Pre GE2025 Tuzijue "Sera za Mbowe" dhidi ya "Sera za Lissu," uchaguzi mwenyekiti CHADEMA 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Haya ni kutokea katika waliyosema wenyewe hadi sasa, watia nia hawa:

A. SERA ZA LISSU:

1. Ukomo wa madaraka kwa Kiongozi wa chama.
2. Uwazi katika mapato na matumizi.
3. Upatikanaji wa wawakilishi wa chama mfano Viti maalumu na ngazi zingine zifuate utaratibu.
4. Uwepo ukomo wa kupata nafasi za viti maalumu yaan time limit.
5. Katiba ya chama kubadilishwa.
6. Kutokomeza Rushwa ndani ya chama.

IMG_20241226_071102.jpg

B. SERA ZA MBOWE

1. Nimekitoa chama mbali sana na mi ndo nimebakia najua in and out.
2. Siwezi kuondoka nikaacha chama katika mvurugano wa namna hii.
3. Bado Nina nguvu sana naweza fanya kazi na vikao nane kwa siku “Ebo give me a break” sijachoka.
4. Sijatimiza Umri aliostaafu nao Mtei wa miaka 68, mpaka nitimize.
5. Maridhiano yana umuhimu katika siasa ntaendelea kuyatumia inapobidi.
6. Nimekaa gerezani sababu ya chama.

Pia soma: Uchaguzi wenyeviti taifa Chadema, Debates za wazi ziandaliwe kwa wagombea tuzione mbivu na mbichi zao, itapendeza zaidi!

Uchaguzi ni sera.

Kufahamika wazi wazi nani anasimamia nini, ni muhimu zaidi.

Uchaguzi si mahaba!

Kwa hisani ya mdau: Tanzania Abroad TV (TAT).
 
Haya ni kutokea katika waliyosema hadi sasa watia nia hawa:

A. SERA ZA LISSU:

1. Ukomo wa madaraka kwa Kiongozi wa chama
2. Uwazi katika mapato na matumizi
3. Upatikanaji wa wawakilishi wa chama mfano Viti maalumu na ngazi zingine zifuate utaratibu
4. Uwepo ukomo wa kupata nafasi za viti maalumu yaan time limit
5. Katiba ya chama kubadilishwa
6. Kutokomeza Rushwa ndani ya chama

View attachment 3185289

B. SERA ZA MBOWE

1. Nimekitoa chama mbali sana na mi ndo nimebakia najua in and out
2. Siwezi kuondoka nikaacha chama katika mvurugano wa namna hii,
3. Bado Nina nguvu sana naweza fanya kazi na vikao nane kwa siku “Ebo give me a break” sijachoka.
4. Sijatimiza Umri aliostaafu nao mtei wa miaka 68, Mpaka nitimize
5. Maridhiano yana umuhimu katika siasa ntaendelea kuyatumia inapobidi
6. Nimekaa gerezani sababu ya chama

Pia soma: Uchaguzi wenyeviti taifa Chadema, Debates za wazi ziandaliwe kwa wagombea tuzione mbivu na mbichi zao, itapendeza zaidi!

Uchaguzi ni sera.

Kufahamika wazi wazi nani anasimamia nini, itapendeza zaidi.

Kwa hisani ya mdau: Tanzania WikiLeaks.
Hapo haujaitendea haki thread. Umeandika ukiwa na mlengo wako tayari ili watu wakufuate. Ni vyema ukaweka sources za hizo sera, na uweke wazi kuwa hata wagombea wa nafasi ya chama kumbe nao huwa wanatakiwa kuwa na sera hata kama zitatofautiana na katiba ya chama waliyoitunga wanachama wengi.
 
Nimenukuu mmoja baada ya mwingine.

Wapi nani hajasema nini au kasema nini zaidi weka tufanye maboreshe.

Ndiyo maana subject iko wazi tuzijue sera zao na pia miito ya kuwa na midahalo ya wazi wahojiwe kwenye viti vya moto.

Wapi hapakutendewa haki nani, ndugu mjumbe?

Cc: imhotep, Erythrocyte, Pascal Mayalla, JokaKuu, Retired, Yoda, Tlaatlaah, Allen Kilewella, waliokuwamo na wasiokuwamo.
 
Nimenukuu mmoja baada ya mwingine.

Wapi nani hajasema nini au kasema nini zaidi weka tufanye maboreshe.

Ndiyo maana subject iko wazi tuzijue sera zao na pia miito ni kuwa na midahalo.

Wapi hapakutendewa haki ndugu mjumbe?

Cc: imhotep, Erythrocyte, Pascal Mayalla, JokaKuu, Retired, Yoda, waliokuwamo na wasiokuwamo.
Kwa hiyo walichosema ndio sera? Mtu akisema wananchi wanatekwa, nayo utaiongeza katika sera? Wote hao wanaongozwa na katiba plus sera za chama. Katika ngazi hii huwezi kuja na sera tofauti na za chama. Mfano mtu hawezi kusema hataki majimbo wakati ni uamuzi uliofanywa na vikao vikubwa. Yeye aombe kura halafu akipata madaraka ndio ashawishi mabadiliko ya anachoona hakifai
 
Tambua maana ya sera ndugu.

"Sera ni asemayo mgombea kujinadi ili achaguliwe."

Au mgombea wako ayasemayo kujinadi hujayapenda?
 
Mjadala uko wazi na wewe tiririka mkuu tukusome
 
Tambua maana ya sera ndugu.

"Sera ni asemayo mgombea kujinadi ili achaguliwe."

Au mgombea wako ayasemayo kujinadi hujayapenda?
Mimi sio mjumbe wa Mkutano wa Uchaguzi, kwa hiyo haisaidii lolote kuwa na 'mgombea wangu' maana sina uamuzi zaidi ya kuukasimisha kwa wajumbe waliopo kikatiba.

Yeyote atakayechaguliwa itabidi niishi naye, na hiyo ndiyo maana ya demokrasia, yaani kukubali sauti ya wengi.

Kuhusu sera, sina uhakika kama wagombea wa ngazi ya Chama nao huwa wana sera zao. Nijuavyo, wagombea wa Uchaguzi wa Kitaifa huwa wananadi sera za vyama vyao, sijajua hawa waliopo kwenye chama kimoja wanatakiwa wawe na sera pia, na zitanadi nini!
 
Tunaweza kuita sera au dira kifupi ni kuwa mgombea anaeleza jinsi ambavyo atakiongoza chama kama akipewa nafasi ya kuongoza.
 
ninachofurah tu, pamoja na watu kusema Chadema imekufa, lakini ndio chama kinachomulikwa zaidi, CUF kuna uchaguzi, nafasi ya mwenyekiti ina wagombea 9 akiwemo Lipumba lakini hakuna anayechambua
 
Mimi sio mjumbe wa Mkutano wa Uchaguzi, kwa hiyo haisaidii lolote kuwa na 'mgombea wangu' maana sina uamuzi zaidi ya kuukasimisha kwa wajumbe waliopo kikatiba.

Yeyote atakayechaguliwa itabidi niishi naye, na hiyo ndiyo maana ya demokrasia, yaani kukubali sauti ya wengi.

Kuhusu sera, sina uhakika kama wagombea wa ngazi ya Chama nao huwa wana sera zao. Nijuavyo, wagombea wa Uchaguzi wa Kitaifa huwa wananadi sera za vyama vyao, sijajua hawa waliopo kwenye chama kimoja wanatakiwa wawe na sera pia, na zitanadi nini!

Kumbe kama si sera ulidhani kunachaguliwa nyuso?
 
Kitendo cha kung'ang'ania madaraka ujue sera yake ni ya ufujaji wa mali ya chama
Kwa nini useme kung'ang'ania madaraka wakati katiba ya chama tena chenye wanasheria nguli kabisa ndio inaruhusu asiwe na ukomo, na anapata kura za wajumbe?

Nadhani ungekuwa na hoja tofauti ningekuelewa, kwamba labda anawahonga wapiga kura au anaiba kura. Lakini suala la kugombea tena na tena, hilo lipo kidemokrasia, yaani uhuru wa kupiga na kupigiwa kura ili kuruhusu sauti za wanachama. Unajua haya mambo ya kuzuia vitu vilivyokubaliwa katika katiba yenu wote ndio ukandamizwaji wa demokrasia?
 
Kumbe kama si sera ulidhani kunachaguliwa nyuso?
Unahitaji zaidi kujua maana ya sera. Sera ni dira ya kuiongoza taasisi kufikia malengo fulani katika kipindi fulani. Sasa mawazo ya mtu mmoja hayawezi kukubalika yatumike kuipeleka taasisi katika uekekeo anaoutaka yeye. Katika ngazi hii, mgombea anapaswa aeleze namna na mbinu za kutekeleza sera ambazo tayari zipo, sio alete sera zake binafsi. Hapa haongozi familia yake, anaongoza taasisi ambayo ipo, tena mbaya zaidi wote wameikuta ipo.
 
Kwa nini useme kung'ang'ania madaraka wakati katiba ya chama tena chenye wanasheria nguli kabisa ndio inaruhusu asiwe na ukomo, na anapata kura za wajumbe?

Nadhani ungekuwa na hoja tofauti ningekuelewa, kwamba labda anawahonga wapiga kura au anaiba kura. Lakini suala la kugombea tena na tena, hilo lipo kidemokrasia, yaani uhuru wa kupiga na kupigiwa kura ili kuruhusu sauti za wanachama. Unajua haya mambo ya kuzuia vitu vilivyokubaliwa katika katiba yenu wote ndio ukandamizwaji wa demokrasia?
Hata kama katiba inaruhusu ni kwanini utumie rushwa kupata uongozi wakati unapendwa.
Rejea wanachama aliowaita nyumbani kwake, aliwaita ili iweje
 
Maana ya sera:

Sera ni seti ya kanuni, maadili na nia zinazoongoza kufanya maamuzi na ugawaji wa rasilimali kwa suala mahususi.
 
Hata kama katiba inaruhusu ni kwanini utumie rushwa kupata uongozi wakati unapendwa.
Rejea wanachama aliowaita nyumbani kwake, aliwaita ili iweje
Walau hili linaweza kuwa hoja. Sio mtu anasema tu eti anang'ang'ania madaraka, wakati akina Lissu wapo tu kama wanasheria wa chama wala hawajataka kubadilisha kifungu cha ukomo.

Sasa kama wanachama kuja kukusikia nyumbani (Mbowe) na kwenye ukumbi wa Hotel maarufu (Lissu) mojawapo itatafsiriwa kuwa ni rushwa, basi miongozo ya mwenendo wa uchaguzi ipo, na mgombea anaweza kuenguliwa mapema tu.
 
Hapo haujaitendea haki thread. Umeandika ukiwa na mlengo wako tayari ili watu wakufuate. Ni vyema ukaweka sources za hizo sera, na uweke wazi kuwa hata wagombea wa nafasi ya chama kumbe nao huwa wanatakiwa kuwa na sera hata kama zitatofautiana na katiba ya chama waliyoitunga wanachama wengi.
Ili mzani uweze ku balance na uridhike, ungeweka yale unayoona yameachwa
 
Back
Top Bottom