Uamuzi wa Russia kuivamia Ukraine ni mbinu iliyoshindwa (Strategic Failure)?

Uamuzi wa Russia kuivamia Ukraine ni mbinu iliyoshindwa (Strategic Failure)?

Nikionacho mimi.hata ikitokea russia akashinda vita tayari nchi kama marekani na washirika wake wamefanikiwa kumpima nguvu na wameishajiridhisha kwamba akilianzisha anapigika kirahisi.

Mfano angalia warusi wanavyokufa,ukraine huku wakisaidiwa na mizinga ya masafa marefu kutokea urusi ndani
ambayo ukraine hana.
NATO na marekani walimnyima silaha za masafa marefu,kitu ambacho angekuwa nazo si ajabu sasa hivi wangekuwa ndani ya urusi.
Hivyo maamuzi ya putin kuvamia ukraine na hasara kwake badala ya faida.
Na ni fundisho kwetu .usimdharau jirani yako kwa sababu ya mwonekano,anawezakuwa na marafiki wenye nguvu kuliko zako ukaumbuka.
Hili la Ukraine kunyimwa silaha nzito na za masafa marefu hawaliongelei Pro Russia. Wamebaki na wimbo wa NATO NATO.
Ukraine angepewa silaha anazotumia NATO (NATO arsenals) mpaka sasa kusingekuwa na Vita.
 
Mwenyewe umeona una point za nguvu 🤣🤣🤣🤣 Mleta uzi una tatizo la kukariri mambo.

Sababu y Russia kuitandika Ukraine ni nyingi sana lakini media za mgharibi hazisemi ukweri badala yake mmekaririshwa sbabu moja tu eti

Kuhusu Finland na Sweden kujiunga NATO, Russia walishasema hawana tatizo na hilo ila ita react iwapo mifumo na zana za kijeshi a NATO zikipelekwa Finland. Na kumbuka Russia akitoa ahadi huwa hatanii na ninakuahidi iwapo haya aliyoyaonya yakitokea, Finland itashambuliwa na joka la kibisa NATO hawataweza kufanya kitu chochote kile
Haya,
1. tueleze sababu unazozijua wewe za Russia kuivamia Ukraine.

2. Mbona Lithuania pale kuna NATO military base na kuna wanajeshi wa NATO zaidi ya 1,600 ulishawahi kusikia Russia karusha hata bomu la mkono ndani ya Lithuania au Estonia?

3. Romania na Poland kuna NATO military bases, uliwahi kusikia Russia karusha missile yake pale

4. Usichokijua ni kwamba NATO iko kwenye preparation ya kuweka military Base Finland.
 
1. Unataka nikupe takwimu za Ujerumani kiuchumi ila wewe huna sehemu uliyokuja na takwimu zaidi ya bla bla tu.
Unazitaka kwa base ya mwaka gani au ndani ya accounting period ya mwaka huu?

2. Eti USA hujataja economic indicator[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wakati fuel price imepanda hali ambayo inasababisha whole production sector kuwa na gharama zaidi.

Swali lako lilitakiwa lijikite kuonyesha nimetumia base year ipi na kulinganisha na ipi?

3.unaelewa hata nilichokielezea pale imeanza kucrumble au ni maamuma tu upo Dunia hujui la mbele Wala la nyuma.
Kwa hiyo hizi ndo takwimu. Tumesema lete takwimu siyo porojo. Mnarukaruka tu kama kende kwenye suluali. Porojo kibao lakini vichwani mko watupu
 
Hii thread ilikuwa posted long ago, naona imekuwa reposited
 
Haya,
1. tueleze sababu unazozijua wewe za Russia kuivamia Ukraine.

2. Mbona Lithuania pale kuna NATO military base, ulishawahi kusikia Russia karusha hata bomu la mkono ndani ya Lithuania?

3. Usichokijua ni kwamba NATO iko kwenye preparation ya kuweka military Base Finland.
Iithuania nayo ni nchi? NATO mtapata tabu sana kwani ubavu wa kupambana n Russia hamna. Challenge tumewapa hapo Ukraine

Na kubwa lenu linakwenda kuangushwa ki strategy na likitu linaitwa BRICKS. 🤣🤣🤣Putini ni mwamba, ukicheza naye unacheza na moto
 
Hapa ndo umeleta takwimu za tulichokuuliza. Naona unajitekenya na kujamba mwenyewe.

Hebu tueleze maana ya BRICKS kama ukivyoandika na sisi tuelewe
 
Urusi mpaka Sasa ameweza kuiangusha dollar.

Urusi mpaka Sasa ameigaragaza NATO.

Ukumbuke Hii SMO Urusi akishinda, NATO imekufa,Sweden na Finland malengo Yao yameshatibuliwa.View attachment 2645284
Nato wameshindwa kwa kutuonesha huo mchoro wako tu? Finland malengo yake yametimia tayari yuko Nato huyo Sweden mwenyewe ni Turkey tu ndio analeta kauzibe.
 
Mleta uzi ameleta swali na bado akajijibu mwenyewe na anapambana na wanaopinga majibu yake!
 
Before Russia invaded Ukraine, projections estimated global economic growth in 2022 would be around 5 percent. The war in Ukraine was a “massive and historic energy shock” to the markets, according to a November 2022 report by the OECD. The “shock” of the war was one of the main factors that had slowed economic growth in 2022 to just 3.1 percent, and why the OECD projected it to slow to 2.2 percent in 2023. The war, the report found, has had the greatest impact on Europe's economy, where growth in 2023 is projected to be just 0.3 percent
 
Sawa, tupe na wewe majibu ya maswali yetu yote tuliyouliza. Au maswali huyaoni
Majibu umeshatoa,sasa unataka ujibiwe kipi?Na kila anayekujibu tofauti na unavyopenda inakuwa kesi!
Mimi nimeanza na kukupa anguko la uchumi duniani na hasa Europe kutokana na vita!
 
Before Russia invaded Ukraine, projections estimated global economic growth in 2022 would be around 5 percent. The war in Ukraine was a “massive and historic energy shock” to the markets, according to a November 2022 report by the OECD. The “shock” of the war was one of the main factors that had slowed economic growth in 2022 to just 3.1 percent, and why the OECD projected it to slow to 2.2 percent in 2023. The war, the report found, has had the greatest impact on Europe's economy, where growth in 2023 is projected to be just 0.3 percent
1. Nakubaliana na wewe kuwa vita ya Russia na Ukraine imeleta madhara kwenye maeneo mengi sana kiuchumi, kijamii na kimazingira. Hilo halina ubishi. Na waathirika wakubwa wa vita hii ni nchi za africa. Hii inaweza ikawa mada nyingine

2. Hoja iliyoko mezani ni faida na hasara alizopata Russia kwa kuivamia ukraine. Conclusion ya mada inasema Russia kashindwa kutimiza mkakati au malengo ya uvamizi wake (Strategic failure) kwa hoja ya kwamba alichokuwa hakitaki (kusogelewa au kujitanua kwa NATO) ndo kakipata maradufu.
 
Nani kakuambia Russia ni mtu wa takwimu? Takwimu xipo CNN na BBC
Mkuu uwe unatulia na kuelewa hoja vizuri basi usiwe kama kasuku kupiga kelele tu.

Hapo mimi wala sijaomba takwimu wala sijazungumza takwimu ni hoja. Au hufahamu maana ya takwimu?

Hizi akili huwa mnatoa wapi na bado unataka kubishana na watu.

Mkuu Fanfa hapa utapoteza energy zako bure humu hakuna wa kujibizana hoja.
 
Majibu umeshatoa,sasa unataka ujibiwe kipi?Na kila anayekujibu tofauti na unavyopenda inakuwa kesi!
Mimi nimeanza na kukupa anguko la uchumi duniani na hasa Europe kutokana na vita!
Sijaona aliyejikita kwenye hoja zaidi ya porojo na matusi. Hata wewe ulichojibu ni nje ya hoja.

Ukisoma hoja iko very clear na maswali ya kuchokoza mada yako very clear. Bado mtu anapiga porojo badala ya kujikita kwenye hoja.
 
Mkuu uwe unatulia na kuelewa hoja vizuri basi usiwe kama kasuku kupiga kelele tu.

Hapo mimi wala sijaomba takwimu wala sijazungumza takwimu ni hoja. Au hufahamu maana ya takwimu?

Hizi akili huwa mnatoa wapi na bado unataka kubishana na watu.

Mkuu Fanfa hapa utapoteza energy zako bure humu hakuna wa kujibizana hoja.
kikiboxer Wala usipate tabu, Pro Russia nawamudu kwa hoja. Ndiyo màana hawawezi kujibu maswali yangu. Fuatilia maswali nayowauliza hakuna anayejibu wanaibuka na porojo badala ya kutupa majibu.

Hoja zangu zinapima uelewa wa Pro Russia ili tujue wana uelewa kweli wa mambo au ni porojo na propaganda ndo zimetawala vichwa vyao?
 
Back
Top Bottom