Mohammed Said usiwe mnafiki.
Wewe ni mmoja wa watu humu mtandaoni mlioendeleza ubaguzi, kwako ulikuwa wa kidini.
Mwalimu aliwaonya, na sasa utabiri wake unatimia.
Mwalimu alisema,
"Zanzibar ikianza kujibagua toka Bara hawatabaki salama maana slama ya Zanzibar ni umoja na Bara.
Wakiisha kuwabagua Bara watakuwa wamefanya dhambi kama wachawi wanaokuka nyama ya watu.
Ulila nyama ya mtu utaendelea kula nyama ya mtu.
Mwalimu aliendelea kuwa, baadaye Wazanzibari wataendeleza dhambi ile ile ya ubaguxi na kugundua kua Zanzibar kuna Wazanzibari na Wazanzibara, na kuna Wapemba na Waunguja, hawatabaki salama hata kidogo"
Leo Mohammed Said, ukiwa mtu mzima mwenye akili yako washangaa nini, umeuendekeza sana ubaguzi wa kidini na makala zako za kuwa sifia na kuwaenzi "wazazi wako waislamu" humu mtandaoni, kwamba ndo walileta uhuru.
Ulihusika moja kwa moja kupanda mbegu za chuki katika jamii.
Zanzibar walipoanza na sera za kujibagua, ili wapate kujitambulisha nani ni mzanzibari(kwa kuwabagua wabara) sikuwahi kuona makala zako za kuonya juu ya ubaguzi huu.
Wengi tulilaumu hili, lakini kwa vile wazanzibari kupitia Baraza La Wawilishi, ndo liliendeleza ubaguzi huu hadi kufikia hatua ya kumpiga mrufuku ya kukanyaga Zanzibara Waziri Mkuu Pinda, wengi walishangaa ubaguzi na umoja wa kibaguzi wa wazanzibari.
Lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kuonya juu ya hili.
Leo mbele ya kadamnasi u Hizbu na u ASP unaonyeshwa hadharani- tofauti zilizokuwepo hata kabla ya uhuru.
Halafu mtu mwenye akili unailaumu CCM.
HUU NI UNAFIKI MKUBWA.
Mnavuna mlichopanda, na Mwalimu was right, salama ya Zanzibar ni Tanganyika.