Tuweke ukweli hapa; nini hasa chimbuko la ugomvi wako na jirani yako?

Wahaya tunaonewa. Weka msingi wa fence. Au Kuna baadhi ya watu huwa wanajenga beacon (ndefu kidogo) za tofali Kama kozi 3 kwenye Kona zote za kiwanja.
Au zungushia nguzo za cement na wire.
Wakora waitu[emoji122][emoji120]
 
Ugomvi kati ya majirani wawili mara nyingi ni matokeo ya fahari wawili kutoweza kukaa zizi moja.

Jirani yangu wa kwanza nikiri kabisa mimi ndie niliyemkosea. Nilianza kujenga ukuta kwenye mpaka kabisa wa viwanja vyetu. Yeye alikuwa anaishi hapo na mimi nilikuwa sijahamia maana nyumba ilikuwa bado kukamilika. Bahati mbaya mafundi wakawa wameingia kwake kama centimeter 7 hivi. Kesho yake asubuhi walikuta jamaa ameshusha ukuta wote kozi nne urefu wa meter 25. Niliiwaambia waache kujenga mpaka nirudi maana sikuwa mjini.

Niliporudi jioni ilibidi niende nikamuone mshkaji kwake. Kwanza nilimkuta akiwa ameshajiandaa kwa mtifuano mkali maana inaonekana alipoona ujenzi umesimama labda alidhani nipo napanga mashambulizi heavy. Nilifika na kumuomba sana radhi kwa kuingia ndani ya kiwanja chake na nikamwambia tulisitisha ujenzi ili nije anionyeshe nijenge na kuishia wapi maana labda yeye anafahamu zadi mipaka yetu. Jamaa aliona aibu mwisho wa siku akanipa meter moja zaidi kuingia kwake. Mpaka leo jamaa ni mshkaji.

Jirani wa pili yeye ni recent case na mpaka leo naona kama mahusiano yameyumba. Ilianza siku nilipotuma kijana wa kazi aende kwake akakate majani ya miti yake yaliyokuwa yamerefuka na yakawa yanagusa wire za electrical fence na hivyo kupiga kelele kila ninapowasha. Jamaa aliwaka sana kwamba kwanini nitume mtu na nisiende mimi mwenyewe? Mimi sikuona sababu ya kwenda kumbembeleza mtu ambaye kimsingi alipaswa kukata hayo majani yeye mwenyewe. Well, yale majani tuliamua kuyakatia kutokea ndani ya fensi yetu.
 
Dah
 
Wakuu nimepata dawa ya huyu mama mshenzi anaekata mchai chai wangu.nimemuendekeza sana amenionea sanaaa.amerudia kukata mchai chai wangu bana.nilichofanya niliamka SAA Tisa usiku nkaenda kwenye mlango wake nkakuta vi yebo yebo vya watoto wake na Ndala zake.nilichukua ule wembe wa theatre nikafyeka fyeka yebo yebo na Ndala zake nkaziacha mlangoni kwake vile vile..kulipokucha sasa hayo macho ya maswali alivyokua ananitolea macho Huyo mama na mie ndo najifanya sina habarii kanisa napiga na tu pambio.nyoko zake mbona wiki hii hajaukata....arudie kuukata tena nimuoneshe.kipindi hichi ntachukua bomba LA sindano nivute maji ya betri akianika kanga kwenye kamba namwagia...nimeamua kua baba ubaya sasa....yani miaka mitatu sijawai chuma mchai mchai???maninaaa zake
 
Mkuu we ni mzee baba kweli?
Mchaichai wa nini,mbona kama ishu ndogo sana mzee baba
 
WAHA wanasema AMAGAMBO BUKEBUKE!

Ulakoze!!!!!!
 
Uzi mzuri kweli unafundisha na kuburudisha, binadamu tuna roho mbaya sana sometimes, na vioja hivi vinapatikana uswazi au half uswazi kwa wakishua Ni nadra kukuta hizi mambo

Mi nina visa vingi ila nikiona jirani waluwalu mara nyingi nakula buyu no salamu na nachukua hatua ikihitajika sana dhidi uonevu naofanyiwa (ukorofi pia ni hawa wajinga wamenifundisha ubabe), huwa sijui kubembeleza mtu asiejali umuhimu wa mahusiano

Kingine niliwahi kuishi huko mpakani Kama tunavyojua mipakani kunakuwaga na raia wa nchi jirani wanaendesha maisha nchi isiyo yao, sasa Basi usiombe upakane na muhaya, mchaga, mganda na mnyarwanda especially mtutsi na mbaya ukute wanakuzidi uchumiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚lazima uwe mnyonge na utahama tu, ukiwazidi basi watakufanyia chokochoko na usishangae ukawa Kama uko kisiwani kabisa na unaweza kufa wanakuona hawakusaidii kwa chochote ili tu wakukomoe, hawa watu wengi wao sio kabisa kuishi nao ujirani
 
Sijaona mantiki ya kutaja kabila. Mbna wa kwanza hujataja
 
Mkuu we ni mzee baba kweli?
Mchaichai wa nini,mbona kama ishu ndogo sana mzee baba
We unaona ni mchai chai tu??je juhudi zangu za zaidi ya miaka mitatu kupambana mchai mchai ukue huoni??miaka 3 na zaidi mchai mchai haukui???kwahio aendelee kunionea tuuu??
 
Mzee wa mchai chai[emoji23][emoji23]
 
Jirani yako anasemaje
Wakati mafundi wanaanza tu msingi wakachukua vitofali kwa jirani nikiwa sijui
Akanipigia simu analalamika wameiba tofali kibao, weekend moja nikaenda kucheki site nakuta tuvipande tuchache tu, cha ajabu nae mafundi wake wamechimba shimo la udongo wa kujengea kuvuka mpaka wangu nikampigia akasema nae hakuwa anajua

Nikakausha sema najiandaa hapa, bado sijahamia lakini najiona kabisa nikiishi na jirani mtata

Kwahiyo nasoma visa hapa najifunza, siku akilizua tayari nitakuwa na mbinu kibao kumdhibiti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…