Ubaguzi wa kisiasa, mikoa ya Kusini ni Soweto ya Tanzania

Ubaguzi wa kisiasa, mikoa ya Kusini ni Soweto ya Tanzania

herikipaji

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2016
Posts
1,198
Reaction score
1,369
Mikoa mingi inayopatikana kusini mwa Tanzania iko nyuma kimaendeleo.

Ruvuma, Lindi, Mtwara hii mikoa ni imetengwa na kupuuzwa kwa miaka mingi.

Nitaelezea kwa Ruvuma, mkoa wa Ruvuma makao makuu Songea hakuna chuo cha elimu ya juu hata kimoja, vilivokuepo vyote vilifungiwa na ikawa mwisho wake.

Yanayotokea huko mengine yanastaajabisha.

Kata ya Tanga manispaa ya Songea uchaguzi mkuu 2015 walichagua upinzani kwa nafasi ya udiwani.
Yule diwani alikuja kujiunga na upande wa chama kilicho madarakani kwa sasa.

Alikuwa kati ya viongozi wa kwanza kujiunga kwa kudai kuunga juhudi. hii ilisababisha tafrani kubwa kwa wakazi wa huko.

Kwa kua watu walichagua upinzani wakaambiwa sasa mtaona cha mtemakuni kimaendeleo mtatengwa adi mtapojirekebisha yani wachague wale wa chama kilicho madarakani.

Sasa kuna mtaa ambapo yule diwani anatoka umeme umewekwa kata nzima isipokua hapo tu kwenye huo mtaa wameruka lakini ilipokaribia uchaguzi mkuu 2020 wiki moja kabla walileta wafungwa kuekea nguzo wakidai wanafunga umeme hii ilikua zuga sababu adi leo hakuna huo umeme na wanaambiwa tunawakomesha, sababu walichaguaga diwani kutoka upinzani mwaka 2015 ambae nae alijiunga na ule upande wa chama kinachotawala 2017.

Kosa la hawa watu ni nini?

Hii mikoa imekosa maendeleo miaka mingi sehemu nyingi hakuna hata umeme, maji, hospitali etc. Wameleta umeme lakini nao unawekwa kwa ubaguzi hawa watu wanapandikizwa chuki kwa lazima hilo muelewe.

Yale ya Soweto miji iliopuuzwa, iliotengwa kimaendeleo sababu walikua wanaishi watu weusi kule Afrika ya kusini, yanatokea na Tanzania.

Afrika ya kusini ulikuwa ubaguzi wa rangi uliofanywa na makaburu, Tanzanaia ni ubaguzi wa kisiasa unaofanywa na watu wanaofikiri taifa hili ni mali ya chama chao.
 
Wewe unaongelea Tanga kata Ruvuma, Huko ni maporini kama mapori mengine ya Tanzania

Je, Lizaboni, Majengo, Mahenge, Makambi hakuna umeme?

Kila nchi ina vijiji hata Marekani kuna vijiji havina umeme na lami wanatumia Solar power

Ruvuma hasa hapo Songea pameendelea sana huwezi linganisha na Singida, Dodoma au Manyara

Wewe hujatembea nchi hii, Songea kuna maji ya kutosha, Huduma za afya bora na umeme wa kutosha kwa sasa, kuna kila aina ya vyakula hapo ili uwe na afya bora

Nenda Dodoma ukaone maji ni shida hakuna mfano, Kila kitu kimepelekwa Dodoma lakini bado hapabebeki

Huko kata ya Tanga ni Songea vijijini taratibu Mtakuja kupata huduma

Hata Dar es Salaam kuna mitaa kama Buguruni, Mwananyamala, Sinza na mingine mingi ni hovyo huwezi kuishi mtu smart

Ni shida kila kona hapo Dsm maji ya shida kwenye madumu, uchafu kila kona mpaka mlangoni

Songea na Mtwara ni miji imepangwa

Mtwara mitaa kama Ligula, Raha Leo au Shangani pamepangwa kuliko mkoa wa mbeya

Mbeya mitaa kama kalobe, Iwambi, Nzovwe kufika gari nyumbani kwako tu ni shida

Hiyo ni mifano kidogo tu

mkoa wa Mbeya ni hovyo yaani slam huwezi linganisha na Mtwara au Ruvuma
 
Siasa za awamu hii ni za kishamba sana, watu wabinafsi utadhani hizo pesa za maendeleo wanazitoa mifukoni mwao kumbe ni pesa za walipa kodi.
Zimewanyoa vipara kwa chupa watoto wa kubana pua mmebaki kuhangauka.
Komaeni kama wanaume msilielie.
 
Uwenda labda hulka za watu wa huko hasa viongozi awachangamkii fursa.
Kusini ilishatoa Rais,mawaziri pia wabunge.
Embu kumbuka fast lady wa awamu ya tatu alivyoitumia Ikulu vizuri kunufaisha watu wa jamii yake pamoja na kwao.
Awamu ya nne fast lady ni wa kusini sidhani hata kijijini kwao tu alipotoka kama alipajali.
Embu fikiria siku Rais awe mchaga wa kilimanjaro,kwa jinsi walivyo wachaga kaskazini itakuwa half europe.
Kila jamii ina asili yake na mambo yake.
 
Mleta mada hebu tuambie:-
= Kutokuwepo kwa Chuo Kikuu kuna vijana wamekosa Elimu ya Chuo Kikuu? na iwapo hoja yako ni muhimu hebu tuambie mikoa ya magharibi (kigoma, tabora na katavi) kuna Chuo Kikuu?
 
Kusini msijione mko wenyewe, hata kaskazini kuko hivyo tena wao waliambiwa live 'wasubiri'! Hii awamu ni sheedah! kanda pendwa ndio wanaangaliwa zaidi kwa sasa.
 
Uwenda labda hulka za watu wa huko hasa viongozi awachangamkii fursa.
Kusini ilishatoa Rais,mawaziri pia wabunge.
Embu kumbuka fast lady wa awamu ya tatu alivyoitumia Ikulu vizuri kunufaisha watu wa jamii yake pamoja na kwao.
Awamu ya nne fast lady ni wa kusini sidhani hata kijijini kwao tu alipotoka kama alipajali.
Embu fikiria siku Rais awe mchaga wa kilimanjaro,kwa jinsi walivyo wachaga kaskazini itakuwa half europe.
Kila jamii ina asili yake na mambo yake.
Mkuu, K'njaro kwa kiasi kikubwa huchangia maendeleo yao wenyewe bila kusubiri serikali. Migombani watu huchanga fedha kwa ajili ya kusafisha na kutengeneza barabara za ndani kwa ma-catapiller ya kukodisha! Umeme wa REA uchagani umekuta watu walishajiwekea umeme vijinini kwa kuchangishana! Maji nayo hivyohivyo! X-mass mnayoona watu wanakwenda kutambikia ndio kipindi cha kusemana, kukosoana na ikiwezekana kuchekana kama wewe ni mvivu, huangalii kwenu, hujengi, huendelezi au unaendekeza starehe tu! Je vipi kwenu?
 
Mwanzo wa comment yangu hapo nimeandika hivi"uwenda ni hulka za jamii ya huko" na mwisho wa comment yangu pia nimeandika hivi"kila jamii ina asili yake na mambo yake"

kuna jamii zipo radhi walale njaa lakini ni lazima wacheze ngoma za kila mwaka,awapo radhi kujinyima na kulala njaa kwaajili ya maendeleo iwe ya elimu,afya n,k.

mchaga anapenda maendeleo yake,kwao na jamii yake,hii ni hulka ya wachaga na baadhi ya makabila mengine machache hapa TZ.
kuna mambo yanaendana na asili ya jamii ya watu,piga uwa uwezi kukuta tofauti.
 
Back
Top Bottom