KERO Ubabe huu wa Kampuni ya Pepsi unalindwa na serikali?

KERO Ubabe huu wa Kampuni ya Pepsi unalindwa na serikali?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Nipo kijiji fulani hivi, nikaenda kununua chapati 3 nikajibiwa siwezi kununua 3 wenzangu watakosa.

Labda mbili.

Hawa wauza chapati wanatoa wapi huu ubabe?
 
Nipo kijiji fulani hivi, nikaenda kununua chapati 3 nikajibiwa siwezi kununua 3 wenzangu watakosa.

Labda mbili.

Hawa wauza chapati wanatoa wapi huu ubabe?
Huenda chapati inaendana na chai au maharage na profit margin kubwa ipo huko..., au wewe ni msala upitao sasa akiacha mbachao ambao kila siku wanakula nusu nusu siku ukirudi mjini itakuwaje ?
 
Hata wao wanapoenda kununua Zile reagent kwa ajili ya utengenezaji wa soda Aina zote za Pepsi, huuziwa kwa kulazimishwa vivohivo.
 
Hawana mshindani makini...
Siku moja gari lao la vinywaji lilipita mtaani nikataka kununua kreti kadhaa .. Jamaa walinigomea eti hawauzi bila order wakati walikuwa wanapitisha gari ndani ndani Kusaka wateja. 🤔
 
Bora umelisema hili mkuu,niliacha kuuza soda za pepsi kwa sababu hii,yaani ni vitu vya ajabu nataka kununua peps cret 2 naambiwa napewa moja peps na yapili nichanganyiwe mirinda na 7up au mountdue kama sitaki niache,aisee sijui meneja wa hii comp.anafanya nini officin
 
Pole Sana Allen.
Mimi nimefanya Kazi Miaka kadhaa Kiwanda cha Pepsi mkoa flani plant katika wadhifa wa Mauzo.

Ukisema madereva au mamemeneja na salesman ndio chanzo unavuna dhambi ya Bure ndugu.

Kuna kitu Kinaitwa SALES TARGET Wahusika wanapewa target ya Mauzo na General manager kushuka Kwa sales manager, area sales manager, salesmans, Distribution team, drivers na idara nyinginezo kupush namba ya mauzo ya kila brand husika Kwa mwezi... Kama target ya mountain dew kuuzwa Kwa mwezi ni 1,000 crate, mirinda fruit 10,000crates, 7up nk hivyohivyo walio chini wanapaswa kufanya hivyo hivyo. Na Mtu yeyote hatayekwamisha hiyo namba ya mauzo ya brand husika Anawajibishwa hata kufukuzwa KAZI.

Kwahiyo huyo meneja unayemsema naye anapapambania ugali wake kupitia target za mauzo ya brand mbalimbali kama alivyopewa maelekezo kutokea juu.

Kwa msaada Wa Jambo lako inabidi uonane na Mtu mwenye wadhifa wa Cheo Cha General Manager ama CEO ndo utapatiwa uvumbuzi. Hawa wengineo mtachanganyana na kuvurugana Tu.

Sasa jitahd katika hili, Uwe angalau unauwezo Wa Kununua mizigo Wa crate 200 Kwa week.
Ila chini ya hapo mtafute Anayekuuzia huo mizigo anayekuleteaga myajenge mnazungushaje hizo brand Maisha yaendelee...
 
Kwa wauzaji wa reja reja wa soda hulazimishwa na Kampuni ya Pepsi, kununua soda wasizotaka kununua wala wasizo na wateja nazo Ili wapewe soda aina ya Pepsi.

Huu ubabe wa Kampuni ya Pepsi unakera sana Lakini wauzaji wa soda kwa reja reja hawana ubavu wa kupambana nao.

Kwa nini Pepsi walazimishe wateja wao kununua soda wasizozihitaji? Watu wao wa masoko wanafanya kazi gani ya kutangaza bidhaa zao badala ya kufanya ulazimishi Kwa wateja wao?
Tuendako ni kugumu zaidi
 
Sasa jitahd katika hili, Uwe angalau unauwezo Wa Kununua mizigo Wa crate 200 Kwa week.
Kreti 200 si Agent huyo? Nazungumzia wauzaji wa reja reja.
Ila chini ya hapo mtafute Anayekuuzia huo mizigo anayekuleteaga myajenge mnazungushaje hizo brand Maisha yaendelee...
Sasa tuyajenge nje ya taratibu zinazojulikana?

Maelezo yako yameonesha kuwa kumbe huu ni mfumo lazimishi wa Kampuni na hautokei kwa bahati mbaya.

Nadhani siyo ya kwangu binafsi, huu mfumo si halali na lazima itafutwe njia ya kuukomesha.

Kampuni iweke hayo malengo yake lakini yafikiwe kitaalam na iwekeze kwenye kutangaza hizo bidhaa zake zisizotoka sokoni badala ya kulazimisha wateja wake kununua bidhaa wasizoweza kuuza.
 
Kwani unalazimishwa kuchukua.Kataa wasiliana na Meneja wa Tawi linalohusika upewe maelezo kwanini unalazimishwa kununua usichokitaka.Kulalama tu hakutakusaidia chochote. Kama uliwasiliana na wahusika ulijibiwa nini?Sio kila jambo hata lililopo kwenye uwezo wako unailaumu Serikali.
Solution ipo hapa. Wasiliana na Mkuu Wa Tawi akizingua endelea na uongozi wa juu.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Solution ipo hapa. Wasiliana na Mkuu Wa Tawi akizingua endelea na uongozi wa juu.
Angalia maelezo aliyotoa airwing . Ni mfumo toka ngazi ya juu kabisa ya Kampuni.

Kampuni inaweka "target" lakini haiwekezi kwenye kutangaza bidhaa wanazoziwekea target. Matokeo yake bidhaa zile zisizo na soko zinawekwa juu ya soda ya Pepsi.
 
Ikiwezekana awaandikie hata makao makuu ya PEPSI wenyewe. Wako serious sana wale jamaa kwenye kulinda brand yao.
 
Kwa wauzaji wa reja reja wa soda hulazimishwa na Kampuni ya Pepsi, kununua soda wasizotaka kununua wala wasizo na wateja nazo Ili wapewe soda aina ya Pepsi.

Huu ubabe wa Kampuni ya Pepsi unakera sana Lakini wauzaji wa soda kwa reja reja hawana ubavu wa kupambana nao.

Kwa nini Pepsi walazimishe wateja wao kununua soda wasizozihitaji? Watu wao wa masoko wanafanya kazi gani ya kutangaza bidhaa zao badala ya kufanya ulazimishi Kwa wateja wao?
Mm mkuu sojakuelewa,umelazimishwa wapi?hela ya kununua ni ya nan?
 
Back
Top Bottom