Ubabaishaji wa Benki ya NBC kwenye kutoa mikopo

Ubabaishaji wa Benki ya NBC kwenye kutoa mikopo

Hii kubwa! Makato ya mkopo yanaanza kabla mteja hajaona hizo pesa za mkopo kwenye account yake? Huu ni wizi wa mchana.

Tatizo hakuna idara husika serikalini inayopokea na kufuatilia malalamiko ya wateja.
 
Hii bank imekuwa ya kizee sana, yani kama unatala kwenda kupoteza siku yako ukila kiyoyozi bank na NBC,
 
Usizidishe tu miaka 3, Benji zote ubabaishaji umewajaa na kinachouma processing fee
Kwani processing fee inakuwaje? Mfano umekopa milioni moja na riba jumlisha insurance kwa mwaka unarudisha 1,226,000/.
Swali processing fee inajumlishwa kwenye marejesho ama watakata kwenye iyo 1 million uliyokopa?
 
Bank ya NBC ni wababaishaji sana kuhusu utoaji wa mikopo. Sijui tatizo ni nini? Mtu anaomba mkopo taratibu zote zimesha kamilika mpaka makato tayari lakini hawaingizi mkopo. Kuna jamaa ameomba mkopo NBC yapata mwezi sasa umekwisha mkopo hawaingizi na anakatwa.

Amefatilia kwa Afisa Mikopo kamwambia yeye kashamaliza sehemu yake bado sehemu sijui ya mtu gani uko anayehusika kuapprove.

Kwakweli hii bank ni tatizo huduma zake haziriziki sishauri mtu hata siku moja kama ana uhitaji wa fedha kwa dharura aende NBC hakika utakwamishwa bila hata sababu za msingi. Kama kuna mdau anajua tatizo la kucheleweshewa mkopo atuambie.
Shukuru Mungu umekosa......mikopo yao haina baraka.....unaweza kuingia kwenye mitihani....
 
Back
Top Bottom