Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alipokutana na Evander ambaye hatangazwi nini kilimkuta?Hakuna popote ulipo jibu, eti alikua anatangazwa , hao kina evanda walikua hawatangazwi ? Kwamba mapambano yaliyokua yanarushwa ni yake tu ? Kwenye vyombo vya habari anaandikwa yeye tu?
Na ni matangazo gani hayo yamefanya jina lake lidumu kwa miongo minne sasa ?
Habari za vijiwen ziache vijiweni , anejua anajua tu ambae hajui hajui full stop
Ni kama zile story za vijiwen, Ronaldo hamna kitu , hattrict zake anapigaga timu ndogo tu...
Mzee na wewe kaangalie makala youtube rudi na hoja za kupinga kilichoandikwa hapa.Si unajua tena wabongo wakiingia utube wakisoma vimakala viwili vitatu basi wanajifanya magwiji wa mambo. Mashirikisho ya ngumi duniani yanamtambua Tyson, halafu anatokea mtu kwa mtogore kashiba ugali na kabichi anijafinya mtaaalam kuliko WBO, WBC,IBF, shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania nk. Chambueni tu singeri ndio fani zetu hayo mengine tuyaache tu kama yalivyo
Kama ulikuwa ujazaliwa bora usiongeee uwongo. Nikimbuka pambala la Tyson vs Bruce Seldon. Siku ambayo 2Pac anapiga Risasi, wee acha tuuuu. Jamaaa alikuwa vizuri, Cocaine Ndio imemmalizaCus D'Amato alimuokota Tyson mtaani, aliona ubabe, aliona sharpness, aliona njaa, aliona vingi lakini cha muhimu zaidi ni aliona 'eye of the tiger'.
Akamchukua Tyson, akam-train, akapambana, kwa ubabe wa Tyson ulingoni akapachikwa jina la Kid Dynamite, kisha Iron halafu likaja Baddest man on the planet.
Ni kweli alistahili?
Ninasema hapana. Na hili ni jibu la wote ambao reference yao ya bondia mzuri ni Tyson.
Tyson alibebwa na journeymen, alibebwa na vikongwe, alibebwa na media, akabebwa na promoters ndiyo akafanikiwa kumilikia hizo nicknames tatu.
George Foreman baada ya kupigwa na Jimmy Young (Nalipenda hili pambano sichoki kuangalia) na kuokoka palepale ukumbini alistaafu na kuwa mchungaji. Baada ya kurudi tena ulingoni ndiyo zikawa enzi za Tyson zimepamba moto.
Sasa siku hiyo Tyson akiwa anahojiwa akaulizwa "Unafikiria kupambana na Foreman?" Akajifanya hajasikia swali, akaelezea swala jingine alipomaliza yule mwandishi akarudia tena "Unafikiria kupambana na Foreman?" Tyson akang'aka "KWANI NI LAZIMA NIPAMBANE NAE? NENDA KAPAMBANE NAYE WEWE BASI"
Huyo ndiye Tyson sasa. Muoga na anayeogopa kusimama ulingoni na bondia aliyekamilika.
Wanaomtetea wanakwambia alichukua ubingwa akiwa mtoto. Rekodi ambayo hakuna aliyeiweka, it's true. Alichukua ubingwa kutoka kwa Trevor Berbick mwaka 1986, Trevor Berbick alichukua ubingwa kutoka kwa Pinklon Thomas mwaka 1986 huo huo.
So Trevor Berbick ametoka kupambana na Pinklon Thomas, mkali wa left jab, pambano la raundi 12 na ushindi wake aliupata kwa uamuzi wa majaji, means alizunguka raundi zote 12 bila kuacha hata moja.
Na unataka jua kivipi pambano lilikua gumu? Hakuna aliyeanguka kwenye hili pambano mpaka Berbick anatangazwa bingwa.
So mtu wa miaka 32 ametoka kupigana pambano la heavyweight la raundi 12 unampa kijana wa miaka 22 ili apigane naye kutetea ubingwa. Unategemea nini? Ndiyo nikasema mapromoter pia wanambeba.
Tafuta siku hizi ni heavyweight gani anaingia ulingoni zaidi ya mara mbili tena kwa mapambano ya umuhimu. So Berbick risked it, iwe ni madeni au vitisho vya promoter hatujui, ila ni alipanda ulingoni kumpa ushindi Tyson.
Ok akampiga Michael Spinks (ndugu wa Leon) bondia aliyekua anatafuta pambano moja tu limstaafishe akiwa tajiri, akalipata baada ya pale na ngumi akaacha. This was not a completed boxer.
Akaenda kumpiga Holmes, again, babu mwingine alikutana na bahati mbaya ya kijana ulingoni.
So promoter na kocha wake wakawa wanavizia 'has been' na journeymen ili kuikuza rekodi ya Tyson, wakisaidiana na media.
And then 'has been' na journeymen wakaisha ikabidi apambane na mabondia wakali wa kizazi chake.
Alipigwa na kila bondia. Alipigwa na Evander akang'ata (kuliko kupigana ukang'ata sa si bora ukimbie - Chid Benz) alipigwa na Lenox Lewis,
Yeye na mapromota wake wakajichanganya wakamchagua Douglas Buster kama stepping stone kwa Tyson. Douglas akamchapa huyu bwana kwa KO raundi ya kumi. Ikawa aibu. Unajiita Iron mara Baddest how do you lose to underdog? You lose kwakua promoter hakutoa maelekezo kwa Douglas kua inabidi ashindwe so hata journeyman akimkazia Tyson, Iron linakua plastiki.
Anyway akaanza safari ya kutaka kurudisha mkanda toka kwa Douglas, bwana Douglas akaenda kuuacha mkanda kwa Evander, Tyson akapangiwa apigane na Evander ili arudishe mkanda wake. Bwana Tyson akaona isiwe kesi akalikimbia pambano.
Manina, akadai ati amepata jeraha la mbavu hivyo hawezi kuingia ulingoni na Evander. Plan yao ni atokee bondia mlaini amkalishe Evander kisha wao ndiyo wamkurupukie huyo bondia mlaini.
Akajichanganya akamvagaa Evander hivyo hivyo, kufika raundi ya 11 Tyson akabutuliwa kwa KO. Akajifanya anataka kurudiana naye, walivyorudiana akaona balaa limezidi akamng'ata Evander.
Akajichanganya akaenda kwa Lennox Lewis. Huyu anaye akamtoboa toboa Tyson hadi aibu.
Huyu sasa ndiyo Tyson. Ambaye watu wanamsifia huku hawajui kua jamaa alikua ni mwoga, mtegemea journeymen kama stepping stone na media.
Overrated nigga
Update:
Kuna watu wanadai sasa kwanini apigane na Foreman wakati Foreman alishajichokea. Lakini mbona hawajiulizi inakuwaje mtu huyu huyu akapigana na Holmes na Berbick ambao ni watu wa kizazi cha Foreman?
Wanadai eti anajulikana dunia nzima. Nimewajibu mbona uzi una majibu ya kwanini anajulikana? Si nimeandika Media zilitengeneza hype au?
Wanasema ni mkali yupo top 5 ya greatest heavyweight boxers. Ni kweli ila hiyo ni kwakua amepelekwa pale na rekodi ambazo kazivuna kwa journeymen na has been.
Yaani watu wanajenga hoja ambazo tayari uzi umejibu. Kwa mwingine anayetaka kujenga hoja tafadhali aangalie kama uzi umeshajibu swala analotaka kuleta.
Dah chief mbona sasa unakua hujajibu hoja za uzi.Kama ulikuwa ujazaliwa bora usiongeee uwongo. Nikimbuka pambano la Tyson vs Bruce Seldon. Siku ambayo 2Pac anapigwa Risasi, wee acha tuuuu. Jamaaa alikuwa vizuri, Cocaine Ndio imemmaliza.
Ila Wilder anapiga jamani, hata wa enzi hizo wangekaa tu ingawa style yake haivutii.Nini kinachofanya uoungue, kutokana pia hakuna wapiganaji wazuri kama zamani, tangu afe michael jackson poo kushney maregea sababu hakuna anaefanya kama yeye..
Hawa kina anthony joshua kina wilder ni kama kufa kwa waganga hadi walevi wanapunga watu majini, n ndio maana mayweather akateka vyombo vya habari mnoo sababu hakukuwa na mabondia wakali wa uzito wa juu.
Wilder ana ngumi nzito ila kwa mimi Evander alikua na uwezo wa kuvumilia kuliko mabondia wengi wa kipindi chake, yaani alikua anapigwa ngumi nzito mfululizo lakini jamaa alikua ngumu kukaa, kama utapata nafasi ingia u- tube uangalie alafu upime kama wilder angekua na kazi raisi kama anavyo hisi.Ila Wilder anapiga jamani, hata wa enzi hizo wangekaa tu ingawa style yake haivutii
Asante kunisaidia kumjibu, bado alitaka eti Tyson apigane na Alli, wakati Alli kastaafu 1981, Tyson anakuwa bingwa wa dunia 1986 akiwa kinda, angepigana na Alli lini?Mbona hueleweki mzee? Holmes mzee lakini hapo hapo unalalamika kwanini hakumuingia Foreman? Kwani Foreman kizazi chake? Angempiga pia Foreman ungesema hivyo hivyo kwamba kampiga mzee!
Overrated TKO, haaa haaa haaaaKwahiyo zile TKO zote zilikiwa sio za halali
Mkuu naomba unipe jina la kitabu na picha yke utojari...Ni hard copy. Ndiyo nakisoma wakati huu. Infact nakisoma tena mara ya pili.
Alikulia Mazingira magumu sana. Hana uhakika na baba yake. Akiwa na miaka sana alitumika kwenye wizi majumbani. Udogo wake ulitumika kupenya sehemu finyu.
Huyo mwenzako nimeijibu hiyo hoja yake kakimbia.Asante kunisaidia kumjibu, bado alitaka eti Tyson apigane na Alli, wakati Alli kastaafu 1981 , Tyson anakuwa bingwa wa dunia 1986 akiwa kinda, angepigana na Alli lini???
Yes, Evander pengine angeweza kuvumilia, but ni wangapi walikuwa kama Evander?Wilder ana ngumi nzito ila kwa mimi Evander alikua na uwezo wa kuvumilia kuliko mabondia wengi wa kipindi chake, yaani alikua anapigwa ngumi nzito mfululizo lakini jamaa alikua ngumu kukaa, kama utapata nafasi ingia u- tube uangalie alafu upime kama wilder angekua na kazi raisi kama anavyo hisi.
Hakuna kama Tyson?
Uzi na komenti 10 za kwanza umejibu hili swali.
Tawile baba tawile!Mi nililiona pambano live sikuhadithiwa
Hata nikikutajia haina faida maana kwako wewe kila aliepigwa na Mike ni mbovu nimtaje nani sasa?Wewe na wewe unaanza komedi. Kwahiyo losses zote za Tyson zimetoka kwa Evander? Hao mbwa aliowapiga mtaje aliyekua kwenye prime kama yeye
Sasa hata kama alipiga vibabu tumuite bora? Anyway mi mada ikishamaliza siku hatujaelewana hua siijadili tena.U bora wa bondia unapimwa kwa uwezo wake uwanjani.SIO KAPIGANA NA NANI.
HAUWEZI KUSEMA RONALDINHO HAKUWA BORA KISA HAJACHEZA EPL.
Sasa hata kama alipiga vibabu tumuite bora? Anyway mi mada ikishamaliza siku hatujaelewana hua siijadili tena.
Kesho nitaandika makala juu ya mapambano mawili ninayokumbuka ambayo ni bondia alitaka mtelezo kama ndugu Tyson.
Tukutane huko