Ubadhirifu wa dawa zenye thamani ya Tshs 26.7 billioni wabainika kwenye Hospitali za Rufaa za mikoa 28 Tanzania bara

Ubadhirifu wa dawa zenye thamani ya Tshs 26.7 billioni wabainika kwenye Hospitali za Rufaa za mikoa 28 Tanzania bara

Haya mambo Ndiyo yamelifanya bara la Africa kuwa na watu wachache wanaoshika Uchumi wake na wengine wengi kuwa masikini wa kutupwa

Wizara iwachukulie hatua Kali hawa majambazi wasiotosheka na haki ya jasho Lao

JPM na Serikali yake wanahaha Ni Kwa kiasi gani maji yawafikie kila mwananchi, umeme na huduma Bora za kiafya, halafu watu wachache tu wawe sehemu ya mamilioni ya Watanzania kukosa haki zao na saa nyingine kupoteza maisha Kwa sababu Yao!!

Wakamatwe na Sheria ifuate mkondo wake
 
Wizara ya Afya imebaini upotevu wa Sh26.7 bilioni za dawa uliosababishwa na uzembe, kutojali katika usimamizi wa mfumo wa ugavi wa bidhaa za afya, viashiria vya hujuma, wizi na udokozi wa bidhaa za dawa.

Hayo yamesemwa leo Machi Mosi, 2020 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Doroth Gwajima wakati akitoa tamko kwa vyombo vya habari kuhusu matokeo ya ufuatiliaji huo.

“Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kukosa huduma ya dawa na vipimo katika vituo vya kutolea huduma katika ngazi zote kinyume na matarajio, jumla ya thamani ya fedha ambayo imethaminishwa kwa upungufu huu inakadiriwa kuwa siyo chini ya Sh26.7 kwa kipindi cha Julai 2019 hadi Desemba 2020,” amesema Dk Gwajima.

Amesema kufuatia malalamiko hayo, wizara iliunda kamati ya wataalamu kutoka Wizara na taasisi za sekta mbalimbali ili kufanya ufuatiliaji katika hospitali 28 za rufaa za mikoa kwa kipindi cha miezi 18.

“Lengo ilikuwa kubaini changamoto zinazochangia upatikanaji duni wa dawa na vipimo licha ya kuongezeka kwa mtaji wa dawa,

Jumla ya bidhaa za dawa na vipimo 20 hadi 30 tu kati ya nyingi zilizo kwenye orodha ya bidhaa za afya kwa kituo husika ndiyo zilifanyiwa ufuatiliaji kuanzia ununuzi, mapokezi na matumizi,” amesema Dk Gwajima.

Mwananchi
Sahihisha paragraph ya 2 iwe Machi 1, 2021.

Katika hili yule mtu ambaye anashtakiwa Mahakamani na TAKUKURU ndiye mhusika Mkuu ambaye amepelekea upotevu wa Tsh 26 Bilioni. Huyu ni Laurean BWANAKUNU Rugambwa ambaye kwenda kwake MSD kuligubikwa na mizengwe.

Na akiwa Mkurugenzi Mkuu MSD alijenga mtandao wa yeye, Waziri Ummy Mwalimu, supplier wa dawa Bahari Pharmacy na baadhi ya watu wa TISS katika kuhujumu MSD.

Sasa ni wakati mwafaka wa kuboresha mashataka yake ili upotevvu huu uweze kuwa accounted
 
Wizi wa dawa ni biashara kubwa sana kuna kipindi Marekani kupitia usaid ilikuwa inatoa msaada wa dawa za malaria Tanzania lakini dawa hizo zilikuwa zinakutwa zinauzwa Angola walipoamua kufatilia qakakuta kontena likifika airport linapotea
Mbali ya kuibwa na kuuzwa nchi jirani zingine zimekuwa zikiozea Bohari ya Dawa - MSD na badae kuharibiwa na kuchomwa kwa maana ya expires!!!!!!.

Hii ni aibu sana kwa Serikali kuozea dawa kwenye Bohari ya Dawa - MSD badala ya kuzisambaza kwenye mahospitali hapa nchini.
 
Sahihisha paragraph ya 2 iwe Machi 1, 2021.

Katika hili yule mtu ambaye anashtakiwa Mahakamani na TAKUKURU ndiye mhusika Mkuu ambaye amepelekea upotevu wa Tsh 26 Bilioni. Huyu ni Laurean BWANAKUNU Rugambwa ambaye kwenda kwake MSD kuligubikwa na mizengwe.

Na akiwa Mkurugenzi Mkuu MSD alijenga mtandao wa yeye, Waziri Ummy Mwalimu, supplier wa dawa Bahari Pharmacy na baadhi ya watu wa TISS katika kuhujumu MSD.

Sasa ni wakati mwafaka wa kuboresha mashataka yake ili upotevvu huu uweze kuwa accounted
Ni kweli kabisa!!!!

Na manunuzi ya hizo dawa zilikuwa zinanunuliwa kiholela sana pale MSD wakati wa uongozi wa huyo Laurian Ruganbwa Bwanakunu. Ni kweli kabisa kulikuwa na syndicate kubwa na hatari sana kwenye suala la manunuzi ya dawa pale MSD hadi kwenye Tender Board ambapo Bwanakunu alihakikisha anaweka team yake kwa mfano; Abdul Mwanja - Katibu wa Tender Board, Victoria Mwanri Elangwa - Mwenyekiti wa Tender Board, hii combination ilikuwa ni hatari sana kwa ustawi wa Bohari ya Dawa - MSD!!
 
Kwa nchi hii mtu hawezi kujificha!!

Heko Sana mkuu,
 
Ni kweli kabisa!!!!

Na manunuzi ya hizo dawa zilikuwa zinanunuliwa kiholela sana pale MSD wakati wa uongozi wa huyo Laurian Ruganbwa Bwanakunu. Ni kweli kabisa kulikuwa na syndicate kubwa na hatari sana kwenye suala la manunuzi ya dawa pale MSD hadi kwenye Tender Board ambapo Bwanakunu alihakikisha anaweka team yake kwa mfano; Abdul Mwanja - Katibu wa Tender Board, Victoria Mwanri Elangwa - Mwenyekiti wa Tender Board, hii combination ilikuwa ni hatari sana kwa ustawi wa Bohari ya Dawa - MSD!!
Tukiishi Kwa kufumbiana macho hakuna kitakachofanyika

Nashauri kuwepo Sheria itakayobainisha wizi unaofikia milioni kumi tu serikalini mtu huyo afungwe maisha
 
If this is true, lifestyle audit ya wahusika wote ni ya muhimu sana. Nchi hii ina majizi mengi sana ya kufunga maisha
 
Bado kuna watu wanamdharau huyu Waziri Gwajima? Tuachane na COVID 19 je wangapi walikuwa wanajuwa kuwa kuna upotevu wa Billion of Tsh kwenye Shirika la MSD?

Halafu bado eti wanamsifia UMMY MWALIMU kuwa alikuwa anaweza. Waziri alikuwa wapi wakati haya yanatokea? Huyu Waziri ndiyo inadaiwa Bwanakunu alikuwa kiserengeti boy chake?

Kuna ripoti ya CAG ya 2018/19 sehemu moja unasema hivi;
" Ukaguzi huo wa CAG una mashaka kuwa ukwasi wa MSD unazidi kushuka hivyo kuathiri utekelezaji wa mipango mbalimbali ikiwemo usambazaji wa dawa na vifaa tiba kwa jamii pamoja na utekelezaji wa mipango yake mingine. "

Hii ni ripoti ya 2018/19 na bado Waziri Ummy Mwalimu hakuchukua hatua
 
Haya mambo Ndiyo yamelifanya bara la Africa kuwa na watu wachache wanaoshika Uchumi wake na wengine wengi kuwa masikini wa kutupwa

Wizara iwachukulie hatua Kali hawa majambazi wasiotosheka na haki ya jasho Lao

JPM na Serikali yake wanahaha Ni Kwa kiasi gani maji yawafikie kila mwananchi, umeme na huduma Bora za kiafya, halafu watu wachache tu wawe sehemu ya mamilioni ya Watanzania kukosa haki zao na saa nyingine kupoteza maisha Kwa sababu Yao!!

Wakamatwe na Sheria ifuate mkondo wake
Kwa vile huna unalolijua, una haki ya kubwabwaja namna hii.
 
Timu ya ukaguzi maalumu kutoka Wizara ya Afya imegundundua ubadhirifu huo wa dawa na vifaa tiba kutoka hospitali hizo za rufaa za mikoa kwa kipindi cha miezi 18 kuanzia Kula 2019 hadi Desemba 2020. Hayo yametangazwa leo na Waziri wa Afya Dr Dorothy Gwajima wakati akitoa taarifa ya uchuguzi huo uliotokana na malalamiko ya wananchi ya kukosa dawa mara kwa mara kila wakienda kutibiwa kwenye hospitali hizo. Taarifa kamili soma kiambatanisho hapo chini
Walaji na wapigaji ni watumishi wa hiyo wizara,hakuna mtu anayeweza kutoka kubeba zege akaenda kuhujumu hospital
 
Pamoja na kumkaanga wazi wazi waziri mwenzie aliepita,sasa na yeye kwa kugundua madudu hayo tuone ana jambo lipi jipya la kuboresha hiyo taasisi.
 
Duh yaani pamoja na ukali wa Dkt Magufuli watu wanaiba tu? Kuna MD mmoja alikuwa na range rover sport plus life nouma
 
Mfumo wa afya wa nchi hii lazima ubadilike kinyume na apo mtakuwa mnawaonea watumishi kila siku kuwa wanawaibia dawa.
Hospital na na vituo vya afya vilivyochin ya serikali huduma za misamahaa ziko juu kuliko wanaolipia so kujiendesha n kaz
Kama nchii tuamue if tunatoa huduma za afya kama sehemu ya kusaidia wanachi au tuiendeshe sekta ya afya kama private sekta kina aga khan.
Nb wananchi wasifurahie iyo kashfa anayoieneza Mama coz kinachofuata n maumivu kwao maaana sasa huduma zinaenda kuwa ghali kwao kwa lengo la hospital kupata faida na kujiendesha kama taasisi binafsi
Duuh!

Sent from my TECNO BC1 using JamiiForums mobile app
 
Sijaona sehemu waharifu watapelekwa mahakamani.

Maigizo tu.
 
Mlungula kivipi mkuu? Fafanua tujifunze wengi hapa
Wanaowalipa hukata malipo kwa visingizio mbalimbali ikiwemo dawa ni nyingi sana au ghali kuliko kawaida.

Mwenye pharmacy " akinyoosha mkono" malipo yanapita bila matatizo.

Kuna uzi humu ndani kuhusu suala hilo.
 
Back
Top Bottom