KERO Ubabe huu wa Kampuni ya Pepsi unalindwa na serikali?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Tushalalamika sana kwa meneja wa hapa Iringa. Aliniambia ni sera ya Kampuni. Nina Lengo la kuwasilisha rasmi malalamiko yangu kwa Tanzania Fair Competition Commission (TFCC) Kwa hatua zaidi za kisheria.
Wajinga sana hao, sasa kama wanaona baadhi ya aina za soda hazinyweki si waache kutengeneza au kuzalisha kidogo sana?
Kwanini walazimishe kuwa na aina kumi wakati zenye soko ni sita kwa mfano?
 
Maana unachukua soda ambazo huna wateja nazo, matokeo yake zinafanya mtaji ushindwe kuzunguka.

Na wenyewe hawajali na imeshakuwa kama ni sheria, na watanzania tulivyo, tunanung'unika tu huku tukiendelea kukandamizwa.
Achana anazo peleka pesa kwenye bidha nyIngIne zinazotoka haraka kwanza faida ya soda ni ndogo sana 2000 kama sikosei..japo kibishara ni pesa lakini si ya kuwekewa vikwazo vya kijnga
 
Wajinga sana hao, sasa kama wanaona baadhi ya aina za soda hazinyweki si waache kutengeneza au kuzalisha kidogo sana?
Kwanini walazimishe kuwa na aina kumi wakati zenye soko ni sita kwa mfano?
Nashangaa kwa nini hii mantiki ya masoko inawapiga chenga. Kama bidhaa haikubaliki sokoni iondoe acha ile inayokubalika.
 
Kwani wakiwa wanakuuzia Soda zao wanakushikia Bunduki?
Hitaji la soko. Pepsi Ina wateja wengi Sana hivyo wauza soda wanaona ni fursa kwao kutengeneza faida kupitia soda aina ya Pepsi.

Ila bidhaa nyingine za Kampuni ya Pepsi hazinunuliki. Kwa ivo Kampuni inatumia uhitajikaji wa Pepsi sokoni kuwafanya wauza soda mateka wao.
 
Soko lolote linakuwa determined na supply na demand.Anzisheni kwanza umoja wa wauzaji wa Pepsi then fikieni maazimio kwamba hamkubali kununua kwa masharti hayo.Watakubaliana tu na uhuru wenu wa kutochaguliwa.Nafikiri uongozi wa Pepsi umeona ni rahisi kuwaburuza kwani mnakubaliana na uvunjifu wa masharti ya soko huria.
 
Point.

Wazo la kuungana ni mujarabu sana.
 
Na hili nalo ni la kilia lia? Watanzania nani katuroga? mbona tu wajinga sana? aisee inafikirisha sana
 
Ningekuwa mimi nanunua bidhaa za Coca Cola tu,
Na nyinginezo
 
Yees!!

Kwa dar hawathubutu. Lakini kwetu Iringa ni kawaida. Haiwezekani wakupe kreti lenye Pepsi Pekee, ni LAZIMA uchanganyiwe ama na Mirinda Orange au Fruit, Seven Up au Mountain Dew.
Hata Dar wameshawahi kufanya huo mchezo ila haukudumu Dar walalamikaji ni wengi Sana na wakiamua kulalama aisee utajuta maana vijiwe vyote vikiamua story ni za Pepsi kuanzia ilala sharifu shamba mpaka Lumumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…