Ubaguzi wa kisiasa anaouonesha Magufuli hadi CCM wenyewe wanamshangaa

Yeye alikuwa mbunge wa chato toka 95 je alimaliza changamoto zao, Tena wananchi wake waliwahi kumpa Kero ya barabara, akawaambia wanye watandaze mavi yawe lami
😁😁😁😁
 
Ila hapo aliponyang'anywa mic si kwasababu alimuadentify kama ni diwani wa chama gani bali ni kwasababu huyo mzee anazunguka sana kujielezea.....

Raisi amekuja kwa ziara ya kushtukiza yeye anaanza kutoa salamu kwa ndugu na jamaa badala ya kwenda straight kwenye point iliyomleta anazunguka na kuleta mambo ya chama cha mapinduzi.....

Nyoosha maelezo, NASHUKURU MHESHIMIWA AND RAIS. CHANGAMOTO ZA WANANCHI ENEO LETU NI MOJA MBILI TATU, SISI KAMA VIONGOZI TUMEFANYA MOJA MBILI TATU KUKABIRIANA NA CHANGAMOTO HIZO NA TUMEKWAMIA HAPA.....


Sasa yeye anaanza, magufuri hoyeeeeeee kwann asishushuriwe....
 
Hili ndiyo lengo lake,hata CCM wenzake wanamshangaa.
Watu wazima wanajichekesha huku uvunjifu mkubwa wa katiba ukifanywa na watawala na taasisi za dola na hakuna anayethubutu kuhoji/kuuliza/kukemea.Hivyo baada ya 2020 atawahenyesha na anaenda kuondoa ukomo wa urais au kufuta chaguzi kabisa na hatutakuwa na LA kufanya.
 
Kwanini baada ya kuambiwa ni diwani wa ccm akaridishiwa?
 
Kuna watu watasifia hivo vitu
 
Kweli tutakwisha maana Kim Jong ni noma
Msijiite wapinzani, nyie ni wachumia tumbo, wala hamkua na nia ya kuuza sera bali ni kutaka kuleta mtafaruku. Uzuri sasa hivi mmekwisha kabisa kabisa hamna mpya wala pa kujifichia
 
Ni sawa wa tu hata ningekuwa mimi diwani/mbunge wa chadomo wa Kazi gani? Ningemfukuza kabisa eneo nililokuwepo, Kazi kupinga pinga tu.kama ndio wa Cha Domo unafikiri angeongea Nini? Wapinga maendeleo ndio dawa yao hiyo, Safi sana magufuli.
Wazee wa kusia kila kitu
 
Ubaguzi huu umeshaanza kumea na kama atapitishwa tena kipindi cha pili hadi anamaliza miaka yake kumi ubaguzi huu utakuwa umekomaa na kuzaa chuki na uhasama hivyo kuiacha Tanzania yenye chuki kati ya wanaccm na wapinzani wa kweli. Hii ni hatari kubwa.
 
Anadhani kupiga virungu mawazo mbadala ni kufanikiwa..
 
Nikiwa mdogo tunapiga story na babu tulipokuwa tuna mtembelea kule kijijini kuna mmoja aliwahi kumuuliza, tunamtambuaje mchawi tukikutana naye?
Nakumbuka sifa moja aliyoisema ni kuwa mchawi ni mbaguzi. Hata kama kuna shughuli na watoto (kama sie) tumekaa pamoja na tunapaswa kugawiwa chakula au hata mahindi ya kuchoma tuu basi bila aibu atawapendelea wa kwake kwanza.
Na msipo angalia wengine hata sumu aweza kuwapa.
Mbaguzi hana tofauti na mchawi, na mtu kuwa mchawi haijalishi cheo chake bali ni hulka eitha ya kurithi au kujilazimisha kutokana na moyo wako kuwa wa chuki.
Hatuwezi kumnyooshea mtu kidole kuwa ni mchawi lakini tunaweza kuwa na mashaka naye kutokana na viashiria
 
Sasa hivi hayo ni manyunyu,akimaliza kubagua upinzani ni anahamia kubagua CCM rasmi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…