Uasi mkubwa unakuja CCM

Uasi mkubwa unakuja CCM

Imebidi niingie kwenye ukurasa wa Bunge.
Kwenye news and events kuna heading. Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai Ajiuzulu.
Hapo utakuta taarifa kwa vyombo vya habari kuwa yeye Job ameandika barua kwenda kwa katibu mkuu wa chama chetu kujiuzulu nafasi yake.
Para 2 ‘Pia nakala ya barua yangu hiyo ya kujiuzulu nimewasilisha kwa katibu wa bunge…’
Hoja yangu:
1. Kwenye ukurasa wa Bunge, ipo tu taarifa kwa vyombo vya habari ambayo ndo imesambaa mitandaoni.
2. Barua ya Job kujiuzulu haipo.
3. Katibu wa Bunge hajakiri kupokea barua y job
4. Hakuna mahali katibu wa chama chetu amekiri kupokea barua ya Job
5. Sijaona mahali hiyo nafasi imetangazwa kuwa wazi[emoji848]

My take: Job ni Spika halali wa Bunge.View attachment 2078330
Katibu alikiri kuupokea BARUA ya mstaafu Ndungay

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
FB_IMG_1642046386736.jpg
 
Wakigombana na kuvurugana ndio furaha yetu, ili CCM itoke hapo ilipo na kuparaganyika, ni CCM wenyewe washindwe kuongea lugha moja...yaani CCM wawe kama wale jamaa waliokuwa wanajenga mnara wa babeli. Otherwise hawa mafisi wapumbavu wataitafuna hii nchi hadi vizazi vyetu vipite.
Divide and rule
 
Raia wa Tz wasio na meno ni kama mazombi,ata mkiambiwa cha kufanya hamtofanya maana kuandamana tu kunawashinda.
Wabongo sio wa kuwategemea,ukijidai kukomaa utanyooka mwenyewe,Mbowe yupo huko anateseka hakuna anaejali.
 
Ndio maana waliona waanze kumtoa tumbo tumbo then wafate na stone hili kwenye chama abakie mmoja mwenye nguvu, maana yule mwenye miaka 90 akili isharudi utotoni......lakini yote kwa yote huyu bi mdashi hasifikiri kundi jipya kukaa kwake kimya ni kwamba wamefyata.......jeshi la wananchi limetoka kutoa kauli majuzi na hiyo sio kawaida, that means huko juu wameshindwa kupata mapatano.
 
Pigeni ramli chonganishi ila shehe wenu ameishiwa udi na ubani na maduka hayafunguliwi usiku huu wa manane
 
Hakuna kitu kinaitwa sukuma gang ni conspiracy tu kuharibu reputation ya watu fulani

Kuhusu ccm maji ndio kwanza yanachemka
Naamini lile tamko la jeshini halijatoka bahati mbaya
Tuombe busara itawale wastaafu wasitumie nguvu zao vibaya
Jeshini kuna habari gani
 
Ni uasi ambao haujapata kutokea ndani ya chama cha mapinduzi CCM.. Baada ya kukaa madarakani muda mrefu sana ni kama kuna kikundi ndani yake kimejikuta kinajiona wao ndio ELITES wa hii nchi, na lolote ama chochote kinachofanyika ni lazima kipate kibali chao.

Imefika mahali kikundi hicho kilichojitengenezea ukwasi na mtandao wa ajabu wenye ufadhili mkubwa wa matajiri waliojatajirikia CCM ambao si watanzania asilia kwa asilimia 100. Kina uwezo wa nani awe nani kwenye nafasi gani.

Ujio wa mwendazake ulifanikiwa kwa kiasi chake kuudhoofisha huu mtandao wa hiki kikundi lakini naye akanaza kuharibu kwa kuanza kutengeneza himaya nyingine mpya ya upande mmoja tena kwa ukatili mkubwa sana.

Hapa kitisho kilikuwa wazi ni vita kati ya himaya mpya ya mwendazake vs mtandao kongwe THE ELITES ... Halafu sasa hiki kirusi kipya cha visiwani chenye vinasaba vingi na The elites! Hili linakolezwa na fununu zisizothibitishwa kwamba Taifa la Tz liko chini ya watoto wa familia moja.. 'Baba mmoja'... Ni TUHUMA!

Yaliyotokea ya mhimili mwingine mpaka kupelekea kujiuzulu, kauli ya mkuu wa kaya kuhusiana na 2025, uteuzi wa baraza jipya la mawaziri na makatibu wakuu pamoja na wengine wote kuna tafsiri moja tuu... Uasi ujao na vita mpya kati ya sukuma gang, mtandao wa the elites , visiwani na bara na chawa wenye maslahi kwa kila upande..

Kila kundi liko chimbo likijiandaa kivyake... Ni mchezo wa kuwindana...uasi mkubwa waja...na ndio nafasi pekee ya walio nje ya mfumo ku take cover!
Itakuwa Bora wakidhoofishana itakuwa fursa kwa wenye uhitaki wa katiba mpya iondoshe ujinga ujinga mwingine🤔.
 
Back
Top Bottom