Twaha Kiduku amtwanga Alex Kabangu wa DRC, ashinda Mkanda wa UBO

Twaha Kiduku amtwanga Alex Kabangu wa DRC, ashinda Mkanda wa UBO

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Bondia wa Tanzania Twaha Kassim Lubaha anapambana na Alex Kabangu kutoka Congo DRC kushindania mkanda wa UBO Super Middle weight, African Title ambao hauna mwenyewe

===================
Twaha Kiduku ampiga Alex Kabangu, ashinda Mkanda wa UBO, Mkoani Morogoro

Bondia Mtanzania Twaha Kiduku amefanikiwa kushinda mkanda wa Afrika UBO kwa kumpiga Alex Kabangu kwa pointi katika pambano la uzito wa kati raundi nane lililofanyika usiku wa kuamkia Jumapili Machi 27, 2022, Mkoani Morogoro.

Kiduku ambaye jina lake kamili ni Twaha Kassim alionyesha kutawala pambano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Tanzanite Complex Hall dhidi ya Kabangu ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) aliyekuwa alitumia muda mwingi wa mchezo kukumbatia katika raundi zote nane.

Mara baada ya mchezo huo Kiduku alishukuru Watanzania kwa kumuunga mkono muda wote huku akisema pambano lilikuwa gumu kwa kuwa mpinzani wake alitumia muda mwingi kumkumbatia.

=====================

Mapambano ya utangulizi

1. Hamad Furahisha Vs Yunus Mhina Superfeather weight Rounds 4
Winner: Hamad Furahisha

2. Najma Isike Vs Halima Bondola
Super flyweight
Rounds 6
Winner: Najma Isike

3. Stumai Muki Vs Lulu Kayage
Super fly weight
Round 6
Winner: Stumai Muki

4. George Bonabucha Vs Juma Fundi (Pambano la Ubingwa)
Bantam Weight
Rounds 8
Winner: George Bonabucha

5. Pascal Goba Vs John Luwa
Super light weight
Rounds 6
Winner: Pascal Goba

6. Ayub Mwankina Vs Abdallah Yoba
Walter weight
Rounds 6
Winner: Ayub Mwankina

7. Magambo Christopher Vs Karim Mandonga
Super middle weight
Rounds 6
Winner: Magambo Christopher, KO

8. Shabani J. Kabuji Vs Paul Magesa
Super Bantam weight
Rounds 6
Winner: Paulo Magesa

9. Fatma Yazidu Vs Zawadi Kutaka
Feather weight
Rounds 6
Winner: Draw

10. Juma Misumari Vs Joseph Kafilimkoko
Winner: Juma Misumari, TKO
 
Mabondia wa Tanzania wajitahidi kwenda nje kupigana na wenye viwango, wakishinda huko watapanda kwenye chati very rapidly.

Nimeona juzi juzi "Mjeshi" Galiatano Ismail ametoka Ulaya kwenye pambano, japo alipigwa lakini naamini amepata experience muhimu itakayomsaidia huko mbeleni.

Tuwe serious tusibweteke "kushinda" mapambano kwenye hizi show za Azam.
 
Mapambano ya utangulizi

1. Hamad Furahisha Vs Yunus Mhina Superfeather weight Rounds 4
Winner: Hamad Furahisha

2. Najma Isike Vs Halima Bondola
Super flyweight
Rounds 6
Winner: Najma Isike

3. Stumai Muki Vs Lulu Kayage
Super fly weight
Round 6
Winner: Pending
Stumai yupo vizuri sana
 
Back
Top Bottom