Uchaguzi 2020 Twende na Bernard Membe, tuunde Serikali ya kazi na bata! Naomba kura zenu

Yaliyomkuta mheshimiwa Membe ni yale yaliyo wakuta wakina Lowassa na Sumaye na bado yatawakuta wengi. Na haya siyo kwa CCM tu hata vyama vingine na mfano mzuri ni CDM na Dk. Slaa. Vyama vina katiba zake lakini hatuzifuati na kanuni zintelekezwa kwa kuangaliana usoni. Fikiria CCM wanatayarisha fomu moja tu ya mgombea, sisi wengine tunasherehekea na yeyote akiamsha kichwa anakatwa shingo. Mazoea hayo wenyewe wanaita utamaduni tunaupigia makofi hata kama unakosesha watu haki zao. Membe alikuwa huko akaona poa sasa safari hii kwawaza tofauti imekula kwao.
CDM waliruhusu gia kubadilishwa hewani wakamkaribisha Lowasa na kumpoteza Slaa. Wenyewe wanajigamba Lowasa kuongeza kura lakini mwisho wa yote Lowasa karudi CCM, hivyo hivyo Sumaye. Mpaka leo najiuliza Lowasa angeshinda angesimamia nini? Haiba yake haiendani na CDM. Angeshinda CDM sasa ingekuwa kitu tofauti kabisa. Nafikiri Lowasa alikuwa liability. Nafikiri kuwa CDM wamejifunza hawataokota tena reject za CCM au Chama kingine.
ACT wamenasa hapo hapo na sasa inabidi wavumiliane tu na Membe.
Tamaduni zinazokinzana na sheria ni nzuri lakini iko siku zitaleta kasheshe. Tamaduni za mwenyekiti kuja na majina mfukoni. Mzee Malecela aliambiwa amsaidie mwenyekitiikawa ndio njia ya kumtoa. Membe kaonesha nia tu ikawa shida. Kuna wenye viti wa maisha shida wanaibuka wakati wa uchaguzi tu.
Membe kavuna alichopanda CCM-alikuwa na sauti hakusema sasa inakula kwake. Mola atusaidie.
 
Hata hivyo karibu ungekuwa umejiunga jf mapema ungekuta ushapata lau 72% ya kura za urais

Karibu jf natumai utapata kura za akina Kawe Alumni na @Biayetu
Mie nimeshabookiwa✌️✌️✌️
 
Ahahahahaha.....Membe tena,Da walishamtupa lando waungwana.
Membe angeonekana bora iwapo angegombea CCM, kule angebebwa na system ambayo kwa miaka mingi imekuwa ni organ ya kutegemewa na Chama kuelekea chaguzi mbalimbali.
 
Nitakuchagua Mh.Membe😂😂😂😂😂 kura yangu unayo wewe ndio Mgombea pekee wa Urais umetambua uwepo wetu
 
Mzee wangu huku umekuja kujidhalilisha.Hahani kweli unataka ukagawe kura za Lissu Lindi?.

Umejidhalilisha sana.
 
Membe angeonekana bora iwapo angegombea CCM, kule angebebwa na system ambayo kwa miaka mingi imekuwa ni organ ya kutegemewa na Chama kuelekea chaguzi mbalimbali.
Hata angekuwa CCM huyu ndugu yetu hana mvuto wa kisiasa, ongea yake hata uenyekiti wa kijiji haumfai
 
huko tulishatoka kwasasa ni haki,uhuru na maendeleo ya watu Lisu ni yeye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…