Uandaaji wa filamu ya Royal Tour tumepigwa lakini uzinduzi wake tunapigwa zaidi!

Uandaaji wa filamu ya Royal Tour tumepigwa lakini uzinduzi wake tunapigwa zaidi!

Ukikitaka kizuri lazima uzurike wanasema waswahili wa mjini. Zipo faida tutakuja kuziona mbele ya safari, wanasema haraka haraka haina baraka.

Tuwe wapole tu kuna neema katika hii Royal Tour, kwani kukua kwa utalii pesa inayopatikana inakuza sekta nyinginezo (multiplier effect).
Utalii kukua kwa miundombinu ipi?
 
Umeniwahi, nilikua naanda mada niliyotaka kusema bado uwazi ni tatizo chini ya serikali hii ya CCM
Pascal Mayalla napata wasiwasi ungekuwa mbunge hawa watu wanaodaiwa kuwa si waongea ukweli ungeshirikiana nao vipi? Maana naona suala la uwazi bado huko lumumba ni tatizo kubwa
Rais Samia Suluhu amekuwa maarufu baada ya kuhutubia Baraza la Umoja wa Mataifa 2021. Rais Samia pia ameingia katika rekodi ya wanawake 100 wenye ushawishi Duniani 2021 katika Jariba la Forbes.

Mimi ni miongoni mwa watu waliompinga Magufuli kwa 100% na mpaka leo hii simkubali, lakini katika suala la umaarufu, Magufuli alikuwa maarufu huenda mara tano zaidi ya Samia Suluhu, iwe hapa Tanzania au duniani. Kwa nini? Sababu kuu ni hizi.
 
Huyu mama arudi maana kauli yake imeleta mfumuko wa bei Tanzania nzima
 
Your IQ is lowest in human kingdom! Kwa kushindwa kung'amua kuwa unaliwa katika uwekezaji wako ni upumbavu! Utapata akili wakati tayari umefilisika!
Hivi unadhani kuna kitu tutapata hapa wakati hata miundombinu ya kupokea watalii haipo!

Tutapigwa sana!
Umeshindwa kuiweka hiyo miundombinu? Ni fursa unaiona inakushinda wenzako wanaitumia.

Unangoja ufanyiwe au ufanyiziwe?
 
Utalii kukua kwa miundombinu ipi?
Ndege zinazonunuliwa ni miundombinu itakayosaidia kukuza utalii. JPM wakati anazinunua hizi ndege wapingaji wa kila kitu humu JF waliponda.

Samia anaifungua nchi kwa maana halisi, watanzania bado na akili zetu zile zile za kejeli na kupinga. Hatukui kifikra wala kimtazamo.
 
Narudia tena na tena, kuhusu mambo ya utalii shida ya sinema hiyo mmechemka sana, huwezi kunielewa ila ukiwa karibu na wadau wa sekta ya utalii ndipo utaelewa.

Pili mmechemka kwa upande wa pili, hiyo sinema yenu mmegusia Unguja na Arusha tu, mmesahau kugusia sehemu muhimu kutoka mikoa ya kusini hasa Kikwa kule Lindi.
Tunakwenda na big catch. Wewe na Sukuma Gang tumewacha mtengeneze ya kwenu itakayoonyesha vivutio vya kusini
 
Sijui viongozi wetu wanawaza nini lakini kwa kifupi ama wamepotoka au wanapotoshwa. Filamu ya aina ya Royal Tour si ya kwanza kuandaliwa duniani, ndugu zetu wa Rwanda walikwisha iandaa na imekwisha tazamwa sana. Sasa sijui kama viongozi wetu walikwisha fanya research ndogo tu kuona imeinufaishaje Rwanda. Manufaa ambayo kama Rwanda imepata basi yasingeweza kuwa siri ya ndani ya Rwanda bali pia spill over tungezipata hapa Tanzania au nchi nyingine za jirani.

Kitu cha kuzingatia ni kuwa wazo la kuandaa filamu hizi si la kwetu bali la hao wenye kumiliki uchumi lakini gharama ni za kwetu. Siyo siri katika kujenga uchumi wa nchi hakuna rafiki bali mwenye nguvu ndiye hushinda na kufaidi. Akili mu kichwa! Walio andaa wamefanikisha malengo yao bila jasho na kwa gharama nafuu.

Uzinduzi wa Royal Tour umekuwa balaa zaidi kwa hazina ya nchi! Rais wa nchi akiwa na wapambe wapatao 50 wamekaa zaidi ya wiki mbili nchini Marekani kufanya uzinduzi wa filamu hii kwa gharama za Watanzania walipa kodi. Wamarekani wamenufaika kwa kutembelewa na watalii kutoka Tanzania. Big brain amenufaika!

Kama hiyo haitoshi sasa uzinduzi utafanyika tena Tanzania kwa kodi zetu. Uzinduzi utafanyika Arusha, Zanzibar na Dar es Salaam. Tena washiriki watakuwa wengi zaidi! Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma! Tumepigwa!

Tujisahihishe!
Huko Amazon ni Watanzania wachache sana wataiona. Bora wangeiweka Netflix au Showmax..... Ngoja tuone huo uzinduzi wa Arusha. Labda watauza CDs kwa Wananchi.
 
Ndege zinazonunuliwa ni miundombinu itakayosaidia kukuza utalii. JPM wakati anazinunua hizi ndege wapingaji wa kila kitu humu JF waliponda.

Samia anaifungua nchi kwa maana halisi, watanzania bado na akili zetu zile zile za kejeli na kupinga. Hatukui kifikra wala kimtazamo.
Subiri uone zitakavyotumika!
 
Hata bombadia walisema tumepigwa, tz hua tunapigwa kila siku sio, Samia the planner
 
Pasi ndefu na Kilwa94 angalieni hii mtu inavyotapika lugha ya kitoto.
Hijui kitu wewe msukuma zaidi ya kula mahindi barabarani, kununua mapapai na kugawa, kunywa kahawa vijiweni na kununua jogoo.

Ile Serikali ya washamba kutoka Kolomije ilizikwa pamoja na mungu wenu Chato mwaka jana mweziachi
 
Pole sana, mpaka mwaka kuisha marehemu atakuwa na matarajio kapata wajukuu wa kutosha si kwa kufunguka huko aseee.

Tunajiandaa kununua zawadi as diapers.
 
Sijui viongozi wetu wanawaza nini lakini kwa kifupi ama wamepotoka au wanapotoshwa. Filamu ya aina ya Royal Tour si ya kwanza kuandaliwa duniani, ndugu zetu wa Rwanda walikwisha iandaa na imekwisha tazamwa sana. Sasa sijui kama viongozi wetu walikwisha fanya research ndogo tu kuona imeinufaishaje Rwanda. Manufaa ambayo kama Rwanda imepata basi yasingeweza kuwa siri ya ndani ya Rwanda bali pia spill over tungezipata hapa Tanzania au nchi nyingine za jirani.

Kitu cha kuzingatia ni kuwa wazo la kuandaa filamu hizi si la kwetu bali la hao wenye kumiliki uchumi lakini gharama ni za kwetu. Siyo siri katika kujenga uchumi wa nchi hakuna rafiki bali mwenye nguvu ndiye hushinda na kufaidi. Akili mu kichwa! Walio andaa wamefanikisha malengo yao bila jasho na kwa gharama nafuu.

Uzinduzi wa Royal Tour umekuwa balaa zaidi kwa hazina ya nchi! Rais wa nchi akiwa na wapambe wapatao 50 wamekaa zaidi ya wiki mbili nchini Marekani kufanya uzinduzi wa filamu hii kwa gharama za Watanzania walipa kodi. Wamarekani wamenufaika kwa kutembelewa na watalii kutoka Tanzania. Big brain amenufaika!

Kama hiyo haitoshi sasa uzinduzi utafanyika tena Tanzania kwa kodi zetu. Uzinduzi utafanyika Arusha, Zanzibar na Dar es Salaam. Tena washiriki watakuwa wengi zaidi! Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma! Tumepigwa!

Tujisahihishe!
Wewe ndo popoma kweli. Huoni Rwanda inavyopaa kiuchumi na sector ya utalii ndo inaipaisha? Kwani umejiuliza Rwanda pesa ya kigeni wanaipataje!! Nenda Rwanda ujionee ndo uje ufute ujinga wako hapa. Sukuma gang mna kazi Sana mwaka huu kumtetea Simba wa yuda
 
Nikijibishana na mpumbavu nitakuwa mjinga! Rwanda umefika au unasimuliwa?
 
Umeandika vitu vya kubumba, tena kubumba haswa. Eti Samia Suluhu ni mtu maarufu sana duniani? Kivipi? Kwa lipi?
Mimi ni miongoni mwa watu waliompinga Magufuli kwa 100% na mpaka leo hii simkubali, lakini katika suala la umaarufu, Magufuli alikuwa maarufu huenda mara tano zaidi ya Samia Suluhu, iwe hapa Tanzania au duniani. Kwa nini? Sababu kuu ni hizi.

1. Magufuli alipenda na kulazimisha aonekane maarufu kuliko mtu yoyote, kwa gharama zote. Magufuli alitamani kuua umaarufu wa wanasiasa wote ili umaarufu wote ubakie kwake. Ndio rais aliyetaka picha yake kwa lazima itundikwe kwenye ofisi zote za umma na binafsi nchi nzima kwa lazima. Popote alipokuwepo alitaka redio na Tv zote zirushe tukio lake kwa lazima tena live.

2. Misimamo migumu, ya ajabu, isiyoyumba yumba. Duniani ilimfahamu Magufuli kwa misimamo yake ya ajabu. Kuanzia misimamo ya kuwapinga vikali mabeberu, kuwaangamiza wapinzani wake, Korona.

3. Visa, vituko na mikasa. Magufuli alikuwa ni mzee wa drama mwanzo mwisho. Magufuli aliona fahari kujiita Kichaa na kujifananisha na mungu. Magufuli aliamini anajua kila kitu na anaweza kufanya kila kitu na kikafanikiwa. Mtu wa namna hii akicheza movie ni lazima ingehit tu duniani.

Note:
Waandaji wa Royal tour hawakuwa wanamtafuta mtu maarufu ili kutengeneza movie yao bali walikuwa wanatafuta mkuu wa nchi husika (rais) ili kucheza movie yao kwa sababu ya aina ya maudhui( mchango wa wanasiasa katika kukuza utalii) na malengo (kutangaza utalii) ya movie yao. Hata kama Samia Suluhu angekuwa maarufu sana kisiasa duniani bado asingetosha kucheza movie yoyote maarufu huko marekani kwa kuwa hana kipaji chochote cha kucheza movie. Mwisho kabisa unapaswa kufahamu kuwa project ya Royal tour ilianza kabla hata Samia hajawa rais wa Tanzania, na rais yoyote wa Tanzania ambaye angekuwa madarakani ingemhusu ikiwa angeridhia kushiriki.
Ukanikumbusha ile hashtag ya #whatMagufuliwoulddo dunia nzima ili trend Aiseeeh
 
Back
Top Bottom