Twende mbele, turudi nyuma: Nchi za wenzetu zilizoendelea wanapiga kazi

Hata ungekuwa wewe usingeweza kuandamana. Ilishatokea madaktari wakaandamana ila mkuu wao, alitekwa na watu wasiojulikana na mpk leo hakuna kesi ya kutekwa. Ilikuwa kipindi cha Kikwete
 
hakika,huko watu wakiwa kazini akuna story akuna simu ni kazikazi.

mfano huku kwetu bank kuna madirisha sita tellers,ila dirisha linalohudumia ni moja tu msululu wa watu na bado huyo muhudumu dakika moja simu dakika moja anahudumia.
Sababu hawalipwi kwa saa ajitume asijitume mwisho wa mwezi atapokea yote.
Kule ukichezea simu mfumo unakutoa nje pia usipojituma unajiibia mwenyewe
 
Huku uhakika wa kesho haupo thus watu wanapiga ukiwa na pesa upo juu ya Sheria kufungwa ni kupenda kwako
 
Bila kusahau na kodi wanalipa, njoo kwetu huku........ kukwepa kodi ndio ujanja.
 
Sababu hawalipwi kwa saa ajitume asijitume mwisho wa mwezi atapokea yote.
Kule ukichezea simu mfumo unakutoa nje pia usipojituma unajiibia mwenyewe
hapana iyo sio sababu,hali hiyo kwa hapa bongo niliyotolea mfano huwa inatokea sana kwenye bank au taasisi za umma,taasisi,bank au biashara binafsi uwezi kuta iyo hali na awalipwi kwa masaa.
 
Hii kaulimbiu yako ya twende mbele turudi nyuma ndo imefanya nyumba nyingi zimeishia kwenye renta.
Kama tunaenda mbele twende tu kama tunarudi nyuma tirudi.
mambo ya kwenda mbele na kurudi nyuma at the same time HAPANA.
 
Sawa mimi ni mediocrity
wewe umefanya nini cha maana huku duniani
Cha maana ni nini?

Kila mtu ana vitu vyake anavyoona vya maana hapa duniani na wengine hakuna cha maana kwao hapa duniani

Kuna watu hata uhai hauna maana kwao, wanataka wafe tu. Kifo ndio cha maana kwao.

Kwa hiyo "cha maana" depends upon your frame of reference.
 
Daaah hakika sisi weusi ni sawa na bure
 
Tanzania inakabiliwa na changamoto moja tu mfumo wa elimu ya juu haujakaa vizr coz watu wengi saivu wamesomea mambo ambayo hayapo kwenye maisha ya kweli na kama yapo basi ni kidogo sana kulinganisha na idadi ya watu walio somea kitu hicho.

Mfano; vyuo Vinavyo toa program za managers, supervisor, HRM vina idadi mubwa ya wanafunzi ukilinganisha na Vyuo vya ufundi.

Pia maeneo ya kuajiliwa ni machache sana kulinganisha na idadi ya wahitimu.

Fursa zipo na ideas juu ya maendeleo zipo ila wakuzisapot wapo bize kujenga shule.
 
Hata ungekuwa wewe usingeweza kuandamana. Ilishatokea madaktari wakaandamana ila mkuu wao, alitekwa na watu wasiojulikana na mpk leo hakuna kesi ya kutekwa. Ilikuwa kipindi cha Kikwete
Huweziacha kudai mfumo mzuri wa maisha yako na vizazi vyako kisa mwenzio katekwa ama kuuwawa. Hizi ni kauli za kioga , ujinga na umaskini na ndo tabia ya watanzania. Kudai mfumo bora ni vita na mnatakiwa kuwa na mbinu mbalimbali na si kukariri kuandamana tu.
 
Mbunge analipwa mafao kila baada ya miaka 5 na si 10.Hapo kwa walimu , hiyo 500k ni secondary lakini primary wanakula hadi 350k.
 

Hapo kwenye bold…

Hao viongozi wanatokana na sisi wananchi wenyewe, hawatoki kuzimu.

Kinachowajenga na kuwapa nguvu kuwa hivyo walivyo sasa ni jamii yetu. Wao ni zao letu, ni watu miongoni mwetu na matokeo ya mienendo ya jamii yetu.

Bado kuna jambo lipo linalosababisha hii tofauti kati yetu kuwepo.

Kama sisi tulikua bora zamani na hao wenzetu wameiga kwetu basi ni kwanini tunashindwa kurudi katika ubora wetu? Kikwazo haswa ni kipi?

Kwamba tumeshindwa kabisa hata kuanza upya basi? What really happened to us??

Hii hali ukiifikiria kwa umakini unaona kabisa it goes beyond colonialism.

Walitufanya nini mpaka tuko hapa leo hii na kila juhudi ya kunyanyuka tena inapotea kila ikichipua?
 
Dah nilitaka nilale muda huu, ila kwa hii comment imenipa challenge.. ngoja niendelee kukomaa ase.
 
Nakubali wao wanafanya kazi sana kwasababu hizo kazi pia wanazo. Hapa kwetu kazi hakuna tufanye nini?Watu wengi kila mahala unapopita masaa yote kwasababu kazi hakuna.

Mtuletee kazi tutafanya, Msituambie twende kulima, wengine tumezaliwa mijini hatujawahi kulima na hatuna mashamba.
 
Uko sahihi mia mia
Halafu wanajali sana muda na pia kwenye kazi na huduma ni wa KWELI hawana ubabaishaji.
 
Sasa huku kwetu watu kama TID na Ray kigosi kwa umri wao bado wanaishi na kula kwao,what do you expect?
 
Kazi zipo nyingi tu,ajira ndio hakuna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…