Tuweke ukweli hapa; nini hasa chimbuko la ugomvi wako na jirani yako?

Duh pole sana
 
Case yako inafanana na yangu kabisa. Sema yeye hiyo barabara ilikuwa kwenye kiwanja chake. Nilinunua barabara kwa 1M mambo yanaenda poa tu ila jamaa hata akikuta umekaa sehemu fulani hasalimii tangu mwaka 2015 hatujwahi peana hata salam.
Maisha haya bana.
 
Aiseeee
 
Jirani mwenye mifugo anataka mifugo yake iwe inakula kwenye eneo la mwenzake [emoji23][emoji23][emoji23]aisee kwa kweli ni shida
 
Namuona jirani anaongea na mke wake, baada ya dk 5 mke anakuja nyumbani kaingia ndani anaomba jembe, mara naona mme wake akiongozana na kundi la wajumbe na wazee wanaingia ndani wanasema wanahisi nimemuweka mke wa jamaa kimada,, nikawaambia si kweli wakasema ngoja tusachi kama kweli, kuingia chumbani wakamkuta kalala kitandani, wanamuamsha anakoroma tu baadae ndo anaamka anajinyooshaaa hajielewi
 
Mtego huo
 
Ukihama na wewe kazibe hako ka njia, mbwai mbwai.
 
Acha uoga kamuulize ni nani anakata mchaichai wako, umewahi muuliza? Na bwana ake naye mwambie kuwachutaki mtu akate mchaichai wako.
 
Kero yangu ni huyu jirani kuja kila mara kuomba kuingiza LUKU yaani haipiti siku2 bila kuja tena muda mwingine unasikia hodi usiku saa4 au saa5 tayari ukiwa umejipumzisha ukitoka unamkuta ni yeye au kamwagiza kijana wake anaomba kuingiza LUKU.

Aisee jirani kama utapita huku acha uduwanzi wa kuweka umeme wa buku buku. Weka umeme angalau wa elfu20 halafu sio usubiri hadi LUKU inaisha na umeme kukatika kabisa na kuja kusumbua watu usiku, aisee ipo siku nitakukaushia mlale giza.
 
Muda mwingine upole unatuponza. Ubabe Ni muhimu. "The great question of the day will not be settled by means of speeches and majority decision but by iron and blood".
 
Kama una hakika Ni yeye anayekata, mtafute mfundishe jinsi ya kupanda, mpe mche mmoja au miwili kwamba akapande kwake.
Hapo utakuwa umemfundisha kuvua samaki. Akileta kiburi Basi hapo na makofi yatumike.
 
Unasema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…