Jinikashkash
JF-Expert Member
- Nov 27, 2020
- 455
- 871
Daraja la Busisi kule Misungwi kuelekea nyumbani kwa Mutukufu ni la tsh 700 BILLION ,mikoa yenu yote haina mfano hata mmoja Kama huuMikoa mingi inayopatikana kusini mwa Tanzania iko nyuma kimaendeleo.
Ruvuma, Lindi, Mtwara hii mikoa ni imetengwa na kupuuzwa kwa miaka mingi.
Nitaelezea kwa Ruvuma, mkoa wa Ruvuma makao makuu Songea hakuna chuo cha elimu ya juu hata kimoja, vilivokuepo vyote vilifungiwa na ikawa mwisho wake.
Yanayotokea huko mengine yanastaajabisha.
Kata ya Tanga manispaa ya Songea uchaguzi mkuu 2015 walichagua upinzani kwa nafasi ya udiwani.
Yule diwani alikuja kujiunga na upande wa chama kilicho madarakani kwa sasa. Alikuwa kati ya viongozi wa kwanza kujiunga kwa kudai kuunga juhudi. hii ilisababisha tafrani kubwa kwa wakazi wa huko.@Paschal Mayyala
Kwa kua watu walichagua upinzani wakaambiwa sasa mtaona cha mtemakuni kimaendeleo mtatengwa adi mtapojirekebisha yani wachague wale wa chama kilicho madarakani.
Sasa kuna mtaa ambapo yule diwani anatoka umeme umewekwa kata nzima isipokua hapo tu kwenye huo mtaa wameruka lakini ilipokaribia uchaguzi mkuu 2020 wiki moja kabla walileta wafungwa kuekea nguzo wakidai wanafunga umeme hii ilikua zuga sababu adi leo hakuna huo umeme na wanaambiwa tunawakomesha, sababu walichaguaga diwani kutoka upinzani mwaka 2015 ambae nae alijiunga na ule upande wa chama kinachotawala 2017.
Kosa la hawa watu ni nini?
Hii mikoa imekosa maendeleo miaka mingi sehemu nyingi hakuna hata umeme, maji, hospitali etc.
Wameleta umeme lakini nao unawekwa kwa ubaguzi hawa watu wanapandikizwa chuki kwa lazima hilo muelewe.
Yale ya Soweto miji iliopuuzwa, iliotengwa kimaendeleo sababu walikua wanaishi watu weusi kule Afrika ya kusini, yanatokea na Tanzania.
Afrika ya kusini ulikuwa ubaguzi wa rangi uliofanywa na makaburu, Tanzanaia ni ubaguzi wa kisiasa unaofanywa na watu wanaofikiri taifa hili ni mali ya chama chao.
Kwa sasa huwezi abadan kufananisha kimaendeleo ya vitu Chatto na Songea ,Lindi wala Mtwara miji iliyokuwepo hata kabla Karl Peters hajazaliwa
Mlie tuu 'mitano tena', au nasema uongo ndugu zangu?