Msalimieni
The bold jama...
Ujumbe
"Hatimaye imerudi "[emoji39]
Hiki kiuzi chenu nilikuwa nakipita tu, sasa ngoja niwatolee uvivu [emoji35] [emoji35]
Kwanza mimi ntabaki kuwa tomaso mpaka nikiona Kiba amekabidhiwa hiyo tuzo otherwise naona kelele za chura tu hizi.
Na endapo akikabidhiwa kweli hiyo tuzo hii nadhani ndio itakuwa tuzo yake ya kwanza ya kimataifa lakini naona ameanza kwa kujitilia nuksi! Tuzo gani unaipata kwa kung'ang'aniza?? Kuandika mibarua kama mwanasiasa?? Kutuma mashabiki wako wakatukane watoaji tuzo ili upewe wewe???
Hainogi, haisisimui, haina mvuto..
Hata kama tuzo ikitokea (nasisitiza kama ikitokea) akapewa hiyo tuzo hakuna ubishi kuwa Katika kile kinyang'anyiro hakukuwa na msanii aliyefanya vizuri kuliko Wizz, sasa unajisikiaje kutukana mitusi kumshutumu aliyepewa tuzo kwa kustahili kabisa anyang'anywe upewe wewe??? Hebu tuwe wa kweli, Africa yote hii ni moja wazungu ndio walituwekea hii mipaka hivyo hata wanaigeria ni ndugu zetu na ndugu yetu Wizz amefanya vizuri kuliko msanii yeyote yule mwaka huu. Mnaweza kuleta ubishi wa kupiga kura na mambo gani sijui lakini hamuwezi kubisha kuwa Wizz ni msanii bora mwaka huu kuliko msanii yeyeto yuke Afrika.
Naijua hulka ya Wizz na naijua hulka ya meneja wake Mr. Sande, inawezekana kabisa baada ya mashabiki wa kiba kufululiza kumtusi kwenye mitandao, labda wamesusa na wameamua wairudishe kwa hiari yao hiyo tuzo! Wizz sio mtu mwenye kukodolea macho tuzo, ni msanii anayejua thamani yake hata usipompa tuzo ndio maana kamwe huwezi kumkuta anahamasisha apigiwe kura. Ni mtu yuko bize na hustle zake, hanaga hizi drama za tuzo tuzo, binafsi kuna siku nimewahi kuongea na Ricardomomo yuke meneja wa WCB nikamshauri wamfanye Diamond kufuata mfano huu wa Wizz unaoonyesh ukomavu na kujitambua.
Mnasema kuwa mashabiki wa mondi walikuwa wanamtukana Davido na bado akapata collabo!! Aisee inamaana hamkumbuki au mnajisahaulisha makusudi??
Collabo ya Number 1 ilirekodiwa mwezi novemba 2013, video ikafanyika January 2014 na nyimbo ikatoka february mwaka huo. Bifu la mondi na davido lilianza mwezi wa 11 baada ya tuzo za channel O. Kwa ufupi bifu lao lilianza mwaka baada ya mwaka mmoja kupita toka collabo ifanyike..
Sasa juzi juzi Kiba amemgomea Wizz kupanda jukwaani mombasa kabla yake, leo mnawaandikia barua MTV wampokonye tuzo wampe yeye kiba.. Hivi mnadhani atawafikiriaje?? Akiwanyima collabo mtasema mondi kafanya figisu kwasababu ni maswahiba na Wizz?? Mnajiharibia wenyewe kila siku na mnakesha kutafuta mchawi wakati mnajiroga wenyewe!!
Kumbukeni Wizz ndiye mwanamziki mwenye mashabiki wengi zaidi huko west africa kwasasa, hivi vitendo mnavyomfanyia kumtukana na kumuandama kiasi hiki mnadhani mashabiki wake wataanza kumchukuliaje msanii wenu??? Kinyongo wanachokitengeneza dhidi ya msanini wenu itafanya iwe ngumu sana kwa Kiba kupenya west africa..
Narudia tena na tena, kiba hana washauri, hana watu strategic, hana gret thinkers, watu wanaowaza kibiashara kuhusu mziki, hana watu mahiri wenye uwezo wa kunetwork, hana management yenye kufikiri nje ya boksi.
Umahiri pekee walionao ni kulalamika, kuongeza maadui kila uchwao, kutafuta sympath kwa jamii hata kwa kupotosha, kujihisi wanajua ilhali wana mengi bado ya kujifunza, kumpumbaza msanii wao kwa kumuwekea kioo mbele yake mfano wa hadubini ili ajione mkubwa kuliko uhalisia.. Hii itawagharimu sana.!
Kiba ni msanii mzuri na anakipaji kikubwa but he has a long way to go.
The Bold.