Tuzogoe: Uliza swali la kizushi, tukujibu!

Tuzogoe: Uliza swali la kizushi, tukujibu!

Dduuh...mbaya hio
Ungepiga hata makelelee 😔
Mie kwa kulia ndio mwenyewe 🤣. Ila sio sana kulia mbele za watu hata nikipata msiba hutaniona nalia. Lkn nikikaa mwenyewe nalia sana. Tena kimyakimya. Kuna some relief fulani unapata ukiwa una jambo halafu ukalia
Umenikumbusha Kuna kipindi nilikuwa na insomnia nilikuwa nalia Sana 😭
 
Ukishakua tayari niambie nikuthaminishe kwanza 😅
Maana mambo yako ya kubadili badili ID yanafanya nikufikiri wewe ni tapeli @Bigballs baMtu ApolloShadow
😎😎 Nipo tayari nithamishe basi, achana na mabo ya ID, mie ndio maana sijifichi kuwa ID zangu, huwa nasahau password na email hii.. Ook.. Nipo tayari nifanyie evaluation basi
 
Mie kwa kulia ndio mwenyewe 🤣.
Mimi pia, nikiwa na furaha machozi, nikiwa frustrated nalia, nikiwa na huzuni nalia.
Ila sio sana kulia mbele za watu hata nikipata msiba hutaniona nalia.
Sina hiyo self control, hata mbele za watu nitalia.
Nilivyoanza kazi na kaumri kadogo Ilibidi nijifunze sana kutolia kazini nikiwa frustrated.
Lkn nikikaa mwenyewe nalia sana. Tena kimyakimya. Kuna some relief fulani unapata ukiwa una jambo halafu ukalia
Hii ya kimya kimya halafu iwe ile deep cry, unarelase, ukimaliza unajisikia kabisa kuna weight imekua lifted.
 
Pole sana mkuu,
Nina rafiki wa karibu sana, kwa sasa naweza kusema nina rafiki. Jamaa mwanzo ilikuwa akikerwa au akiwa na changamoto hata saa6 usiku atanipigia, atanieleza kila kitu. Nikawa simuelewi, yaani angeweza kunimwagia upupu wote, iwe ni mkewe, kazini kwake, madili yake, kukosa pesa nk.

Siku moja akaniambia Eroni unajua kwa nini nakuambia mambo yangu, nikamsikililiza..akasema mwanzo alikuwa analia😅😅😅😅 ila baadae alipoanza kuniambia majanga yake yote akaacha kulia, siku ile nilicheka sana😅😅😅.

So, badala ya kulia tafuta mtu unayehisi anaweza kukusikiliza bila kutoa judgements.

Unaliaje kidume😅😅
kulia ni njia ngumu ya kutoa sumu ila ndio njia yenye matokeo chanya...

kumwambia rafiki ni sawa...

ila si kila rafiki ana roho kama yako mkuu...

kuna rafiki anaweza kuchukua matatizo yako akayatumia kama fimbo kukuongezea machungu...

so, mimi hulia pia sometimes...

niliwahi kulia nikiwa mwenyewe, baada ya hapo nikajisikia vizuri...

sikulia kwa sauti hasha...

machozi yalitoka tu...
 
Back
Top Bottom