHATO NATIONAL PARK....!!!
Kwa Serikali yoyote makini LAZIMA IWE NA VIPA UMBELE KULINGANA NA HALI YA KIUCHUMI! Kwamba kipi kianze kwa umuhimu wake!! Jiwe alikuwa ana kurupuka tu kwa kulazimisha kwenda na MIRADI YOOTE KWA PAMOJA BILA KUJALI PESA IKO WAPI!!! Matokro yake ikawa hii tabia ya UPORAJI WA MALI ZA WAFANYIBIASHARA, WAJASIRIAMALI, WAWEKEZAJI na WATU BINAFSI!!!

Nihitimishe kwa kusema kwamba Marehemu Jiwe ameiacha Tanzania ikiwa taabani kiuchumi. Tunaweza kuona Mifly overs, SGR, BWAWA LA MAGUFULI na Mibombadier lakini WATANZANIA WAKO HOI BIN TAABAN KIUCHUMI!!!. Walokuwa wanasema Jiwe ni Rais wa VITU na siyo WATU they're correct by 100 %!
Kama Mhe. Rais Bi Samia Siluhu Hassan aliye vaa viatu vya Jiwe/Mwamba ataamua kufuata nyayo za JIWE basi Uchumi wa nji hii utaendelea kuumia na kuzidi kuwa kilema. Tusije tukashangaa siku moja TANZANIA INATANGAZWA KURUDI KWENYE NCHI MASKINI kama ilivokuwa...!!

Tusubiri.
 

Sasa usilaumu wanaoweka thread usizopenda wakati wasipoweka hizo, ww/nyinyi mlio neutral hamtaweka kabisa. Hayo mengine kwenye post yako nimeshindwa kuyaelewa.
 
Mwandiko wako tu unakutanabaisha ulivyo mweupe kichwani pure mataga
 
Idiot.
 
Kha!kha!kha!,Usimlaani Bali mwombee alale mahali pema peponi.
Yeye alimwombea beni Saanane? Risasi 16 za lisu mbona alikataza uchunguzi huru ? Azory gwanda unadhani mkewe na watoto wako kwenye trauma kiasi gani kupotea kwa baba Yao mpaka Leo siwezi kumuombea muuwaji alieuwa watu jambazi la chato Lile Mungu ka mmute milele.
 
ilikuwa inaenda kutokea nose crash..huu ndio ukweli lilikuwa suala la muda tu...

Huwezi kujenga nchi kwa kuwatumia wanyonge ambao ni idadi kubwa ya population, Mzee aliamini mzunguko wa hawa wanyonge unaweza kufanya kila anachowaza kufanya... baada ya kuchukua hela zote za wanyonge kwenda kwenye miradi akajikuta miradi haijafika hata nusu ya ujenzi na wanyonge wameishiwa tayari na yeye anataka kusimamisha legacy yake hapo ndio tukaanza kukopa kwa fujo...
 
Watanzania wengi ni masikini na mzunguko wao wa hela ni wa humu humu ndani hawana muunganiko na dunia...ukiwakamua hawa unawamaliza kabisa, ndipo alipokosea Mzee wetu...

Kazi kubwa iliyopo ni kufungua nchi na kuwaunganisha watanzania wengi na dunia, kuileta dunia hapa, serikali kuacha kufanya biashara ili sasa mzunguko uwe mkubwa mtaani..Hali hii itasaidia kuendesha miradi huku maisha mtaani yakiendelea kama kawaida...
 
Amejenga masoko alafu wamachinga wapo kila sehemu, nini faida yake?
 
Mkuu unaweza kutaja viwanda vilivyoinuka upya wakati wa magu?

Mkuu uchumi wa kati upi? Ile lower side tuliyoingia ni kwasababu tumekuwa na increase ya mikopo na sio ya gdp. Wale wanakuingiza kule ili waendelee kukukopesha.
 
JPM ametwaliwa ili watanzania milioni 60 wapone imagine angeendelea kwa miaka mitano nchi ingekuwaje? Na wale wapuuzi wengine walitaka atawale miaka 20 zaidi Mungu akasema nitaliponya taifa langu Tanzania.
Baada ya utawala wake kama ungefikisha miaka 15 ingekuwa sio ajabu kukuta mwanamume/ mwanamke anatembea makalio yako nje.Magufuli alikuwa anarudisha Enzi za Mawe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…