Tuzioneni tozo kwa facts na namba, zinaumiza hapa wenye namba tu

Songambele

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2007
Posts
4,710
Reaction score
2,587
Nimetuma 100,000 kwenda tigo pesa kwa simbanking, VAT sh. 974.70, govt levy sh. 1,009.00, TMS CHARGE TIGO 5,415.00, wenye akili timamu nimekatwa sh 7,398.7 kwa transaction hii moja tu. Pesa ilitoka kwa mshahara ambao wajuba walishakata PAYE. ni 7.4%. Mwaka 2017 kwa muamala kama huu nilikuwa naktwa sh. 2,360 maana yake sh. 5,038 imeongezwa kwa kipindi cha miaka mitano. Hali ya uchumi na inflation ni kubwa sasa kuliko ilivyokuwa 2017.

Jinsi mambo yanavyokuwa magumu tigo nimetoa sh 5,000 makato ni sh. 1,010 ambayo ni 20.2% hii ni zaidi ya 18% VAT. Tujuzane hapa mambo haya ya kukatana pesa tulizotolea jasho yataisha lini? Kwanini mnatukata kwa kiasi hiki kwa value ipi mnayotuongezea? Wale ambao mnalipwa kwa kushadadia na kujibu humu hata hili na nyie linawagusa pia, twendeni kwa namba kwanza.

Maisha sasa ni ghali mno na watunga sera lazima wawe flexible, kama mashirika ya kimataifa yanaona hali ngumu na kutoa nafuu kwa nini hawa viongozi wetu wanaweka pamba masikioni na kulazimisha kuendelea na mipango yao tu?! Maana hata midege tumelazimishwa kuyanunua bila kuona hali halisi na midude inaleta hasara. Reli toka waanze kujenga hawamalizi tu(Dar, Moro tu) politiks kila kukicha na wanatutwisha gharama bila sababu matokeo yake hata makampuni ya simu na yao yanatupiga pia.
 
Awamu hii imeamua kuua uchumi wa wananchi huku ikineemesha mifuko ya walamba asali. Huduma za jamii na ujenzi wa miundombinu ikidorora na mingine kupotezewa kabisa.

Mwenye ushahidi wa kituo cha afya kilichojengwa kwa tozo za miamala naomba jina la kituo hicho maana muda sasa tangu tozo hizi zianze
 
"Watanzania wameikibali Tozo na wanaifurahia"
 

Attachments

  • Magufuli.jpeg
    31.7 KB · Views: 6
"Hili nalo tutakwenda kulitizama na Mwanangu Mwigulu,lakini sharti muendelee kulipa tozo ya mshikamano"
Nauliza,nani kama Mama?,Mama endelea kufungua nchi usitishwe na wenye akili za kawaida!
Twafwaaa......Wallah!
 
Asubuhi hii nimetuma 55000/= kwa mama kupitia simbanking, nimekatwa 5500/=...

Kwa lugha rahisi ni kwamba makato au gharama za kutuma hiyo pesa ni 10% ya nilichomtumia mama.

Nikiendelea kutumia hii simbanking basi CRDB mje mnivishe kibao cha "ZUZU" nimekaa palee Kariakoo Gerezani.

 
Mwigulu aisee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…