KERO Ubabe huu wa Kampuni ya Pepsi unalindwa na serikali?

KERO Ubabe huu wa Kampuni ya Pepsi unalindwa na serikali?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kwa wauzaji wa reja reja wa soda hulazimishwa na Kampuni ya Pepsi, kununua soda wasizotaka kununua wala wasizo na wateja nazo Ili wapewe soda aina ya Pepsi.

Huu ubabe wa Kampuni ya Pepsi unakera sana Lakini wauzaji wa soda kwa reja reja hawana ubavu wa kupambana nao.

Kwa nini Pepsi walazimishe wateja wao kununua soda wasizozihitaji? Watu wao wa masoko wanafanya kazi gani ya kutangaza bidhaa zao badala ya kufanya ulazimishi Kwa wateja wao?
 
Inashangaza sana. Mtu anapewa Seven Up au Mirinda Orange Ili tu apewe soda aina ya Pepsi.

Matokeo badala ya kupata faida, mtu anaishia kubakiwa na aina za soda asizo na wateja wake.
Wanunuzi wagomee kununua ili sisi wanywa soda tubadilike tuanze kunywa coca ambayo imejifia baada ya pepsi kubamba
 
Na hao wauzaji na wenyewe Wana tatizo. Kwani mkikataa wote kununua hizo soda mtafanywaje? Hapo ni mtu wa marketing anajaribu kuongeza mauzo yao. Haihusiani na serikali. Wakati mwingine market Ina nguvu ya kukorect any imbalance inayotokea.
 
Yees!!

Kwa dar hawathubutu. Lakini kwetu Iringa ni kawaida. Haiwezekani wakupe kreti lenye Pepsi Pekee, ni LAZIMA uchanganyiwe ama na Mirinda Orange au Fruit, Seven Up au Mountain Dew.
hata Arusha,Moshi, Dodoma nk ni ngumu, mtu hatochukua anawahama kabisa anabaki na coca-cola kampuni inatakiwa kuwa na adabu Kwa mteja
 
hata Arusha,Moshi, Dodoma nk ni ngumu, mtu hatochukua anawahama kabisa anabaki na coca-cola kampuni inatakiwa kuwa na adabu Kwa mteja
Maana unachukua soda ambazo huna wateja nazo, matokeo yake zinafanya mtaji ushindwe kuzunguka.

Na wenyewe hawajali na imeshakuwa kama ni sheria, na watanzania tulivyo, tunanung'unika tu huku tukiendelea kukandamizwa.
 
Kwani unalazimishwa kuchukua.Kataa wasiliana na Meneja wa Tawi linalohusika upewe maelezo kwanini unalazimishwa kununua usichokitaka.Kulalama tu hakutakusaidia chochote. Kama uliwasiliana na wahusika ulijibiwa nini?Sio kila jambo hata lililopo kwenye uwezo wako unailaumu Serikali.
 
Tushalalamika sana kwa meneja wa hapa Iringa. Aliniambia ni sera ya Kampuni. Nina Lengo la kuwasilisha rasmi malalamiko yangu kwa Tanzania Fair Competition Commission (TFCC) Kwa hatua zaidi za kisheria.
 
Wala mshiyashangae haya
Wahenga tunajua yalikuwepo na yataendelea kuwepo
Tulilazimishwa kununua betri ukitaka sukari
Unga kwa wembe utake usitake
Mpo kwenye Ujamaa bado
Enzi za Ugawaji na maduka ya Kaya ilieleweka maana kulikuwa na ukiritimba Wa soko wa mashirika ya Umma.

Lakini Sasa hizi ni zama za biashara huria (Siyo holela) hivyo Kuna kanuni za kuendesha mambo.
 
Back
Top Bottom