Pre GE2025 Tuzijue "Sera za Mbowe" dhidi ya "Sera za Lissu," uchaguzi mwenyekiti CHADEMA 2025

Pre GE2025 Tuzijue "Sera za Mbowe" dhidi ya "Sera za Lissu," uchaguzi mwenyekiti CHADEMA 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hakuna vyama vya siasa vya maana vinavyoweka ukomo wa madaraka duniani, Hakuna hoja zenye mashiko hapo.
 
Unahitaji zaidi kujua maana ya sera. Sera ni dira ya kuiongoza taasisi kufikia malengo fulani katika kipindi fulani. Sasa mawazo ya mtu mmoja hayawezi kukubalika yatumike kuipeleka taasisi katika uekekeo anaoutaka yeye. Katika ngazi hii, mgombea anapaswa aeleze namna na mbinu za kutekeleza sera ambazo tayari zipo, sio alete sera zake binafsi. Hapa haongozi familia yake, anaongoza taasisi ambayo ipo, tena mbaya zaidi wote wameikuta ipo.
Usichanganye sera na ilani
 
Sijaona mbowe sera zake, ni mbwembwe tu.Lissu amejipanga.Tunaomba anayejua sera za Mapunda na Odero
 
Kwa nini useme kung'ang'ania madaraka wakati katiba ya chama tena chenye wanasheria nguli kabisa ndio inaruhusu asiwe na ukomo, na anapata kura za wajumbe?

Nadhani ungekuwa na hoja tofauti ningekuelewa, kwamba labda anawahonga wapiga kura au anaiba kura. Lakini suala la kugombea tena na tena, hilo lipo kidemokrasia, yaani uhuru wa kupiga na kupigiwa kura ili kuruhusu sauti za wanachama. Unajua haya mambo ya kuzuia vitu vilivyokubaliwa katika katiba yenu wote ndio ukandamizwaji wa demokrasia?
Katiba ya Chama Aliibadilisha Nani?
Na kwanini aliibadilisha mwaka 2006 miaka 2 baada yaKuanza kuongoza?

Ibara ya 6.3.2(C) Kwanini Ilibadilishwa
 
Usichanganye sera na ilani
Huwezi ukawa na documents mbili zinazopingana. Mgombea hawezi kusema kipaumbele chake cha miaka mitano ni viwanda, wakati chama kinasema ni kilimo, na dira ya Taifa inasema teknolojia
 
Huwezi ukawa na documents mbili zinazopingana. Mgombea hawezi kusema kipaumbele chake cha miaka mitano ni viwanda, wakati chama kinasema ni kilimo, na dira ya Taifa inasema teknolojia
Kwa hiyo hauwezi ukawa na Katiba halafu ukawa na sheria na miongozo?
 
Kwa hiyo hauwezi ukawa na Katiba halafu ukawa na sheria na miongozo?
Haitakiwi miongozo isiendane na sheria, na sheria zisiendane na katiba.
Mfano, katiba iseme hakutakuwa na ukomo wa mwanachama kugombea uenyekiti, halafu sheria iseme mwenyekiti anayemaliza muda wake hatarusiwa kugombea tena nafasi hiyo baada ya kutumikia vipindi viwili vya miaka mitano mitano.
 
na mkutano mkuu ambao upo kikatiba
Una Muhtasari wa Mkutano mkuu Unaosema Hivyo..
Maana Muhtasari ya Mikutano yote hutumwa kwa Msajili na Msajili alisema kuwa Hakuna Ajenda yoyote iliyotoka ya Kubadilisha Katiba..
Mkutano wa Lini uliomtuma??
 
Muulize Dr. Slaa atakuelezea yote, maana yeye ndiye alikuwa mtendaji na anakiri hilo. Tena bahati nzuri anakiri huku akiwa team Lissu
 
Muulize Dr. Slaa atakuelezea yote, maana yeye ndiye alikuwa mtendaji na anakiri hilo. Tena bahati nzuri anakiri huku akiwa team Lissu
Hapana Anaogopa!
Kuna Vitu kwenye Chama wengi wanaogopa kuvisema kwa sababu ya Kumuhofia Mwenyekiti ni hatari sana
 
Haya ni kutokea katika waliyosema wenyewe hadi sasa, watia nia hawa:

A. SERA ZA LISSU:

1. Ukomo wa madaraka kwa Kiongozi wa chama.
2. Uwazi katika mapato na matumizi.
3. Upatikanaji wa wawakilishi wa chama mfano Viti maalumu na ngazi zingine zifuate utaratibu.
4. Uwepo ukomo wa kupata nafasi za viti maalumu yaan time limit.
5. Katiba ya chama kubadilishwa.
6. Kutokomeza Rushwa ndani ya chama.

View attachment 3185289

B. SERA ZA MBOWE

1. Nimekitoa chama mbali sana na mi ndo nimebakia najua in and out.
2. Siwezi kuondoka nikaacha chama katika mvurugano wa namna hii.
3. Bado Nina nguvu sana naweza fanya kazi na vikao nane kwa siku “Ebo give me a break” sijachoka.
4. Sijatimiza Umri aliostaafu nao Mtei wa miaka 68, mpaka nitimize.
5. Maridhiano yana umuhimu katika siasa ntaendelea kuyatumia inapobidi.
6. Nimekaa gerezani sababu ya chama.

Pia soma: Uchaguzi wenyeviti taifa Chadema, Debates za wazi ziandaliwe kwa wagombea tuzione mbivu na mbichi zao, itapendeza zaidi!

Uchaguzi ni sera.

Kufahamika wazi wazi nani anasimamia nini, ni muhimu zaidi.

Uchaguzi si mahaba!

Kwa hisani ya mdau: Tanzania Abroad TV (TAT).
Nimechekeka sana aiseee
 
Unahitaji zaidi kujua maana ya sera. Sera ni dira ya kuiongoza taasisi kufikia malengo fulani katika kipindi fulani. Sasa mawazo ya mtu mmoja hayawezi kukubalika yatumike kuipeleka taasisi katika uekekeo anaoutaka yeye. Katika ngazi hii, mgombea anapaswa aeleze namna na mbinu za kutekeleza sera ambazo tayari zipo, sio alete sera zake binafsi. Hapa haongozi familia yake, anaongoza taasisi ambayo ipo, tena mbaya zaidi wote wameikuta ipo.

1. Kwa hiyo unakubaliana hayo ndiyo kila mmoja kesha sema?

2. Zaidi labda ungependa kusikia kipi cha ziada au kipi kipungue wapi kwa nani?

3. Si unajua kauli ni Moja ya kigezo muhimu kwenye kuchaguliwa au kutoswa?

4. Vipi hili la mdahalo wa wazi Ili tujiridhishe?
 
Wataongea na kujinadi namna ya kutekeleza sera za chama ndani ya ukumbi wa mkutano. Sisi ambao hatutakuwa kwenye mkutano tusubiri kutangaziwa matokeo. Sasa wewe ambaye hauna sifa ya kupiga kura, huo mdahalo ukiusikia, utakufanya uamue jambo gani zaidi ya kusubiri kutangaziwa matokeo?
 
Kwani hawa wapiga kura hawajui wanakwenda kupiga kura kwa niaba ya wanachama?

Kuelekea dakika ya tisini: "Maoni ya wanachama yasiposikilizwa, CHADEMA njiani kulia na kusaga meno!"

Habari ndiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom