Uamuzi wa kuwaondoa Machinga mitaa ya Dar es Salaam urejewe upya

Dah!....uko vizuri sana kwenye kujenga hoja, hongera sana.

Andiko lako linaonyesha wewe ni msomi mkubwa.

Unafanya tafiti nini kuhusu umachinga?
 
Tunafahamu kuwa wamachinga Wana haki zao kama watanzania, lakini tunafahamu pia kuwa waenda kwa miguu Wana haki zao kulindwa. Uhuru wako unakoma pale unapoanza uhuru wa wengine. Wamachinga hawatoi fidia kwa mtu aliyegongwa na chombo Cha mto kwa kutembea kwenye barabara za magari.

Hatuwezi kujiuliza maswali mengiii kama mbegu za papai ili kuwaondoa wavamizi wa maeneo, waliovunja sheria. Hata kupewa maeneo ni hisani TU.

Tunafahamu kuwa wapo wachinga walioletwa mjini na watu wenye kazi zao, hawa ndio watakaopiga kelele nyingi kwa niaba ya machinga, lakini ukweli ni kwamba sio machinga ila wanajificha kwenye mgongo wa machinga.
 
Kupanga ni kuchagua na kutekeleza ni kuamua. Machinga wa Ethiopia wanakimbia nchi yao (EAC ndiyo route yao kwenda Kusini mwa Afrika), ni kioo cha kujitazamia hicho. Ila mawazo yako super!
 
Kupanga ni kuchagua na kutekeleza ni kuamua. Machinga wa Ethiopia wanakimbia nchi yao (EAC ndiyo route yao kwenda Kusini mwa Afrika), ni kioo cha kujitazamia hicho. Ila mawazo yako super!
Nchi yetu Ina bahati sana kuwa ni kubwa sana kuliko idadi ya watu. Yako mapori ambayo hajawahi kukanyaga binadamu. Na bahati mbaya hakuna mtanzania ambae familia yake imekosa ardhi. Machinga wooote kabisa Wana kwao ana huko kwao wanayo ardhi kubwa sana ambayo wameiacha bila matumizi.

Machinga hawa wamekuwa machinga kwasababu TU serikali yetu inafahamu kuwa wananchi wameichoka hivyo wanatumia ujanjaujanja kubakia madarakani, ikiwemo hii ya kuwaacha machinga wafanyekazi kiholela kama hivi wakidhani kuwa ni suluhisho, lakini Sasa tatizo linaanza kuwa kubwa sana kuliko walivyotarajia.

Hata hivyo, it is never too late to do the right thing. Tufanye Leo sio kesho. Kama Leo ni ghali basi itakuwa ghali zaidi kesho.
 
Nimesoma response yako ni nzuri na maswali mengi fikirishi ambayo yanahitaji a good research to come up with good way forward ambao unaweza kupelekea hata kutunga sheria mpya. Machinga walianza kama marching guys watembeza bidhaa mitaani. Wakaongezeka mara wakaanza vibanda vidogo vidogo mara wakaenda kila mahali. Hili lilipaswa kutazamwa kwa undani why do we have these people loitering along our streets. Chanzo cha hawa watu ni nini? Tunakitawala vipi, Elimu, ajira, umaskini, au? Wanapata wapi bidhaa wanazoziuza, je mitaji yao au ni mali za wengine n.k. kwa sasa hatuna tena huo wasaa wa kujiuliza bali ni kuokoa uchumi kwa kuwaondoa na kuwapa maeneo mbadala.
 
Umenena vema kabisa mkuu, lakini kama Kuna kosa serikali inataka kufanya tena ni kuahidi kuwa itaratibu na kuwapatia maeneo machinga wote kabisa hapa mjini. Wamachinga waliopo Sasa ni wengi, wanakuja wengine na wanazaana. Hivyo guarantee ya kuwapatia maeneo wote siioni. Kinachotakiwa ni kanuni za kufanya biashara na mipangomiji zifuatwe kama zilivyo kwa 100%.

Leo hii unakuta bia na vileo/ glossary ziko kila mahali, nchi nzima na maeneo yote yanauzwa bia na pombe nyingine hata kwenye maduka ya hardware. Huu ni uzembe mkubwa sana wa serikali. Mtu ana leseni ya bidhaa nyingine lakini anauza na bidhaa nyingine, na hiyo ni kupambana na umaskini au siasa za bei rahisi TU? Je, wale wenye leseni za kuuza bidhaa hizo kama pombe unawatendea haki?
 
Great Mkuu!
Ulielewa presentation ya research report yangu vzr. Kuongezea kwenye points zako mahiri hizo, ni kuwa tunahitaji Machinga Marshal Plan ya kitaifa to address the problem once and for all.
 
Rais Samia hashauriwi vyema,

anatengeneza kundi kubwa sana la wapinzani nchini,

watu hao wakiachwa bila njia za kujipatia kipato wataichukia serikali yake.

Ni kweli tunahitaji miji misafi ila raia nao wanatakiwa kuwa huru kufanya shughuli zao.

CCM itapata wakati mgumu sana kujinadi 2025 kama hali hii ikiendelea.
 
Great Mkuu!
Ulielewa presentation ya research report yangu vzr. Kuongezea kwenye points zako mahiri hizo, ni kuwa tunahitaji Machinga Marshal Plan ya kitaifa to address the problem once and for all.
Nilipata fursa ya kuishi marekani vijijini, wengi wetu tunaokwenda Marekani wanakwenda kuishi mijini, lakini mimi nimeishi kule vijijini kabisa kama Chelsea na kijijini zaidi ambako watu wanajikamulia wenyewe juice za apple na kuweka kwenye galoni na kuuza kiholela tu.

Ukweli ni kwamba hata Marekani wako machinga wengi sana, lakini hawa wako hukohuko vijijini. Watu kutoka mijini siku za weekeend na public holiday utaona misululu ya magari kuelekea huko vijijini kununua bidhaadh
Great Mkuu!
Ulielewa presentation ya research report yangu vzr. Kuongezea kwenye points zako mahiri hizo, ni kuwa tunahitaji Machinga Marshal Plan ya kitaifa to address the problem once and for all.
Ok, Sir pamoja sana.

Mimi nimewahi kuishi Marekani mjini na vijijini pia. Nimeishi kwenye vijiji hasa kama Chelsea na vingine ambako wajasikiamali wadogo wanauza bidhaa zao hukohuko vijijini. Wanajikamulia wenyewe apple zao kupata juice wanazouza kwenye galoni kiholela TU kwa bei ndogo. Wamachinga kule vijijini wanauza bidhaa zenye bei nafuu sana kuliko mjini, bidhaa zao zimeondolewa Kodi mbalimbali hivyo ni rahisi sana kuliko kule mjini. Hivyo, kila weekends na public holidays utaona misululu mirefu ya magari kutoka mijini kwenda vijijini kufuata bidhaa za bei nafuu kuliko kwenye Malls.

Hivyo serikali inaweza kuondoa Kodi fulanifulani kwenye bidhaa zinazouzwa na machinga walioko kule Mlandizi, Mkuranga, kisarawe na bagamoyo ili machinga wavutike kwenda kule na wakazi wa mjini kuvutika kwenda kufanya manunuzi kule ya bei nafuu.

Mfano, kama bei ya seti ya sufuria inayouzwa laki 3 kariakoo itauzwa laki 2 kule Kisarawe kwenye maduka ya machinga watu wengi sana watakwwnda Kisarawe kununua sufuria hizo badala ya kariakoo. Tunahitaji sera na sio kutumia nguvu zaidi.

Kule Marekani bei ya bidhaa inapungua bei kutokana na mambo yafuatayo:

1. Ubora wa bidhaa
2. Umbali kutoka mjini
3. Aina ya bidhaa
4. Parking, kama sehemu haina parking na bei ya bidhaa hapo itakuwa ndogo.
5. Public transport, kama hakuna usafiri wa umma na bei iya bidhaa husika inaweza kushuka pia.

Shida yetu sisi hapa bidhaa ni rahisi mijini kuliko vijijini, bei inaongezeka kadiri mtu anavyotoka city center. Hivyo kuvuta watu kuja kariakoo kufanya biashara na kununua. Inawezekana huku kariakoo yakaweko maduka ya jumla TU basi.
 
Hapo kwenye 'huru'

Sio huru

Ni wanatakiwa kufuata taratibu na sheria ambazo kila mtanzania anafuata
 
Mbona hujaziandika hizo hasara?
 
Big up Mkuu
 
Nchi yetu inatakiwa ihakikishe vijana wanafanya kazi kwenye sekta za uzalishaji na huduma zenye tija kubwa siko kuwa wachuuzi wa bidhaa hafifu za Kichina
 
Wewe Kipato cha kati hujui tabu ya mtu asiye hata na buku la kumpa uhakika wa mlo wa kesho.
Kwanini mtu akose buko wakati Tanzania Kuna uhaba wa Mayai, kuku, nyama ya mbuzi, mihogo, machungwa, nyanya, mafenesi, malimao, pilipili, samaki, alizeti, maharagwe, nk? Bado uhitqji ni mkubwa kuliko uzalishaji. Tutiane moyo tufanye kazi za uhakika hadi hapo rasilimali zetu zitakapokuwa zimeisha.
 
Hii sio kweli, Kuna kijana niliwahi kumshauri arudi mkoani na kuachana na kazi ya kuuza urembo kwa njia ya kutembezea wateja kwenye kapu, alinichukia sana lakini akarudi mkoani na kuanza kazi ya kufuga kuku wa kienyeji na kulima pilipili. Sasa hivi Yuko mbali sana, ana zaidi ya kuku 1000, Bata 200 na mbuzi 100. Anauza kuku na Mayai ya kuku wa kiejeji anapata hela hata kumzidi mtu aliyeajiliwa kwa mtu, amejenga na amepanua shamba lake kwa kulima kwa Trekta. Leo hii ni rafiki yangu na ananisifu kila siku.

Vijana hawa machinga kwa kuishi hapa mjini wamepata exposure kubwa sana, wanafahamu kitu gani kinatakiwa mjini, hivyo ukiwatimua hapa na kurudi kijijini watafanya vitu vya maana sana vya kimaendeleo. Unachosema wewe ni kinyume chale.

Mfano, sisi tulikulia mjini kwenye nyumba ya serikali ambako baba alikuwa akifanyakazi, nyumba ilikuwa Ina fanicha zote, maji na umeme wa bure. Siku baba alipotuambia tunahamia nyumbani kwetu huko salasala tulimchukia sana kwa kututoa kwenye mtaa na nyumba tuliozoea. Lakini hivi Sasa tunamsifu kwa kufanya uwamuzi ule badala angesubiri kustaafu au tuondolewe baada ya baba kuacha kazi. Tulipohamia kule tukajikuta tuko kwenye nyumba yenye nafasi hata ya kucheza na kulala. Badala ya kumchukia tukamuona shujaa.

Hata machinga ukiwatimua kwenye njia za waenda kwa miguu na chini ya nyaya za umeme Leo lazima kesho watakusifu TU kwa kuwaondolea mateso na hatari.
 
Mkuu, ukizungumzia masuala ya kilimo na ufugaji hakuna Kijana atakayekuelewa. Wewe leta story za kubet na kushinda milioni kadhaa utaona watakavyomiminika.
Uko sahihi. Sijui kama viongozi huwa wanatafakari kuona kijana mwenye nguvu za kutunza shamba au mifugo kwa faida anatembeza saa na handkerchief kutoka china. Kikubwa Barabara zijengwe maeneo ya mashambani vijana wajiajiri kwenye kilimo na mifugo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…