TZ Trends & Analysis: Hoja 30 za The Economist Kumhusu President Samia. Kuna za Kweli, za Uongo na Uzushi na Kutaka Kumpangia Watakacho Mabeberu, Jee?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Salaam,

Kati ya eneo gumu sana kwenye tasnia ya habari ni eneo la uchambuzi wa habari, news analysis. Japo Tanzania tuna vyombo vingi vya habari, na waandishi wengi wa habari, ni vyombo vichache ndio vina waandishi wenye uwezo wa kufanya news analysis.

Kwenye print media ndio angalau wanajitahidi kwenye editorial, lakini kwenye electronics main stream media, ukiondoa TBC ile segment ya Shabani Kisu, na Jicho Letu Ndani ya Habari cha Star TV, chini ya Mkongwe Dotto Emmanuel Bulendu, naweza kusema, Tanzania hatuna any serious news analysis na news analysts.

Hivyo kufuatia uzoefu wangu kwenye media wa miaka 30, sasa baada ya kustaafu, naendelea kuwatumikia Watanzania kwa kujitolea, kila nipatapo muda, nitakuwa nawapatia kitu kinachoitwa trends & analysis za mambo mbalimbali kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Tukio la kifo cha ghafla cha Rais Magufuli, ni jambo ambalo halikuwahi kutokea, matokeo yake bado kuna trials na errors nyingi zitafanyika na serikali ya Samia hapa mwanzo mwanzo hadi itakapo stabilize, ambazo nyingine zitakwenda kinyume cha katiba, lakini kwa vile tukio hilo ni kama force majeure kwenye mikataba, tutavumiliana tuu.

Mfano kwa mujibu wa katiba, baada ya Ripoti ya CAG kukabidhiwa kwa rais, within the first 7 days, ilipaswa itue mezani kwa Spika. This is the most important report, katiba haikuweka mazingira yoyote ya ripoti hii kushindwa kuwasilishwa mezani kwa Spika within the prescribed time frame. Ila kiutu uzima tuu, ripoti hii ilibidi iwasilishwe jana saa 3 asubuhi. Very unfortunately jana hiyo Waziri wa Fedha alikuwa hajaapishwa hivyo hawawezi kuipokea. Natumaini itatinga Bungeni kati ya Jumanne na Alhamisi Ijayo.

Jingine ni ule waraka wa TLS kumtaka rais mpya Samia kulivunja Baraza la mawaziri la JPM na kuunda lake la Awamu ya Sita. Rais Samia kaamua kuanza Awamu yake ya 6, na mawaziri wachache wapya, na wengi ni mawaziri viporo wa Awamu ya Tano!, kwa hoja kuwa kile kiapo chao kwa utii kwa JPM, kinahuishwiwa kwake, kwa hoja kuwa kiapo ni kwa Taasisi ya Urais wa JMT na sio kwa mtu. Kwa maoni yangu, this is the first mistake ya rais Samia!, kwa executive appointees, hata rais akibadilika, wao wanaendelea, lakini kwa political appointees wote, hii ni serikali mpya ya awamu ya 6 na sio serikali ya muendelezo wa awamu ya 5!. Kiapo cha utii kwa Political appointees ni kiapo cha utii kwa rais aliye madarakani kwa awamu mpya, ndio maana hata Waziri Mkuu, hata kama ni yule yule, awamu ikibadilika, anateuliwa tena, anaidhinishwa tena na Bunge na kuapishwa upya!. Viapo vya utii kwa Political appointees ni non transferable!, JPM aliunda baraza lake, JPM kafa, Baraza lake lazima livunjwe ili Samia aanze na awamu mpya na Baraza jipya!. Hivyo ilibidi mawaziri wote wale kiapo kipya cha utii kwa Rais mpya Samia na sio kuhudumu kwa rais mpya kwa kiapo cha utii kwa rais aliyepita! JPM, ndio maana tukamshauri PM Majaliwa ange step down kumpa space Mama to start a fresh, na kama bado Samia anamuhitaji PM Majaliwa, ange m reappoint. Hivyo hii serikali ya Samia ya awamu ya 6, ni serikali ya awamu ya 6 ambayo pia ina muendelezo wa awamu ya 5!. Bila kulivunja Baraza la mawaziri la awamu ya 5, hii serikali ya Samia ni serikali ya awamu ya 5 ya 6!.

Hayo tuyaache yangu ya leo ni haya..
Baada ya kuisoma ile makala ya Jarida la Mabeberu la The Economist na hoja zake kumhusu Presidaa Samia, Nimekuja na hoja 30 kwa waliyoyasema kumhusu Samia. Kati ya hoja hizo, kuna za hoja za kweli, ni muhimu kutozipuuzia, kuna hoja za uongo na uzushi ni za kuzipuuza, lakini pia mabeberu hawa walivyo na akili, kuna hoja ambazo ni za kutaka kumpangia kazi kiana, rais wetu Mama Samia, ili afanye au atende kile mabeberu hawa wanacho kitaka!.

Nilisisitiza humu, kwa vile JPM hakupenda kupangiwa, na hatukumpangia, vivyo hivyo hata Samia, tusimpangie!, ila hakuna ubaya kumshauri na kumweleza jinsi mabeberu hawa wanavyo muona ni silaha muhimu sana ya kujiimarisha dhidi ya hila zozote za mabeberu hawa.

Ili uweze kulifaidi bandiko hili, anza na bandiko hili

Ukiona mabeberu wanaanza anza kuwasifu viongozi wazalendo wa bara la Afrika, ujue, wana lao jambo!.
Karibu kwenye hoja zangu...
Hitimisho.
Swali ni Jee President Samia, atakubali kupangiwa kazi na mabeberu?.
Jibu ni only time will tell.

Nawatakia Ijumaa Kuu Njema

Paskali
 
Summarization nacho ni kipaji..., hususan karne hii ya SMS na watu wapo buzy kama unaweza ukasema / ukafikisha ujumbe kwa maneno mawili usitumi manne... au andika long article alafu summarize kwa wanaotaka maelezo zaidi wayapate huko...
 
Summarization nacho ni kipaji..., hususan karne hii ya SMS na watu wapo buzy kama unaweza ukasema / ukafikisha ujumbe kwa maneno mawili usitumi manne... au andika long article alafu summarize kwa wanaotaka maelezo zaidi wayapate huko...
Hawezi maana amekopi kama ilivyo
 
Hapo kwenye executive appointees na political appointees ndipo penye patashika.

Kusema kwamba executive appointees hawatakiwi kuapa ila political appointees ndio wanatakiwa kuapa nachanganyikiwa kwasababu nijuavyo hata hao wasiotakiwa kuapa bado wanatoka chama kile kile ambapo walishaapa mwanzo wakiwa political appointees kabla ya kupewa majukumu mengine ya kiserikali.

Hapo nahitaji msaada wako kidogo.
 
Ndio maana magufuli alikua anaamua yeye mwenyewe aendeshaje nchi,ukisikiliza sana watu watakuendesha kila mtu anataka umtimizie hitaji lake na makala zao za ajabu ajabu.
Hakuna binadamu mwenye shukrani dunia hii na huwezi pendwa na watu wote
Siku si nyingi wataanza kumropokea na mama samia na kumpangia aongozaje nchi
Hii nchi inabidi iendeshwe kimagufuli magufuli ttu.Ndio itaenda vizuri
 
Ndio maana magufuli alikua anaamua yeye mwenyewe aendeshaje nchi,ukisikiliza sana watu watakuendesha kila mtu anataka umtimizie hitaji lake na makala zao za ajabu ajabu.
Hakuna binadamu mwenye shukrani dunia hii na huwezi pendwa na watu wote
Hakuna mtu anataka fulani apendwe (unless otherwise ni kwenye michakato ya kutafuta life partner) kinachoongelewa na inachobidi kitazamwe ni kama anafuata haki, utaratibu na sheria..., hayo mengine ni ziada....

Sasa cha kujiulize Bwana yule alifuata hayo..., na yaliyosemwa alisingiziwa au yalikuwa kweli (Kama mtu unazo akili za kusoma na macho ya kuangalia unasoma na una-draw your own conclusion sio usubiri upewe na conclusion) Sasa bwana yule kuzima midomo ya wasiokubaliana na yeye na kutumia hoja za nguvu na sio nguvu za hoja...., hapo nadhani alipwaya....
 
Kila utawala una strength na weakness yake. Hio ilikua weakness yake mlibidi mjue jinsi ya kwenda nae maisha yaende.
 
Hilo gazeti lilipigwa marufuku Tanzania wenzetu mnalipata wapi wakati serikali ilishalipiga pini marufuku Tanzania?

Mna quote toka gazeti lililopigwa marufuku?
 
Kila utawala una strength na weakness yake. Hio ilikua weakness yake mlibidi mjue jinsi ya kwenda nae maisha yaende.
Kwahio hao walioongea walikuwa wanaoongelea weakness zake au walikuwa wanatunga vitu ambavyo havipo...,

Na ndio maana binafsi ni vigumu kupinga / kulalamika kazi zake akiwa waziri, huenda hizo strength zake zilifaa akiwa mtendaji na sio kiongozi wa kuongoza na kuunganisha watu...., Mtu anaweza akawa bondia mzuri ila sababu ni mwanamichezo sio necessarily akawa mwanasoka mzuri pia...
 
Naona mzee wa makala ndefu umerudi tena kwa kasi baada ya kupigwa pin.

Sie tupo,karibu sana kwenye jukwaa letu huru ingawa sio tu zati eksitenti.
 
umeanza kujipendekeza na kwa mama samia? wewe uko kwenye black list ya hao watu, concentrate kwenye kazi zako mkuu, hakuna appointment utapata hata lusiku na lumwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…