Tuweke ukweli hapa; nini hasa chimbuko la ugomvi wako na jirani yako?

Tuweke ukweli hapa; nini hasa chimbuko la ugomvi wako na jirani yako?

Kuna watu hawapendi ujirani wa amani kabisa. Na kundi hili la majirani wagomvi ni kubwa sana kuliko tudhaniavyo!

Binafsi ugomvi mkubwa na jirani yangu ilikuwa ni kwenye kununua Umeme. Huyo umeme ukiisha tu alikuwa hawashi taa na hapandishi mapazia anajifungia kimya!

Tulikalishwa vikao hadi vya mjumbe lakini wapi! Ikabidi nihamie nyumba nyingine! Huku nako nilikutana na mama mmoja jirani mchafu hatari, watoto wake walikuwa wanajisaidia kwenye corridor! Halafu hajali wala nini, ukiweka kanyagio la kufutia miguu ukitoka baadae unarudi unakuta wamelichukua wao kufutia miguu!

Nikadhani mtu aliyejenga hana kero ya ugomvi na majirani kumbe huku ndiko kuna balaa zaidi! Huku nako kuna watata vilevile, usipoangalia unaweza pata presha. Wapo majirani mabingwa wa kusogeza mipaka ya viwanja! Huu ugomvi ni mwingi sana umeharibu mahusiano ya majirani wengi sana!

Wapo pia majirani wanaojenga hadi kiwanja wanamaliza halafu paa la nyumba linamwaga maji kwa jirani ilimradi tu wawakere!

Yote tisa, wapo majirani wafugaji wenye mifugo inayoharibu mali za jirani yake na wala hawajali.

Nisiseme mengi. Leo Naomba tushirikishane, ni mgogoro gani hasa ulionao wewe na jirani yako hapo?
Uchawi, nasikia ukimpa shs 10,000/= huyo mama anakutembelea usiku.
 
Wengine Ni mazoea wengine Ni urithi

Kuna mdada ni mke wa mtu akimuona mtu hamjui anamuomba amnunulie soda,anaowajua ni balaa anapenda kuomba omba sijui kwanini na anaona kawaida na sio kwamba hana uwezo
 
nililewa kwakua milango yetu inafata nkajkuta nmelala seblen kwake et akamaind mpaka leo atusemeshan nangoja mkesha wa pasaka nilewe nkanye mlangon kwake
Lete mrejesho vipi pasaka ulishusha mzigo mlangoni kwa jirani?
 
Kuna mdada ni mke wa mtu akimuona mtu hamjui anamuomba amnunulie soda,anaowajua ni balaa anapenda kuomba omba sijui kwanini na anaona kawaida na sio kwamba hana uwezo
Huyo mkuu,kifupi -
Ana tatizo la kisaikolojia
au kirefu-
anajitakisha kwa nguvu
 
Ugomvi kati ya majirani wawili mara nyingi ni matokeo ya fahari wawili kutoweza kukaa zizi moja.

Jirani yangu wa kwanza nikiri kabisa mimi ndie niliyemkosea. Nilianza kujenga ukuta kwenye mpaka kabisa wa viwanja vyetu. Yeye alikuwa anaishi hapo na mimi nilikuwa sijahamia maana nyumba ilikuwa bado kukamilika. Bahati mbaya mafundi wakawa wameingia kwake kama centimeter 7 hivi. Kesho yake asubuhi walikuta jamaa ameshusha ukuta wote kozi nne urefu wa meter 25. Niliiwaambia waache kujenga mpaka nirudi maana sikuwa mjini.

Niliporudi jioni ilibidi niende nikamuone mshkaji kwake. Kwanza nilimkuta akiwa ameshajiandaa kwa mtifuano mkali maana inaonekana alipoona ujenzi umesimama labda alidhani nipo napanga mashambulizi heavy. Nilifika na kumuomba sana radhi kwa kuingia ndani ya kiwanja chake na nikamwambia tulisitisha ujenzi ili nije anionyeshe nijenge na kuishia wapi maana labda yeye anafahamu zadi mipaka yetu. Jamaa aliona aibu mwisho wa siku akanipa meter moja zaidi kuingia kwake. Mpaka leo jamaa ni mshkaji.

Jirani wa pili yeye ni recent case na mpaka leo naona kama mahusiano yameyumba. Ilianza siku nilipotuma kijana wa kazi aende kwake akakate majani ya miti yake yaliyokuwa yamerefuka na yakawa yanagusa wire za electrical fence na hivyo kupiga kelele kila ninapowasha. Jamaa aliwaka sana kwamba kwanini nitume mtu na nisiende mimi mwenyewe? Mimi sikuona sababu ya kwenda kumbembeleza mtu ambaye kimsingi alipaswa kukata hayo majani yeye mwenyewe. Well, yale majani tuliamua kuyakatia kutokea ndani ya fensi yetu.
fensi ipo na bado mnagombana.je ingekuwa changanyikeni uswahilini?[emoji3][emoji3][emoji3]
 
daaah mimi nina jirani ambae ni bora kuishi na ngedere mbwa wale!!nilinunua shamba miaka ya nyuma,tumepakana na yeye akawa shahidi,mwanzoni tulikuwa vizuri na nilikuwa nahifadhi vifaa vyangu vya ujenzi kwake,chokochoko ya kwanza,alijenga banda kwenye eneo langu,nikamuuliza akakiri ataliondoa ni temporary tuu,baada ya muda akaanza kujenga kwa tofali,nikamuuliza akaruka,siku hiyo hiyo nikanunua tofali nikamuachia hatua za ziada nyingine kadhaa nikajenga ukuta,nikaanza kufuga pale kwa ustawi mkubwa tuu,baada ya muda nashangaa mifugo inaibiwa,kufuatilia mishe zote za wizi zinapangiwa kwake,akaanza kushawishi vijana kila anayekuja lazima amvuruge!amenifanyia uovu mwingi sana huyu takataka!yeye na familia yake,mbaya zaidi alikuwa na kacheo kijijini na ndio ametumia kunifanyia uovu,iko siku ataingia timing tuu,nyambaf....yaani najisikia kichefuchefu
pole mkuu......majirani ni mitihani kwa nchi zetu hizi africa...
 
Kuna watu hawapendi ujirani wa amani kabisa. Na kundi hili la majirani wagomvi ni kubwa sana kuliko tudhaniavyo!

Binafsi ugomvi mkubwa na jirani yangu ilikuwa ni kwenye kununua Umeme. Huyo umeme ukiisha tu alikuwa hawashi taa na hapandishi mapazia anajifungia kimya!

Tulikalishwa vikao hadi vya mjumbe lakini wapi! Ikabidi nihamie nyumba nyingine! Huku nako nilikutana na mama mmoja jirani mchafu hatari, watoto wake walikuwa wanajisaidia kwenye corridor! Halafu hajali wala nini, ukiweka kanyagio la kufutia miguu ukitoka baadae unarudi unakuta wamelichukua wao kufutia miguu!

Nikadhani mtu aliyejenga hana kero ya ugomvi na majirani kumbe huku ndiko kuna balaa zaidi! Huku nako kuna watata vilevile, usipoangalia unaweza pata presha. Wapo majirani mabingwa wa kusogeza mipaka ya viwanja! Huu ugomvi ni mwingi sana umeharibu mahusiano ya majirani wengi sana!

Wapo pia majirani wanaojenga hadi kiwanja wanamaliza halafu paa la nyumba linamwaga maji kwa jirani ilimradi tu wawakere!

Yote tisa, wapo majirani wafugaji wenye mifugo inayoharibu mali za jirani yake na wala hawajali.

Nisiseme mengi. Leo Naomba tushirikishane, ni mgogoro gani hasa ulionao wewe na jirani yako hapo?

Mm napenda kunywa pombe kwa raha zangu lkn nikijinywea pombe zangu bila kugombana na mtu nikifika zangu nyumbani najiimbiaga nyimbo zangu usiku kucha lkn cha ajabu et wamenipeleka serikari za mitaa et nawapigia kelele yaan majilani ni wakorofi sn iv namawazo ya huhama zangu.
 
😂😂😂 We jamaa kwa vijinyimbo vyako Ni kajiukorofi ka chinichini
 
Mm napenda kunywa pombe kwa raha zangu lkn nikijinywea pombe zangu bila kugombana na mtu nikifika zangu nyumbani najiimbiaga nyimbo zangu usiku kucha lkn cha ajabu et wamenipeleka serikari za mitaa et nawapigia kelele yaan majilani ni wakorofi sn iv namawazo ya huhama zangu.
Kwahiyo nani mkorofi kati yako na wao?
Naomba jibu pombe ikiisha kichwani
 
Ukijaaliwa
1- mke mwema
2- Jirani mwema
3- Kipando kizuri

Aisee shukuru sanaa na na maisha utaenjoy sanaaaa
 
Mimi BADO ni mwanafuzi na sijajenga, Naishi room ya kupanga. Kwenye haya maisha nilichojifunza ni kwamba majirani wengi hawana shida. Tatizo litaibuka mkishazoeana. Mwanzoni Mazoea huonekana mema lakini baadae huleta dharau na magomvi yasiyo na ulazima. dawa ni ku hide details zako majirani wasikujue kwa undani. Na katika Hili Mimi nimefaulu. Ni mwaka wa tatu hapa nilipopanga lakini hakuna jirani anayenifahamu kwa jina langu halisi Wala kazi ninayoifanya hapa mjini. Wanafunzi wenzangu wanajua kuwa Mimi Ni Mkurya wa Mara wakati Hata Sina vinasaba vya Wakurya Wala sijawahi kufika Mara. Hide_your_details

Unakuta mtu anafahamiika kwa undani kiasi kwamba mtu yeyote anaweza kumuelezea in and out plus personal future plans! Mtu wa aina hii ni rahisi kuwekewa vikwazo kwenye safari yake ya maisha kwa sababu maadui wapo na hawana alama na shida ni kwamba maadui wengi ni miongoni mwa ndugu na watu unaocheka nao kila siku. Hide_your_details_as_much_as_you_can
 
Jirani kanizibia njia ya kupitisha gari langu. Nimetoka asubuhi narudi jioni nakuta bonge la fence ukuta umepanda kozi 6. Tangu siku hiyo sina hamu nae, nikaongea na jirani wa pembeni akaniuzia njia TZS 1,000,000/= ndiko napitisha gari yangu siku hizi. Sasa kuna ujirani hapo

Hii ya kuuziwa njia inakuwaje mdau
 
Hahahhaahhahahaaha...iliwah nikita nahamia kwangun2017..jiran ana mchai chai nikawa naenda kuomba ananipa .khaaa ikafika kipindi akawaambia wanangu mwambie mama yenu apande wake mbona maua anapanda kila siku🤣🤣..tulicheka..nikapanda wangu...ila sasa ajabu akiishiwa stop ya kwanza kwangu..khaa .namkomoa nampa hela then simdai ..shenji
Usipende kugawa hela utafungiwa riziki mpe mtu anachohitaji sio hela utakuwa masikini wa kutupwa
 
Wapo pia majirani wanaojenga hadi kiwanja wanamaliza halafu paa la nyumba linamwaga maji kwa jirani ilimradi tu wawakere!
Kwenye nafikiri iwepo haja ya kuwa na public sewage system na uwepo wa vibali vya ujenzi.
 
Nipo na jirani yangu paka wangu alihamia kwake mwanzoni alikuwa anaonesha kumjali lakini alipozaa akaanza kuuza vitoto vyake kimya mya sasa na jana nimemtolea uvivu nikamwambia najua paka wangu amezaa ole wako uviuze utajuta binadamu kazi kweli kweli mi nadhani bora kuonekana kauzu kuliko kuwa na watu wabovu eti majirani
 
Back
Top Bottom