Kwanza hongera sana umejitahidi kutoa ufafanuzi wako kwenye filamu ya Royal Tour, lakini niseme tu andika lako limejaa hisia sana (subjective) kuliko kuunda hoja zenye mashiko (objective) ili kubainisha uzito na ukweli wa hoja zako.
Kwanza kabisa: Hadi uamuzi wa kurusha Royal Tour kufikiwa kufanyika Amazon, watu wanatazama data, Amazon mwaka 2021 ilikuwa na Subcribers 200 milioni duniani zote, ambapo siku nne zilizopita Netflix wana watumiaji 221 milion, unaweza kuona kuona tofauti ni ndogo tu.
Hata hivyo, watu wanahama kutoka kwenye traditional media kama Televisheni kuhamia kwenye matumizi ya internet, hivyo kuiweka Amazoni ni rahisi zaidi watu kutazama kupitia simu janja kuliko National Georaphic and Animal Planet kama unavyosema.
Pili: Rais Samia ni maarufu zaidi unavyodhani, hata hivyo, Royal Tour kuja Tanzania ni kwa sababu ya Rais Samia Suluhu. Unadhani kama angekuwa Magufuli Peter Greeneberg angekuja?
Umaarufu wa Rais Samia Suluhu kwanza umeletwa na umaarufu wa Tanzania wakati wa Hayati Magufuli, dunia ilifuatilia hasa siasa za Tanzania na hata Magufuli alipofariki Tanzania ikawa maarufu zaidi na hata Rais aliyefuata akawa maarufu maradufu kwani ni mara ya kwanza, kwa Tanzania kuwa na Rais wa kwanza mwanamke.
Rais Samia Suluhu amekuwa maarufu baada ya kuhutubia Baraza la Umoja wa Mataifa 2021. Rais Samia pia ameingia katika rekodi ya wanawake 100 wenye ushawishi Duniani 2021 katika Jariba la Forbes.
Rais Samia hakuwa na ulazima wa kushika kila taarifa, lengo la filamu ni kuonesha zaidi mandhari na uzuri wa nchi. Rais ni tour guide kwenye ile movie, na kumtumia Rais kuwa tour guide ni kichochoe tu watu wengi duniani wafuatilie, ila sio kutegemea Rais awe packed na kila taarifa ya Mbuga na mnyama, ingeboa. Ndio maana, filamu ilikuwa na shots kali mwanzo mwisho, na most of time, Peter aliingiza sauti mwenyewe.
Peter Greenberg hajaanza na Rwanda kama unavyosema, soma hapa; "He also produces and hosts a television series called
The Royal Tour which airs on PBS. The series features various heads of state giving Greenberg and viewers a personal tour of their country. It has featured a number of world leaders including New Zealand's
Helen Clark, Israel's
Benjamin Netanyahu,
Abdullah II of Jordan, Peru's
Alejandro Toledo, Mexico's
Felipe CalderΓ³n, Rwanda's
Paul Kagame, Poland's
Mateusz Morawiecki and Tanzania's
Samia Suluhu Hassan. Greenberg was previously the Travel Channel's chief correspondent."
Filamu ya Royal Tour tayari kabla ya kutoka, ilishavuta watalii wengi, zaidi ya 600 kutoka Israeli, zaidi ya 200 kutoka France na nchi nyingine za Ulaya.