Ubaguzi wa kisiasa anaouonesha Magufuli hadi CCM wenyewe wanamshangaa

Umesikia na si ni walamba viatu kama Dr slaa kwa njaa xake.
Bora ungekuwa mlamba viatu! Hakuna hasara kubwa hapa duniani kama mtu kuwa ndegative.... you just end up dealing with the marginals maisha yako yote mpaka cku unaenda kaburini. Tatizo kubwa sasa ni kwamba negativity huwa inakuwa na pronounced effect kubwa zaidi kwa wasiokuwa negative, na inawa-affect zaidi wao kuliko mhusika mwenyewe. Nilishasema kuwa ukikuta mtu negative ana kitu positive, ujue kapora kwa nguvu au kwa njia zingine anazozijua yeye!
 
Maendeleo yote tuyayaona South Africa yaliletwa na makaburu lakini akina Mandela nawenzake walikubali wafie jela kuliko kuwa chini ya utawala dhalimu wa makaburu.
 

Huwezi kuona tatizo maana ww ni mfaidika wa utawala huu, hivyo sitegemei maoni tofauti na haya toka kwako. Hilo la kusema utawala wa sheria, nilikuambia toka juzi uwepo wa sheria ni jambo moja, na utekelezaji ni jambo jingine. Na hakuna nchi isiyo na sheria, ila ni sheria za aina gani hapo ndio hoja ilipo. Maoni ninatoa, ila ninatolea wapi? Hivi unadhani kwenye nchi zenye udictator watu hawatoi maoni yao? Wanatoa sana, ila usalama wao ni jambo jingine.

Hao wakoloni walitumia mapato kujenga hiyo miradi, sio kwamba walitoa kwenye mishahara yao. Kama wazungu walijenga reli, viwanja vya ndege, mashule nk, bado hata wao walitumia mapato kujenga miradi. Hao wazungu unaolia waliondoka miaka 60 iliyopita, mbona bado sisi ni masikini?
 
Sitaki niandike mistari mingi kama ulivyotiririka.
Jibu swali moja tu. Hao wakoloni walipoondoka hapa Tz mwaka 1961 waliacha barabara ngapi za rami ambazo ni barababara kuu?
 
 
Team Mwenyekiti kwa sasa meno yote 32 nje...kasheshe ni kwa hawa wenzangu mie ni shughuli pevu kupenyapo.
 
Sitaki niandike mistari mingi kama ulivyotiririka.
Jibu swali moja tu. Hao wakoloni walipoondoka hapa Tz mwaka 1961 waliacha barabara ngapi za rami ambazo ni barababara kuu?

Kwa taarifa yako, watu watakaokuwepo mwaka 2070 watajiuliza Magufuli aliacha barabara ngapi za lami, na madaraja kiasi gani. Maana wakati huo yatakuwa mengi kuliko sasa. Nadhani swali lako majibu yake yako humo.
 
Kwa taarifa yako, watu watakaokuwepo mwaka 2070 watajiuliza Magufuli aliacha barabara ngapi za lami, na madaraja kiasi gani. Maana wakati huo yatakuwa mengi kuliko sasa. Nadhani swali lako majibu yake yako humo.
Kama yameachwa na mtanzania tena mzalendo haina tabu. Nashangaa wewe kusifia reli iliyojengwa na mkoloni aliyekuwa anatunyonya kwa kila namna.
 
Kwani kawe alumni ,bia yetu ,Ussr wanasemaje

Sasa si afute hivi vyama vingine ili tuwe wakomunisti

Maana inaonekana havina maana

Futeni vyama vyote vya upinzani tuanze moja mbaki CCM tu



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesikia shangwe alizopata Prof Jay...Jamaa walitamani wampore MIC ila ndiyo hivyo tena.WanaKilosa wapo Baaado Muacheni aendelee kutuwakilisha.Kuna watu wanakera tuu,sasa Lijualikali alikuwa hana hata cha kuongea yupo yupo tuu
Nimeangalia kipande cha video sehemu anayoongea Mh. Joseph Haule,kwa kweli nimepata uhakika kuwa Watanzania wengi wanajua nani ni kiongozi wao wa kweli na mtetezi wao hasa. Kushangiliwa kule kuna maana kubwa sana,kwamba upinzani unaaminiwa na Watanzania,na kwamba kukiwa na tume huru,uchaguzi huru na wa haki,hakika CCM itakuwa kwaheri.
Keep it up the good work upinzani na Mungu Mwenyezi awatangulie.
 
Hili lilituumiza sana watu wa Kimara,Mbezi,Kibamba kwa kuvunjiwa nyumba zetu bilabila kisa tu,,,tulichagua CHADEMA kuwa wabunge wa Jimbo la Kibamba na Ubungo. Maumivu na Mateso yetu hayatosahaulika kwa vizazi vyetu vyote hadi utimilifu wa dahari!
 
Acha chuki na hasira. Hata treni ya Sgr utaipanda wewe na jamaa zako. Mbona mlikodi Bombardier kwenda na kurudi mpaka Mwanza.

Hata treni ya Mkoloni tunapanda mpaka leo. Kumbe tulikodi Bombardier, nilidhani ni bure. Kwa taarifa yako, hata precision air na fast jet kabla ya figisu tulizipanda sana.
 
Amewahi sema jimbo la upinzani hapeleki fedha.

Jimbo la tundu lissu hakupeleka chochote hadi walipo mfuta lissu ubunge.
Hili lilituumiza sana watu wa Kimara,Mbezi,Kibamba kwa kuvunjiwa nyumba zetu bilabila kisa tu,,,tulichagua CHADEMA kuwa wabunge wa Jimbo la Kibamba na Ubungo. Maumivu na Mateso yetu hayatosahaulika kwa vizazi vyetu vyote hadi utimilifu wa dahari!
 

Ndio moods mkerejetwa wa kijani Sasa hii picha au katuni nikiyoposti ina shida gani hebu nielimishe nijue ,umekazana kublock hivi Mimi au mtu mwingine yoyote tunaweza kufanana mawazo na yako unavyotaka niandike au nifanane na wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…