KERO Ubabe huu wa Kampuni ya Pepsi unalindwa na serikali?

KERO Ubabe huu wa Kampuni ya Pepsi unalindwa na serikali?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mm mkuu sojakuelewa,umelazimishwa wapi?hela ya kununua ni ya nan?
Kwenye biashara wanachotaka wateja ndicho muuzaji hukiweka sokoni.

Kama bidhaa huzalishi wewe na ndiyo inayoongoza kwa kununuliwa sokoni, basi hulazimika kuiweka.

Sasa kwa hoja hii wateja wanataka soda aina ya Pepsi, na muuzaji wa reja reja ANALAZIMISHWA kununua soda aina nyingine ili apewe Pepsi.

Huko ni kulazimishana kinyume cha Sheria za biashara za Tanzania.
 
Kwa wauzaji wa reja reja wa soda hulazimishwa na Kampuni ya Pepsi, kununua soda wasizotaka kununua wala wasizo na wateja nazo Ili wapewe soda aina ya Pepsi.

Huu ubabe wa Kampuni ya Pepsi unakera sana Lakini wauzaji wa soda kwa reja reja hawana ubavu wa kupambana nao.

Kwa nini Pepsi walazimishe wateja wao kununua soda wasizozihitaji? Watu wao wa masoko wanafanya kazi gani ya kutangaza bidhaa zao badala ya kufanya ulazimishi Kwa wateja wao?
utalazimishwaje pesa ni yako bro!!!!???,kama kuna bidhaa isiyo na wateja wanakutaka uinunue acha kabisa kuchukua mzigo wao.
 
Back
Top Bottom