Leo nimkutana na hiki kisa mshikaji analalamika: Mwanao anakupigia simu ana shida ya HELA anakwambia nitaregesha baada ya siku mbili, kimoyomoyo unasema ngoja nimpe tu mwanangu asovu mambo yake wala hakuna haja ya kunirudishia.
Ghafla baada ya siku mbili unampigia mwanao simu kapiga BLOKU afu ww ulitaka kumsalimia tu yy alijua utamdai Hela yako.
Life have got a lot of surprises.
Ilinikumbusha mwanangu Minja aliomba mkopo wa 500k tu ambao angerejesha ndani ya wiki moja ili asolve kipengele cha chap na aliyekuja kuchukua hizo pesa ni mchumba wake , ili kulinda heshima ya mwana nilimwambia shemeji ile pesa ninayompatia mshikaji alikuwa ameniazima siku za nyuma hivyo ninarejesha, ghafla wiki ikawa mwezi ikawa miezi mitatu, mara mwana hapokei kabisa simu, sms hajibu eventually akaniblock , kilichonisikitisha ni kwamba mwana uwezo wa kulipa hizo hela alikuwa nao na nilikuwa nashuhudia bata analokula, na kwasababu tuko na kazi ya aina moja na social life ninafaham uwezo wa kulipa alikuwa nao. Ilibidi eventually baada ya mwaka nimshirikishe uhalisia wote mchumba wake huyo aliyekuja kuchukua hizo pesa kwangu. Yule dada alisikitika sanaaa, to the extent alilia, masaa machache baadaye mwana alinipigia simu kwa aibu akiomba misamaha kibao .kesho yake alituma pesa yangu pasipo hata ya kutolea 😅. Urafiki uliyumba sanaa sio washikaji tena kama zamani.
Nini huwa kinawapa watu ugumu kurejesha mikopo hata pale wanapokuwa na uwezo wa kufanya hivyo?