Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Salaam,
Kati ya eneo gumu sana kwenye tasnia ya habari ni eneo la uchambuzi wa habari, news analysis. Japo Tanzania tuna vyombo vingi vya habari, na waandishi wengi wa habari, ni vyombo vichache ndio vina waandishi wenye uwezo wa kufanya news analysis.
Kwenye print media ndio angalau wanajitahidi kwenye editorial, lakini kwenye electronics main stream media, ukiondoa TBC ile segment ya Shabani Kisu, na Jicho Letu Ndani ya Habari cha Star TV, chini ya Mkongwe Dotto Emmanuel Bulendu, naweza kusema, Tanzania hatuna any serious news analysis na news analysts.
Hivyo kufuatia uzoefu wangu kwenye media wa miaka 30, sasa baada ya kustaafu, naendelea kuwatumikia Watanzania kwa kujitolea, kila nipatapo muda, nitakuwa nawapatia kitu kinachoitwa trends & analysis za mambo mbalimbali kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.
Tukio la kifo cha ghafla cha Rais Magufuli, ni jambo ambalo halikuwahi kutokea, matokeo yake bado kuna trials na errors nyingi zitafanyika na serikali ya Samia hapa mwanzo mwanzo hadi itakapo stabilize, ambazo nyingine zitakwenda kinyume cha katiba, lakini kwa vile tukio hilo ni kama force majeure kwenye mikataba, tutavumiliana tuu.
Mfano kwa mujibu wa katiba, baada ya Ripoti ya CAG kukabidhiwa kwa rais, within the first 7 days, ilipaswa itue mezani kwa Spika. This is the most important report, katiba haikuweka mazingira yoyote ya ripoti hii kushindwa kuwasilishwa mezani kwa Spika within the prescribed time frame. Ila kiutu uzima tuu, ripoti hii ilibidi iwasilishwe jana saa 3 asubuhi. Very unfortunately jana hiyo Waziri wa Fedha alikuwa hajaapishwa hivyo hawawezi kuipokea. Natumaini itatinga Bungeni kati ya Jumanne na Alhamisi Ijayo.
Jingine ni ule waraka wa TLS kumtaka rais mpya Samia kulivunja Baraza la mawaziri la JPM na kuunda lake la Awamu ya Sita. Rais Samia kaamua kuanza Awamu yake ya 6, na mawaziri wachache wapya, na wengi ni mawaziri viporo wa Awamu ya Tano!, kwa hoja kuwa kile kiapo chao kwa utii kwa JPM, kinahuishwiwa kwake, kwa hoja kuwa kiapo ni kwa Taasisi ya Urais wa JMT na sio kwa mtu. Kwa maoni yangu, this is the first mistake ya rais Samia!, kwa executive appointees, hata rais akibadilika, wao wanaendelea, lakini kwa political appointees wote, hii ni serikali mpya ya awamu ya 6 na sio serikali ya muendelezo wa awamu ya 5!. Kiapo cha utii kwa Political appointees ni kiapo cha utii kwa rais aliye madarakani kwa awamu mpya, ndio maana hata Waziri Mkuu, hata kama ni yule yule, awamu ikibadilika, anateuliwa tena, anaidhinishwa tena na Bunge na kuapishwa upya!. Viapo vya utii kwa Political appointees ni non transferable!, JPM aliunda baraza lake, JPM kafa, Baraza lake lazima livunjwe ili Samia aanze na awamu mpya na Baraza jipya!. Hivyo ilibidi mawaziri wote wale kiapo kipya cha utii kwa Rais mpya Samia na sio kuhudumu kwa rais mpya kwa kiapo cha utii kwa rais aliyepita! JPM, ndio maana tukamshauri PM Majaliwa ange step down kumpa space Mama to start a fresh, na kama bado Samia anamuhitaji PM Majaliwa, ange m reappoint. Hivyo hii serikali ya Samia ya awamu ya 6, ni serikali ya awamu ya 6 ambayo pia ina muendelezo wa awamu ya 5!. Bila kulivunja Baraza la mawaziri la awamu ya 5, hii serikali ya Samia ni serikali ya awamu ya 5 ya 6!.
Hayo tuyaache yangu ya leo ni haya..
Baada ya kuisoma ile makala ya Jarida la Mabeberu la The Economist na hoja zake kumhusu Presidaa Samia, Nimekuja na hoja 30 kwa waliyoyasema kumhusu Samia. Kati ya hoja hizo, kuna za hoja za kweli, ni muhimu kutozipuuzia, kuna hoja za uongo na uzushi ni za kuzipuuza, lakini pia mabeberu hawa walivyo na akili, kuna hoja ambazo ni za kutaka kumpangia kazi kiana, rais wetu Mama Samia, ili afanye au atende kile mabeberu hawa wanacho kitaka!.
Nilisisitiza humu, kwa vile JPM hakupenda kupangiwa, na hatukumpangia, vivyo hivyo hata Samia, tusimpangie!, ila hakuna ubaya kumshauri na kumweleza jinsi mabeberu hawa wanavyo muona ni silaha muhimu sana ya kujiimarisha dhidi ya hila zozote za mabeberu hawa.
Ili uweze kulifaidi bandiko hili, anza na bandiko hili
www.jamiiforums.com
Ukiona mabeberu wanaanza anza kuwasifu viongozi wazalendo wa bara la Afrika, ujue, wana lao jambo!.
Karibu kwenye hoja zangu...
Swali ni Jee President Samia, atakubali kupangiwa kazi na mabeberu?.
Jibu ni only time will tell.
Nawatakia Ijumaa Kuu Njema
Paskali

Samia tumaini jipya Tanzania: The Economist baada ya kumsakama sana Magufuli, sasa angalau lina matumaini na Samia, laanza naye vizuri
Wanabodi, Kwa vile hili ndio bandiko langu la kwanza kwa mwaka huu, kwanza tutakiane heri ya mwaka mpya. Pili tupeana pole sana kwa msiba mkubwa wa kumpoteza JPM. Tatu, nitoe pongezi kwa President Samia kuwa rais wa JMT, kuongoza awamu ya Sita, hongera sana Mama Samia, umeanza vizuri kwa...
Ukiona mabeberu wanaanza anza kuwasifu viongozi wazalendo wa bara la Afrika, ujue, wana lao jambo!.
Karibu kwenye hoja zangu...
-
- Hoping for change, Tanzania’s new president surely can’t be worse than the old one.-Hapa wanamsema JPM was worse president, hivyo sasa wana matumaini na Samia. Jee ni kweli JPM was worse president?.
- Tanzania’s new president, Samia Suluhu Hassan, vows to continue where her predecessor left off. –This is true.
- Pity the country if she keeps her promise. Hapa wanatuonea huruma kama atafuata nyayo za JPM. Jee ni kweli, Taifa la Tanzania, linahitaji kusikitikiwa iwapo Samia atafuata nyayo za JPM?.
- John Magufuli, was a covid-denying populist who ran a ruthless authoritarian regime. Jee ni kweli JPM run a ruthless authoritarian regime in Tanzania?.
- Many believe that the virus killed him. Hapa wana suggest JPM kaondolewa na covid!. Huu sio uongo?. Hao many who believes that ni wepi, wa wapi?!. Ili kuipush hii agenda ya covid, hawakuitangaza sababu ya kifo cha JPM iliyotangazwa na serikali yetu. Kumsingizia marehemu amekufa kwa kitu kingine chochote, zaidi ya kilichotangazwa rasmi ni kosa la consecration of the dead!, ni kutaka kumchafua marehemu na kuichafua nchi yetu kuwa watu wanakufa kwa covid, wakati reality wanakufa kwa magonjwa mengine!.
- For the moment liberal Tanzanians are surprisingly upbeat, in part because they do not take Ms Samia, the country’s first female leader, at her word.-Huu ni uongo!.
- She is a product of the ruling party, which has held power in different guises since independence from Britain in 1961. Hapa wanasema CCM inatawala toka uhuru kwa hadaa!-Huu pia ni uongo!.
- But she is no insider. She comes from the semi-autonomous archipelago of Zanzibar, not the Tanganyika mainland, which is the hub of power.-Huu ni uongo!. Samia ni CCM insider!, ila hana makundi!.
- Ms Samia was Mr Magufuli’s vice-president, but it is rumoured that she was foisted on him by CCM bigwigs. Hii sina uhakika, yaani JPM alilazimishwa kumchukua Samia na hao waitwao CCM bigwigs!.
- Foremost among these was Jakaya Kikwete, Tanzania’s president from 2005 to 2015, who is said to have admired her competent efficiency. –Hapa wamemsifu Samia ni efficient
- Mr Magufuli valued it less and she was excluded from his inner circle. Wanadai JPM hakumthamini Samia na hakuwa miongoni mwa watu wake wa karibu!. Huu ni uongo!.
- That is now seen as a reason for hope—as are the flashes of principle she has shown. Hapa wamemsifu Samia kuwa ni mtu wa principles na hapa ndipo matumaini na Samia yalipo lalia.
- In 2017, for example, she defied a presidential directive by visiting Tundu Lissu, a prominent opposition mp, as he recovered from being shot 16 times.Huu ni uongo!. JPM aliwa kuissue any directive Lissu asitembelewe?!, halafu eti Samia alimpuuza JPM akamtembelea Lissu kwa jeuri yake tuu!.
- Still, few are expecting a radical departure from her predecessor’s policies. –Hili lets wait and see, ila Samia tayari ameanza vizuri!.
- Not yet, anyway. Lacking a base within the party, Ms Samia will be concentrating on surviving the early stages of her presidency (inherited in accordance with the constitution), when she will be weakest. Huu ni uongo!. Wanadai Samia hana mimizi na Chama hivyo siku za mwanzo atakuwa dhaifu!. Kwenye hili tayari Samia has proved them wrong!, she is very strong woman!. Ile kuanza na kuanza, ameanza kwa kumgoa Dr. Bashiru pale Ikulu na kumtupia Bungeni as nobody!. Mtu alikuwa KM wa chama chake, then CS, alafu unamgoa na hata uwaziri hakustahili?!. It takes a very very strong man to do this!, sasa kama aliyefanya hili is a woman, then she is dam strong woman!. (Tanzania tutashuhudia “strength of a woman” (emphasize mine)
- Mr Magufuli’s faction still holds dominant positions in the cabinet and the party. (that was then, hii topic imekuwa overtaken by events)
- She is not totally helpless, however. She may not have a base of her own, but she does have potential allies. –Hapa wanasema Samia is helpless, ila atasaidiwa na wanaomuunga mkono ndio anawategemea!- Hapa pia they are wrong!. Wame mu under estimates Samia!. (Samia is a woman with streghth of a woman).
- With the support of Mr Kikwete’s previously sidelined faction, she was able to resist pressure to appoint Bashiru Ally, a Magufuli acolyte, as her deputy. Haya ni yale mauongo ya Twittwer!. Eti kulikuwa na pressure Dr. Bashiru ndio awe VP!. Eti kundi la JK waliokuwa sidelined na JPM ndio wamemsaidia Samia!.
- Instead she tapped Philip Mpango, the finance minister, pleasing international donors. – Huu pia uongo, ati chaguo la Dr. Mpango as VP ni ili to please mabeberu waitwao international donors!. Sababu za why Dr. Mpango, Samia amezitaja na sio hizo!.
- Still, she will have to avoid becoming too reliant on Mr Kikwete. –Hapa pia ni waongo!. Eti Samia anamtegemea sana JK kusimama!. Samia amethibitisha kwa kauli, maneno na matendo kuwa anasimama yeye kama yeye!.
- While foreign investors, often the butt of Mr Magufuli’s nativist policies, would welcome a return to the easy-going pro-market internationalism that marked the Kikwete years, many Tanzanians remember it as an era when corrupt patronage networks flourished. –Hapa mabeberu wanalaani sera za JPM za kutanguliza maslahi ya taifa kwa kuziita “nativist policies”, sasa wana matumaini kuwa Tanzania will return to the easy-going pro-market internationalism, kama cha JK ambapo rushwa na ufisadi vilitamalaki.
- Kikwete factions “smell blood and sense a comeback”, says Thabit Jacob of Roskilde University. It would be sensible to look to the former president for cover rather than guidance.-Hii pia sio kweli!.
- Ms Samia’s first challenge will be to reverse one of the most self-defeating coronavirus policies in the world. –Hapa ni kuichafua nchi yetu!. Jee kweli msimamo wa JPM on Corona ndio “self-defeating coronavirus policies in the world”.
- Mr Magufuli responded to the pandemic with a blend of quackery and denialism. –hii ni kweli
- Turning his back on science, despite having a phd in chemistry, he prescribed God, communion wafers and steam baths as prophylaxes. Hii ni kweli
- Unsurprisingly, the virus spread unchecked through the population. –Huu ni uongo wa kutaka kuichafua nchi yetu, etu kusema Corona imeenea sana Tanzania!.
- A more sensible approach is desperately needed. Hapa wanataka kutuingilia kwa kudai hatua za JPM ku deal na Corona sio sensible, sasa hatua sensible zinatakiwa kuchukuliwa kwa haraka.
- Diplomats and the World Health Organisation hope the new president will again start publishing official data on the virus (after a year-long pause), sack the anti-vaxxer health minister and sign Tanzania up to the covax vaccine-sharing programme. –Hapa wanataka kumpangia kazi Samia, walitaka Waziri wa Afya, atimuliwe, wanamuita anti-vaxxer, wakitumai President Samia sasa atakumbatia chanjo ya corona.
- Continuing to deny Tanzanians the jab would stain her reputation from the outset. –Hapa wanatutisha, eti Tanzania kuendelea kugomea chanjo ya Corona, kutapelekea sisi kutengwa na jumuiya ya kimataifa.
- Whether Ms Samia is for making such changes remains to be seen. In her first public appearances as president, she did not deign to wear a mask. –Hapa wana mashaka kama Samia ataleta mabadiliko tarajiwa kwenye vita vya Corona kwasababu hajaonekana kuvaa barakoa.
Swali ni Jee President Samia, atakubali kupangiwa kazi na mabeberu?.
Jibu ni only time will tell.
Nawatakia Ijumaa Kuu Njema
Paskali